Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 31
Akiongea na wazee wa Dar-es-salaam pamoja na mambo mengine Rais alisema
"Ni kweli kwamba kwa muda wa wiki nzima nchi yetu na hasa siasa na uongozi wa Taifa letu vimepata mtikisiko mkubwa. Ni hali ambayo hatukuitegemea. Imetustukiza, tumefanya maamuzi ambayo hatukuyapanga na kupata matokeo ambayo hatukuyategemea"Baada ya kufuatilia mjadala Bungeni siku iliyofuata na kusikiliza hisia za watu nchini ndipo tukafikia kwenye maamuzi yale magumu na mazito tuliyofanya. Maamuzi ambayo yalipelekea kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri. Ni maamuzi magumu, lakini yalikuwa hayana budi kufanyika kwa maslahi ya utangamano wa taifa letu.Ni uamuzi mgumu kwa sababu unawahusu watu ambao ni wenzangu wa karibu kimaisha na kikazi kwa miaka mingi. Na pia kwa sababu unaona wazi kuwa kama mambo fulani fulani yangefanyika mambo yasingefikia kuwa yalivyo
Nianze na sehemu hii niliyoweka mlalo.Je,matokeo ambayo hakuyatarajia ni yapi? mmh hapana kabla ya swali hilo,kipi kilimstukiza hadi akapelekea kufanya maamuzi ambayo hakuyapanga? Nimetafakari sana kauli hii na kujiuliza,ina maana ni kweli Rais hakuwa anaona upepo wowote wa uovu ndani ya baraza lake?au je,kelele zote zilizokuwa zikipigwa na miito mbalimbali kuhusu richmonduli hakuwa anazisikia au je,zilikuwa zinaingilia sikio moja na kutokea jingine?Na hayo mambo fulani fulani ambayo yangefanyika ni yapi? Nadhani kuna haja ya kumwangalia na yeye iwapo alikuwa na nafasi yoyote kwenye richmonduli.eti wadau ninyi mwaonaje?