Hapa CHADEMA mmeingia kichwakichwa, hii inaitwa force king! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hapa CHADEMA mmeingia kichwakichwa, hii inaitwa force king!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENDAHAKI, Sep 1, 2012.

 1. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Siasa ni mchezo mzuri sana ambao umejaa maigizo na vituko, mbwembwe na visa, Fitna na majungu lakini pia Ujuzi na umakini wa hali ya juu mno kuliko DRAFT!Kila kauli kwenye siasa ina maana sana!Kabla mtu hajagundua adui yake ninani hawezi kuwa salama na hata katika siasa ni hivyo hivyo; Yaani kama hujaambiwa mapungufu yako kabla hujaingia kwenye uchaguzi basi ujue una wakati mgumu sana kujua utakumbana na changamoto gani! Ndio maana namuona SAMUEL SITA kama mtu makini sana kwenye siasa !Nasema hivi kwa sababu naanza kuamini kuwa ana nia ya kweli ya kutaka kugombea urais. Awali nilijua ni mpambanaji tu ndani ya CCM hasa baada ya kukosa uspika!Kumbe hapana alikuwa akiwachokonoa wenzake wamwambie mapungufu yake ndani ya chama chake. Baada ya mivutano ya muda mrefu ndani ya ccm Sita anaona kama ameshinda vita ndani ya chama chake ndio maana ameamua kuhamishia vita kw wapinzani wake wakuu yaani CHADEMA kwa kuwachokonoa makusudi ili wamwambie mambo yanayoweza kuwa kikwazo kwake,bomu kwake na pingamizi katika kupata ridhaa ya kuongoza nchi iwapo chama chake kitamuamini kwenye nafasi ya kuwa mgombea urais!NI wazi kuwa CHADEMA hupata uungwaji mkono mkubwa wa wananchi kutokana na style yao ya kuumbua madudu ya wapinzani wao na ni wazi kutokana na siri nyingi walizokuwa nazo CHADEMA juu ya SITA ingekuwa rahisi kummaliza kama angeteuliwa na chama chake hapo baadae bila kujijua anaweza kukabiliana na nini! Ndio maana nasema kwa hili chadema mmeingia mkenge!USHAURI WA BURE ni kujibu maswali mliyoulizwa tu au kuuliza yale mliyopanga kuuliza na sio kucheza "MUZIKI WA SITA"!waache CCM waucheze mziki wenu na sio kinyume! HII INAITWA FORCE KINGI style maarufu kabisa kwenye drafti!LA sivyo mnasafisha njia ya mtu tu!
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  SITTA , mziki mwingine, hawa CDM wanajikanyaga tu hawana cha kusema juu ya SITTA.
   
 3. Malcom Lumumba

  Malcom Lumumba JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 4,836
  Likes Received: 8,187
  Trophy Points: 280
  ila wadau yule mzee siyo mjinga kama wanavyodhani kawatega na wenyewe hawajajua atakuja na nini.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Atakuja na issue ya mwakyembe kuwekewa sumu
   
 5. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Angalia walivyoharakisha kumjibu,halfu yeye kakaa kimya tu anawasikiliza!akirudi atakuja na lingine tena ili waendelee kupa mwanga wao!Mwishowe cdm watakosa cha kumlipua wakati watakapohitaji sana
   
 6. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  He he he, wapo baa saa hizi wanamalizia, subiri wakiingia humu ndugu yangu utajuta na mitusi yao hasa yule dada wa jimbo letu .....Mie naishi Mlalakuwa.
   
 7. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  kazikubwa sijakuelewa kaka!
   
 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sita sio makini hata chembe.Bado kapu la Cdm halijatema.Yy akija tena ndio itakuwa basi
   
 9. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Acha tusubiri tuone!nini mwisho wake
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ha ha ha sita ndio uwezo wake umefikia mwisho ni mnafiki mtu anaye taptapa na chadema wana mambo yake mengi sana kwa haya machache yanatosha kumtambua 6 ni mtu wa namna gani ila kapewa kubwa sana sijui ana hali gani saizi, au uenda wamewasiliana na dk slaa wanaambiana sasa mbona umenimaliza kabisa ha ha ha yan ni burudani sana
   
 11. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wabongo bado tuna kazi ngumu saa mbele, Wewe waamini 6 anaweza kuongoza nchi hii kweli? jamani tuacheni ushabiki wa kishamba, mwaka jana nilibahatika kwenda jimboni kwa ndugu 6 ambaye amekuwa kiongozi toka mimi sijaanza dalasa la kwanza miaka kama ishirini na tano iliyopita lakini maendeleo ya Urambo ni aibu tupu, Kimsingi sisi wanyamwezi hatuwezi kuongoza labda familia zetu, mifano hai Prof Kapuya, Prof Lipumba, Eng Msekela, yule prof aliekuwa mbunge kabla ya kaboyonga,,,,,,,...............na wengine wengi, Sita siwezi kumpa kura yangu hata kama nipo usingizini
   
 12. O

  Original JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sita ni kigeugeu na ana tamaa sana ya madaraka. CCM wanalijua jilo na sasa Chadema pia wanalijua hilo. Dawa ni kumfukuza kutoka ccm na chadema wasimchukue akitaka aende cuf.
   
 13. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Mr. suggestion unadhani ni watanzania wangapi wanawaza kama wewe!labda ukiniambia Marais walioita walifanya nini kwao nitakuelewa!Kama kumbukumbu zangu ziko sawa hata kwa hayati Mwalimu mpaka leo kuna tatizo kubwa la usafiri, maji na umeme!"Kiongozi bora sio yule anayetazama kwao tu bali yule asiyetelekeza kwao"
   
 14. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Matendo yake hayaonyeshi werevu wake.
   
 15. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  hizi conspiracy theories ni udhaifu wa mtoa mada kushindwa kubali hali halisi mzee kajisahau,kwa vile bado ana positive view juu ya huyu mzee .Pengine hii ndio itakuwa nafasi ya kupata ushauri wa kuligeuza hili kuwa kama mwandishi anavyotaka liwe.Lakini bado tatizo linabaki kuwa mzee hana uwezo wa ku tap any benefit hapa.

  Kwa waliobahatika sikiliza hotuba yake bungeni alivyowaita"... wapinzani wana mambo ya uchonganishi..." na ujinga mwingine ndio wataona uozo uliokuwa umefichwa kichani kwa mzee.Mzee alikuwa na hasira na CDM,baada ya kukosa kupewa assurance ya kugombea urais. Mzee aliwaita wapinzani majina ya kebehi kipindi ambacho wapinzani walikuwa wakifanya mambo ya ukweli bungeni.Alipata support ya magamba wachache wale wa "...ndioooo" ila wengi walimzomea kwa vile waliona kaongea kitoto.

  Kwa ujumla mzee yupo too Naive, mwoga na kalewa na visifa fulani akiwa spika sasa yeye kafanya kuwa "NOBEL PRIZE" kwani yenyewe ndio ina lifelong legacy.Na washindi huwa ni watu wenye integrity na wenye kupambana ku maintain. Mzee hajui kuwa ukishaingia katika harakati za ukombozi basi wapiganaji wenzio lazima uhakikishe nao wanpata haki na ulinzi.Mzee kwa sababu hana vision na ana swing kama wiper basi njaa zinampeleka kila palipo na matambiko.Hajui matambiko mengine yanakinzana na ni mikataba.

  Mimi naweza sema mzee kamwita Mbowe DJ, ila ki ukweli mzee mimi kwa ujasiri mkubwa namwita "mcheza disco" asiyelala usiku kucha akitembelea madisco mbalimbali.This time anacheza disco la EL,CDM,Mbowe,sasa la SLaa, Membe na wengine.Mzee 6 anacheza disco ambalo hajalipia ndio maana ni mwoga kupindukia. Natamani nimwekee Picture ya E.L katika wallet asipate usingizi, akapige ramli.

  Wanaodhani kuwa CDM wanamsadia EL wamechemka sana,hiyo ni coincidence too na pia katik chama itampa EL adavantage kwani kashfa za huyu "dancer" zitakuwa useless kila mahali.Kw aujumla hataaminika tena kwa lolote na raia.sasa kila aliysemwa na huyu mzee atakuwa na ahueni.Kwani credibility inaelekea kuwa kushney.

  CCM wamechemka mambo mengi sana.Mojawapo ni kwamba kama walitaka kumsimamisha mh E.L kwanini walirisk kiasi kiasi hicho kumchafua?Kuna tofauti gani na mtu aliyejitwisha kitanzi na halafu wakati anaelekea kufa ndipo anakumbuka kuwa nahitaji kutokufa wakati hana tena uwezo?Kwa watanzania wasioaimini serikali hadi hawaoni umuhimu wa sensa, ni vipi wataiamini serikali inapotaka wabadilisha imani yao kuwa mh .E.L anahusika na ufisadi? Its easier now mtu yoyote akasema akagmbea na EL na kutumia neno "ufisadi "kwa faida,kuliko the whole CCM machinery kuaminisha watu kuwa Mhe si fisadi.Big Blunder kwa ccm.Walitaka ya Zuma,sasa watahitaji mtoa kafara mtu mkubwa kabisa serikalini ili abebe mzigo.Kama vile Mungu alivyopaswa toa kafara Kubwa na Safi ili kumlipa shetani madeni yake kwa mwanadamu.Mwanadamu aliingia kichwakichwa katik mikataba na shetani halafu baadaye ikawa haitekelezeki.Na huyu si mwingine Zaidi ya Presidaa.Kwani yeye ndie takuwa na thamani ya kuweza msafisha mh EL.Kitu ambacho kitakuw too complicated na matokeo yake si predictable.Zoezi linaweza kuwa kama chain reaction.CCM are ****ed up.Hata wakiivunja CDM, NCCR wataweza chukua nchi katik mtindo wasioutegemea.Ingawa zoezi la kuivunja CDM ni gumu sana kwani hasira ya wananchi wanaweza msimamisha yeyote katik chama na kashinda urais.
   
 16. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hajafukuzwa aliyekihariibu chama chao mpaka kinaitwa cha mafisadi sembuse huyu shujaa wao!think twice Original
   
 17. m

  mliberali JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 2,888
  Likes Received: 1,518
  Trophy Points: 280
  kushinda kisiasa si lazima kushambulia mpizani wako ingawa inaweza kuwa ni mojawapo ya mbinu, tusikariri , sita anaweza kuitumia hii mbinu isimsaidie vile vile. hali ya kisiasa tuliyo nayo kwa sasa inahitaji facts siyo blablah.. za SITA.. watanzania wana uelewa mkubwa wa mambo tofauti na hawa akina SITA wanavyodhani. hivi SITA akiulizwa ni kwa nini aliuzima mjadala wa Richmondi bungeni atajibu nini??

  Watz wanajua kinachawataabisha na kuwafanya kuwa masikini siyo DISCO LA MBOWE"

  sitegemei mtu kama SITA kujisafishia njia kulekea ikulu 2015 kwa mtindo wa kitoto kama huu.

  Sehemu (Jimbo)alipotolea hiyo kauli ya hovyo inasemekana CDM walishinda ila waliporwa ushindi na CCM.

  kushinda uchaguzi hakutegemei kampeni za kushambuliana (personal attack) kutatokana na nani anajenga hoja madhubuti si uwezo wa kushambuliana hadharani au kurushiana mabomu

  kama hiyo itakuwa ndo mbinu ya Mgombea wa CCM ni vyema CDM wakaepuka mbinu hii, wajikite kwenye facts watawin kirahisi
   
 18. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa mtizamo wangu Dr Slaa hakuwa na lazima ya kumjibu angeendelea tu na mishe. Kwani Sitta c alitoa maoni yake tu,,kwamba CDM hawana kitu isipokuwa labda Slaa?
   
 19. C

  Concrete JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Sitta hakuna kitu tena, anajua hatapata nafasi ya kugombea urais iwe kwa CCM wala Chadema, anachofanya ni kutapatapa tu kwa kufanya siasa za kubahatisha tu, yaani kuuma na kupuliza kila upande, ama Liwalo na Liwe.

  Kisiasa ndio amefika mwisho mwisho, mtu aliyewahi kufikia nafasi ya kisiasa ya juu kama uspika wa bunge tena kwa kuchaguliwa anakuja kuishia kuongoza wizara ndogo kama idara ya serikali tena kwa kuteuriwa, hana jipya tena, hata ubunge wa Urambo anaweza asiupate tena asipojipanga vema.

  Kundi lake la kisiasa ndani ya CCM limepukutika kabisa kila mtu yuko kivyake kivyake huku wakikaa kinafiki kila mmoja akimtegea mwenzie, hakuna wa kumsadia mwenzake maana wote wako kwenye hali mbaya sana.

  Ndugu yake Nape mambo yako shingoni, wazee wa chama wamemshika vibaya wanazidi kumwonya kwa kauli zake mbovu na tata.

  Hao aliokuwa anawaita mafisadi leo hii wamekamata kiti cha spika, kamati za kudumu za Bunge, mawaziri, wajumbe wa Nec na kamati kuu, wako kwenye secretarieti ya chama, wenyeviti wa jumuiya za chama nk.

  Wahenga walisema usitukane mamba ukiwa bado hujavuka mto, kamwaga mboga jamaa nao wamemwaga ugali kinachofuata ni njaa kali ya kisiasa kwa Mheshimiwa Sitta.

  Muziki wa DJ na producer wake sasa ni zamu ya Sitta kuucheza!!
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Makosa ya huyu mzee ni kwamba hakuweka "escape door" ukitaka mchapa paka inabidi umpige kutoke aupande ambao haumzuii paka kukimbia kujiokoa.Sasa ukimzuia ili asikimbie basi unatafuta apambane na wewe mojakwa moja na mwishowe utatamani wewe ndio upate njia ya kutoka ila hutakuwa na hiyo nafasi labda aje kuokoa mtu mwingine.Kwani baadaye kila kiungo cha miwli kikijigusa atahisi unataka kiweka juu yake.Na hivyo kukutaka ugande tuu.

  SIta hakuweka escaping doors kwa ajili yake na CDM.Hapa lazima Dr.Slaa akatae hili, kwani angekaa kimya angeonekana kuwa "kufururahia sifa", pia angekuja jutia siku inafikia zamu yake kuporomoshewa hayo.Hatopata tena mtu mwenye credibility wa kuyasema yake jukwaani.Yaani imagine mbowe akiingia jukwaani kumtete Dr. kipindi ambacho watu wameshamin k uwa ni DJ, 6 atasema kirahisi tuu DJ anajua nini?


  Watu wazima wenye akili wakijamba katika umati vibaya,basi hutafuta nji asahihi za kulipotezea huku akiwapa watu ahueni, kwani itakuwa rahisi wao kutolifanya issue, na hivyo mzee kuponea hapo.Ila mijizee mipuuzi huwa itaanza singizia mtu, itashikilia bango mwisho watoto watasimamia kweli,watathibitisha jizee limejamba,watathibitisha ni liongo, watathibitisha lina roho mbaya ya kusingizia watoto,watathibisha ni kandamizi, etc.

  6 kanichosha,kanifanya niondoe hata ile mitazamo yangu juu yake kama mtu makini
   
Loading...