Hapa jukwaani kuna vituko! hata kama una siku mbayw utatabasamu

Aisee mie hiyo ya kucheka mwenyewe hunitokea sana tu. Kuna watu wanajua sana kucheza na maneno humu yaani ukisoma unabaki na kicheko cha hali ya juu. JF ni burudani tosha halafu kwenye idara ya habari hapa ni mwisho. Huwezi amini saa nyingine nikisikia kitu kimetokea ndani au hata nje ya nchi sehemu ya kwanza kukimbilia ni hapa JF na si mahali pengine popote pale, na mara nyingi JF huwa hainiangushi. Idumu JF na mashetani na dhana yao washindwe kabisa.
Ha hahaha hapa tu umeshanichekesha kweli mashetani washindwe...
Tuko sawa katika hilo nikisikia tetesi huwa nawahi kufungua JF nione kuna nini... Mungu awabariki waanzilishi.
 
Humu ndani ni burudani hadi raha, kuna thread kaanzisha miss natafuta ya kuasili mtoto, sasa akawa anajibizana na somebody Nokia, yale majibizano kila nikikumbuka siiishiwi tabasamu usoni
 
duu kama ndo keshawekewa matairi tayari basi pole yako majaliwa na kumpata hata hilo kabulri lake au vinasaba vyake nayo pia ni majaliwa
 
Back
Top Bottom