Hapa dsm wanafunzi wengi wanaishia Kupata zero form four je Serikali inalitambua hili?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,883
45,248
Nipo shule x Hapa dsm nasikitika kusema Kuna zaidi ya watoto wa kike 100 lazima wapate zero maana naandika Hapa hawa Ni watoto hawajui hata kuandika majina yao kwa ufasaha.

Sasa hawa watoto wa kike wengi wanatoka uswahilini je baada Kupata zero wanaenda kufanya shughuli gani au kuolewa na !!!!


Afisa Elimu wa dsm ebu Fanya Kazi yako acha siasa uchwara.
 
Hilo serikali inalifahamu, tena kwa muda mrefu tu

Wale kwa urefu wa kamba yao.
 
Jamaa inchi imeshawashinda hii. Kuendelea kuwaacha na kuwatazama wakikazana na tambo za kisiasa, kuongea uongo na ahadi zisizotekelezeka ni national sabotaging kwa vizazi vijavyo.

Hebu tulitazame hili kizalendo na tuamue mfumo mpya wa kuliongoza taifa hili.

CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuiendesha hii inchi kwa miaka 50 ijayo ila uzembe katika kutengeneza viongozi bora ndio inawagharimu.

Wanaweka vijana waongeaji tu. Siasa wao wanaitazama kama usuperstar na sehemu ya kupatia pesa na sifa za kujulikana badala ya kuitazama kama kazi ya wito na ya kujitoa kwa jasho na akili raia wawe na maisha mazuri.

Tazama vijana wengi wanaowekwa wanakuwa ni empty kabisa vichwani. Wanaona siasa kama michezo michezo ya kukimbizana na wapinzani, kuongea ongea kwa mikwara kwenye media, kusifia viongozi wakubwa. Sasa hawa kesho ndio washike taifa kuliongoza kuelekea wapi sasa.
 
Back
Top Bottom