Hapa Jk Alimaanisha Nini?

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
409
30
Akiongea na wazee wa Dar-es-salaam pamoja na mambo mengine Rais alisema
"Ni kweli kwamba kwa muda wa wiki nzima nchi yetu na hasa siasa na uongozi wa Taifa letu vimepata mtikisiko mkubwa. Ni hali ambayo hatukuitegemea. Imetustukiza, tumefanya maamuzi ambayo hatukuyapanga na kupata matokeo ambayo hatukuyategemea"Baada ya kufuatilia mjadala Bungeni siku iliyofuata na kusikiliza hisia za watu nchini ndipo tukafikia kwenye maamuzi yale magumu na mazito tuliyofanya. Maamuzi ambayo yalipelekea kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri. Ni maamuzi magumu, lakini yalikuwa hayana budi kufanyika kwa maslahi ya utangamano wa taifa letu.Ni uamuzi mgumu kwa sababu unawahusu watu ambao ni wenzangu wa karibu kimaisha na kikazi kwa miaka mingi. Na pia kwa sababu unaona wazi kuwa kama mambo fulani fulani yangefanyika mambo yasingefikia kuwa yalivyo

Nianze na sehemu hii niliyoweka mlalo.Je,matokeo ambayo hakuyatarajia ni yapi? mmh hapana kabla ya swali hilo,kipi kilimstukiza hadi akapelekea kufanya maamuzi ambayo hakuyapanga? Nimetafakari sana kauli hii na kujiuliza,ina maana ni kweli Rais hakuwa anaona upepo wowote wa uovu ndani ya baraza lake?au je,kelele zote zilizokuwa zikipigwa na miito mbalimbali kuhusu richmonduli hakuwa anazisikia au je,zilikuwa zinaingilia sikio moja na kutokea jingine?Na hayo mambo fulani fulani ambayo yangefanyika ni yapi? Nadhani kuna haja ya kumwangalia na yeye iwapo alikuwa na nafasi yoyote kwenye richmonduli.eti wadau ninyi mwaonaje?
 
Nianze na sehemu hii niliyoweka mlalo.Je,matokeo ambayo hakuyatarajia ni yapi? mmh hapana kabla ya swali hilo,kipi kilimstukiza hadi akapelekea kufanya maamuzi ambayo hakuyapanga?

My take ni kuwa Ikulu wanataka kuonyesha kuwa kujiuzulu kwa Lowassa ni uamuzi uliofikiwa na Lowassa mwenyewe bila hata ya kumhusisha Kikwete.Hata Lowassa amelipigia mstari hili kwamba zaidi ya mke wake hakukuwa na mwingine yeyote aliyejua hili.Kilichomstukiza ni Lowassa kuomba kujiuzulu, Maamuzi ambayo hakuyapanga ni kukubali Lowassa ajiuzulu.

Kikwete anataka kula keki yake halafu bado ibaki mezani.Anataka kumuondoa Lowassa ili kujisafisha na kupandisha imani ya wananchi juu ya serikali, lakini hapo hapo hataki kumuudhi Lowassa na watu wake.Sasa baada ya kuuma anapuliza.


Nimetafakari sana kauli hii na kujiuliza,ina maana ni kweli Rais hakuwa anaona upepo wowote wa uovu ndani ya baraza lake?au je,kelele zote zilizokuwa zikipigwa na miito mbalimbali kuhusu richmonduli hakuwa anazisikia au je,zilikuwa zinaingilia sikio moja na kutokea jingine?Na hayo mambo fulani fulani ambayo yangefanyika ni yapi? Nadhani kuna haja ya kumwangalia na yeye iwapo alikuwa na nafasi yoyote kwenye richmonduli.eti wadau ninyi mwaonaje?

Tatizo ni kuwa Kikwete kwa kiasi kikubwa hajali uovu ndani ya baraza na anaweza kuwa influenced kirahisi na watu wake.Kikwete anajali public opinion kwa sababu hana performance na anategemea popularity, sasa mwanzo alifikiri issue inaweza kuzimwa ndiyo maana hakujali sana, baada ya kuona issue ni kubwa na haiwezi kuzimwa akamtoa Lowassa katika zoezi zima la kujisafisha.

Unajua kuna maneno yameongewa katika kamati yanaonyesha kuwa mradi wa Richmond ulikuwa wa "wakubwa" siyo "mkubwa" kwa hiyo siwezi kushangaa nikisikia Kikwete naye anahusika ila kamtoa mshkaji wake kafara na anamtafutia mbinu ya kumsafisha, otherwise kama Kikwete angekuwa serious kuhusu rushwa na mismanagement Lowassa asingeongea kwa kutumia TVT na wala Kikwete asingempamba kwenye hotuba na wazee wa Dar.
 
Back
Top Bottom