Hanstone kinachomkwamisha ni kiburi au wanamsingizia na kumuonea?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Huyu kijana wa Banza Stone Hanstone ninaamini ana kipaji kikubwa sana. Ameonesha uwezo mkubwa sana kwenye wimbo wa Iokote alioshirikishwa na Maua Sama, na hatimaye nyimbo zake mbili ailizozitoa hapo baadaye za acha lipite na I miss you mama. Pamoja na kwamba hizo nyimbo mbili alisema hazikuwa rasmi lakini zilituvutia wengi na kuona ni kijana mwenye bright future kwenye muziki.

Basi mambo yakawa mambo akajitoa kwenye management aliyokuwepo ya kina Abbah na Hanscana na kutokomea kusikojulikana. Ni zaidi ya mwaka sasa hajulikani yupo management gani, wapo waliosema yupo kwa S2kizzy na wengine wakasema anaandaliwa kuingia wasafi, wapo pia waliosema yupo chini ya Harmonize. Siku zinakwenda hakuna lililothibitika yeye mwenyewe hasemi yupo wapi amekuwa Kama Yahaya.

Lakini ni nini kilimtoa kwa Abbah na Hanscana ambako mwenzake Marioo ametulia na anafanya vizuri? Ni kiburi? Abbah process anasema Hanstone aliondoka bila kuaga ni pale alipomkemea baada ya kuiba wimbo walioufanya studio na kuuvujisha, baada ya kumsema akanuna akaondoka. Walipomwita kushoot video ya wimbo wa Chibonge akagoma kutokea hali iliyopelekea wakaondoa verse yake na kumweka gnako.

Akihojiwa na media bila kusema kilichomtoa kwa Abbah anawakana kwamba hakuwa ameingia nao mkataba wowote wa maandishi. Sasa mbona walimpora akaunti yake ya Instagram Kama ndiyo hivyo? Yaani bila mkataba wowote wakamshirikisha kwenye Iokote, Chibonge na kumrekodia nyimbo zingine? Mkataba ni lazima uwe umeandikwa?. Kisheria mkataba ambao ni lazima uandikwe ni wa ajira na kuuziana ardhi tu mingine inaweza isiandikwe na ikawa halali ili mradi kukiwa na ushahidi tu. Kwa hapa Kuna ushahidi wa kimazingira kuwa dogo alikuwa chini ya kina Abbah process na Hanscana na ameondoka kwa jeuri na kiburi.

Hanstone unapaswa ujirekebishe maana kwa staili hii hata labels kubwa unazozitegemea Kama Wasafi na Konde gang zitaogopa kukusaini maana jina lako limeshakuwa labelled kuwa ni kijana mwenye kiburi na dharau na asiye ambilika
 
Rayvanny hataondoka wcb. Yeye mwenyew alitolea ufafanuzi kuwa kweli anaanzisha lebo ila bado ataendelea kuwa chini ya wcb
Ukiweza kutoka WASAFI wewe ni mwanaume.

Pale malipo ni commission based. Toa ngoma ifanye vizuri, mauzo yapatikane WCB wakate chao upewe kinachobaki.

Kinachosaidia matamasha wanaandaa wenyewe, ingekuwa ni kusubiria promoters, watu wangekuwa wanafukuzwa na kutolewa vyombo nje Kwasababu ya kodi ya nyumba.

Youtube channel siyo mali yako.

Nyimbo siyo mali yako.

Jina la kisanii siyo mali yako.

Mpaka mashabiki siyo mali yako ( siku ukijitoa kwenye label ndio utajua hilo )

Support na media coverage yao hupati tena.

( Yaani hata ukipewa gari kwa mbwembwe instagram na kwenye media siyo ZAWADI, kuna kukatana kwenye mapato, hili alilisema Mavoko ndio maana yeye hakuchukua)

NI VITAAAAA.
 
Ukiweza kutoka WASAFI wewe ni mwanaume.

Pale malipo ni commission based. Toa ngoma ifanye vizuri, mauzo yapatikane WCB wakate chao upewe kinachobaki.

Kinachosaidia matamasha wanaandaa wenyewe, ingekuwa ni kusubiria promoters, watu wangekuwa wanafukuzwa na kutolewa vyombo nje Kwasababu ya kodi ya nyumba.

Youtube channel siyo mali yako.

Nyimbo siyo mali yako.

Jina la kisanii siyo mali yako.

Mpaka mashabiki siyo mali yako ( siku ukijitia kwenye label ndio utajua hilo )

Support na media coverage yao hupati tena.

NI VITAAAAA.
mbona wana maisha mazuri tu kuliko hizo labels nyingine hapa bongo.
 
mbona wana maisha mazuri tu kuliko hizo labels nyingine hapa bongo.
Mwenyewe nashangaa,Harmonize anaonandoka Wasafi aliuza nyuma mbili na alitoa milion 200 bank ili alipie mkataba wake na WCB alio uvunja,aliyaongea haya wakati wa uzinduzi wa nyimbo za Country boy na hivyo vyote kavipata ndani ya miaka minne akiwa WCB.

Sasa najiuliza hizo mil 200 na nyumba mbili alizipataje,kama alikuwa ananyonywa.

Wakati wasanii wengine kwenye label wana mwaka wa tatu huu lkn hali zao hazieleweki,brand hazieleweki.
 
Kwa Huyo Harmonize kuna support ya Sara ( Sikiliza Wapo audio ).

Kuna support ya Jembe ni Jembe ( Angalia alichokisema Harmonize siku ya Ushamba party, kwamba huyo Jembe alitoa 100M )

Pili nyimbo za Harmonize mauzo yake na shows zilikuwa juu sana. So, probably hata mgawo ulikuwa mkubwa.
 
Kwa Huyo Harmonize kuna support ya Sara ( Sikiliza Wapo audio ).

Kuna support ya Jembe ni Jembe ( Angalia alichokisema Harmonize siku ya Ushamba party, kwamva huyo Jembe alitoa 100M )

Pili nyimbo za Harmonize mauzo yake na shows zilikuwa juu sana. So, probably hata mgawo ulikuwa mkubwa.

Hiyo Support hatukatai lkn nina uhakika yeye alitoa zaidi ya nusu,je msanii gani unaye mjua ww ndani ya miaka minne akawa na hela kama Kondeboy.

Yy aliuza nyumba mbili na kutoa mil 200,jembe ni jembe akaongeza mili 100.

Show zilikuwa juu,sh ngapi?

Mgao ulukuwa juu kwa % ngapi?

Alafu umemzungumzia Qboy WCB wamemnyonya,sasa mbona kila siku anamwomba msamaha Diamond arudi WCB,manake kama kungekuwa kubaya asinge omba kurudi.

Kifesi WCB ndani ya miaka mitatu WCB ana nyumba mwanza na gari.Kifesi kaondoka WCB sababu ya imani yake ya kisabato,anaona anakosea kufanya kazi siku ya sabato na kaondoka sasa hivi ana kampuni yake ya kupiga picha kwenye masherehe na huwezi mzuia mtu ambaye kwa imani yake anaona anachofanya ni haram.

Mavoko kaingia WCB,alitoa nyimbo ngapi na hit songs zilikuwa ngapi,alikaa kwa miaka mingapi?Mavoko alikuwa chini ya Papaa alipata kiasi gani?,Kaenda Kenya kwa King Kaka alikuwa na kiasi gani?

Alafu useme leo hii WCB wamemnyonya?Kwa mujibu ya intvw aliyoifanya Papa Misifa na Soudy mpaka sasa hivi mavoko andaiwa mil 50 na Papaa,baada ya kuvunja mkataba na kwenda kwa King Kaka.

Mavoko kaondoka WCB 2018,je mpaka hivi sasa ana kiasi gani?
 
Back
Top Bottom