live on
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 772
- 1,249
Hapa maeneo ya Kamata kuna hawa jama sijui tuwaite mgambo wa jiji au sijui polisi jamii hata sielewi.
Wakikuona umeshuka katika daladala na tiketi yako mkononi au umenunua maji ukafungua kizibo wanaanza kukufuata kwa nyuma nyuma maana wanajua tu lazima utakiangusha na pia eneo lote la Kamata jiji hawajaweka dustbins ukiangusha tu hiyo ticket wanakukamata hadi uwapose ndio wakuachie.
Lakini pia kinacho shangaza hii ofisi ya jiji ya hapa Kamata wanajua uwepo wa hawa jamaa na wanabariki kwa yote wanayoyafanya.
Kuna siku mdada mmoja aliweka chupa yake ya maji chini ili aweke vizuri vitu vyake akaja mmoja akayamwaga Yale maji kisha akamwambia dada umetupa uchafu twende ofisi za jiji yule Dada akamwambia haya twende.
Alipofika ofisini akaambiwa Dada unachafua jiji faini elfu 50 kama huna unaenda sero.
Yule Dada akawambia huyu kijana wenu ni tapeli amemwaga maji yangu kisha ndio akaniambia nimetupa chupa ya maji nachafua jiji, haya maji ameninulia mume wangu trafiki yupo hapo darajani hata dk 10 bado hazijapita kama vipi nimpigie simu aje hapa walivyosikia hivyo wakamuachia akaondoka.
Sasa jiulize watu wangapi kwa siku wanaumizwa kwa dizaini hii.
Kwanini hawa jiji wasiweke dustbins ili eneo la Kariakoo Kamata badala yake wanawatuma watu wakafanye utapeli kwa kisingizio cha usafi wa jiji.
Sent using Jamii Forums mobile app