Hapa Kariakoo maeneo ya Kamata watu wananyanyaswa sana na Mgambo wa Jiji

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
496
1,000
Hapa maeneo ya Kamata kuna hawa jama sijui tuwaite mgambo wa jiji au sijui polisi jamii hata sielewi.

Wakikuona umeshuka katika daladala na tiketi yako mkononi au umenunua maji ukafungua kizibo wanaanza kukufuata kwa nyuma nyuma maana wanajua tu lazima utakiangusha na pia eneo lote la Kamata jiji hawajaweka dustbins ukiangusha tu hiyo ticket wanakukamata hadi uwapose ndio wakuachie.

Lakini pia kinacho shangaza hii ofisi ya jiji ya hapa Kamata wanajua uwepo wa hawa jamaa na wanabariki kwa yote wanayoyafanya.

Kuna siku mdada mmoja aliweka chupa yake ya maji chini ili aweke vizuri vitu vyake akaja mmoja akayamwaga Yale maji kisha akamwambia dada umetupa uchafu twende ofisi za jiji yule Dada akamwambia haya twende.

Alipofika ofisini akaambiwa Dada unachafua jiji faini elfu 50 kama huna unaenda sero.

Yule Dada akawambia huyu kijana wenu ni tapeli amemwaga maji yangu kisha ndio akaniambia nimetupa chupa ya maji nachafua jiji, haya maji ameninulia mume wangu trafiki yupo hapo darajani hata dk 10 bado hazijapita kama vipi nimpigie simu aje hapa walivyosikia hivyo wakamuachia akaondoka.

Sasa jiulize watu wangapi kwa siku wanaumizwa kwa dizaini hii.

Kwanini hawa jiji wasiweke dustbins ili eneo la Kariakoo Kamata badala yake wanawatuma watu wakafanye utapeli kwa kisingizio cha usafi wa jiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,080
2,000
Tuache ujinga muda mwingine. Jiji haliwezi kuwa safi kwa kutumia vilaza hao kudhibiti uchafu, suala la usafi ni la kimkakati sio kutumia watu wenye ufinyu wa akili hao.

Kwenye stand za magari hakuna dust bin barabarani hakuna dust bin kisha unatumia nguvu kuweka jiji safi!!?
 
G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,416
2,000
Ni upumbavu wa ajabu wanafanya, siku walinikamata miataa ya Hindu Mandal,
Nikajifanya sijui kiswahili" walitaka wanipeleke jiji nikajifanya hata siwaelewi nikamuita muhindi ni kawa namuuliza kama kuna kituo au polisi karibu kwamba nahisi hawa jamaa ni wezi.

Walipotea ktk mazingira ya kutatanisha, Nikaondoka zangu".Sent using Redmi Y2
 
double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,367
2,000
Ukitaka kupima uwezo wetu wa kutatua matatizo ni hapa.
Wakati kamata wanakamata watupa vifunuko na tiketi, msimbazi wamejaa machinga barabarani na takataka zimezagaa, umbali wa kilometa 1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,241
2,000
Tuache ujinga muda mwingine. Jiji haliwezi kuwa safi kwa kutumia vilaza hao kudhibiti uchafu, suala la usafi ni la kimkakati sio kutumia watu wenye ufinyu wa akili hao.

Kwenye stand za magari hakuna dust bin barabarani hakuna dust bin kisha unatumia nguvu kuweka jiji safi!!?
Eti tunaliita JIJI hata public toilets hakuna,Dustbins bado ni ndoto,tembelea hapo Malaysia(nchi ambayo tulilingana nayo kiuchumi miaka ya 70s,unaona hata aibu kutema mate chini,nchi imerambwa safi),tembelea mji mkuu wa Namibia utapenda ulale siku Zima kwenye zile bustani zake,zipo safi,salama na zimetulia,township ya katutura ni safi mno kuliko masaki yetu.
 
cordoba

JF-Expert Member
Jul 15, 2017
737

Nipo katututura hapa aisee slums za Namibia ni nzur kukiko osterbay

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NDUKI

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
3,229
2,000
Wanakuwa na vitambulisho vya jiji au hata vitambulisho hawana...?
 
Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,730
2,000
Wale jamaa ni matapeli yani mimi sioni tofauti kati ya vibaka waporaji na wale jamaa isipokuwa ni kwamba wale wanatumia kivuli cha jiji kufanya uporaji wao

Pale kamata ubavuni katika lile jengo lenyewe la kamata kuna kikalo Fulani kimeja uchafu kuna mataili mabovu na uchafu mwingine

Kuna dada mmoja alikuwa anapita na juice yake ilipoisha ile chupa akaitupia mle wale jamaa wakamchukua kwa madai eti anachafua jiji sijui wakaenda kumchomoa shilingi ngapi

Sasa mimi nikajiuliza hili kalo limejaa uchafu yani ni kama shimo la taka kama wao wanataka jiji liwe safi kwa nini hawasafishi likawa safi wakafunika vizuri

Ila baadae nikagundua kumbe pale ndio sehemu yao ya mawindo yani pale hawaondoki wanavizia watu wanaotupa taka katika lile kalo na hilo shimo jinsi lilivyo kama una kitu mkononi cha kutupa lazima tu utakitupia mle maana halina tofauti na shimo la taka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
496
1,000
Wanakuwa na vitambulisho vya jiji au hata vitambulisho hawana...?
Matapeli tu vitambulisho vya jiji wapate wapi

Ukipita mida ya saa 1 jioni utawakuta nje pale ofisi za jiji kamata ndio wanagawana pesa zao hadi ngumi wanapigana sasa sijui wanakuwa wamezurumiana wenyewe kwa wenyewe yani kwa kweli ni shida ila lazima kutakuwa na mtu wa jiji wanakula nae mapato ya dhuruma wanayofanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
2,862
2,000
Hapa maeneo ya Kamata kuna hawa jama sijui tuwaite mgambo wa jiji au sijui polisi jamii hata sielewi.

Wakikuona umeshuka katika daladala na tiketi yako mkononi au umenunua maji ukafungua kizibo wanaanza kukufuata kwa nyuma nyuma maana wanajua tu lazima utakiangusha na pia eneo lote la Kamata jiji hawajaweka dustbins ukiangusha tu hiyo ticket wanakukamata hadi uwapose ndio wakuachie.

Lakini pia kinacho shangaza hii ofisi ya jiji ya hapa Kamata wanajua uwepo wa hawa jamaa na wanabariki kwa yote wanayoyafanya.

Kuna siku mdada mmoja aliweka chupa yake ya maji chini ili aweke vizuri vitu vyake akaja mmoja akayamwaga Yale maji kisha akamwambia dada umetupa uchafu twende ofisi za jiji yule Dada akamwambia haya twende.

Alipofika ofisini akaambiwa Dada unachafua jiji faini elfu 50 kama huna unaenda sero.

Yule Dada akawambia huyu kijana wenu ni tapeli amemwaga maji yangu kisha ndio akaniambia nimetupa chupa ya maji nachafua jiji, haya maji ameninulia mume wangu trafiki yupo hapo darajani hata dk 10 bado hazijapita kama vipi nimpigie simu aje hapa walivyosikia hivyo wakamuachia akaondoka.

Sasa jiulize watu wangapi kwa siku wanaumizwa kwa dizaini hii.

Kwanini hawa jiji wasiweke dustbins ili eneo la Kariakoo Kamata badala yake wanawatuma watu wakafanye utapeli kwa kisingizio cha usafi wa jiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni wasanii wa mamlaka ya kodi ART

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom