HansPoppe : Safari hii hatutaki wachezaji wa kuokota kijiweni kama Kiiza

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Hanspope: "safari hii hatutaki wachezaji wa kuokota kijiweni kama Kiiza, hakuwa na timu karibu mwaka mzima yule"

==========

pic+hanspope.jpg


BOSI wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe amewaambia mashabiki na wanachama wa timu hiyo kwamba watavunja benki safari hii. Hanspoppe ametamka kwamba kuna straika mmoja matata kutoka katika nchi moja yenye heshima Afrika ambaye amemuonyesha jeuri ambayo imemshtua.

Kigogo huyo ametamka kwamba maneno aliyomtamkia straika huyo hajawahi kuyasikia tangu aanze kufanya usajili au kushughulika na wachezaji, hata Emmanuel Okwi aliyekuwa tishio Simba hakuwahi kuthubutu kumtamkia. Amesema kwamba mchezaji huyo ambaye anatamba kwa sasa katika kikosi chake na timu yao ya taifa amemhakikishia kwamba ampe fedha ashuke Simba kufanya kazi na kama akishindwa kupachika bao japo kwenye mechi moja au timu isiposhinda akatwe Shilingi milioni moja kwenye mshahara wake.

Hanspoppe amesisitiza kupitia Mwanaspoti kuwa kwasasa kamati yake imeamua kuvunja benki kuleta watu wa maana si kama Hamis Kiiza waliyemuokota kijiweni.

Hans Poppe amesema safari hii wanataka kutafuta wachezaji wa kweli wa kigeni na wa kwanza kwasasa wapo katika mazungumzo na mshambuliaji mmoja ambaye amewaambia Simba wakubali kumlipa Dola 2500 (Sh5.3milioni) kwa mwezi kwa kuwa kazi yake anaijua.

“Mfano mzuri ni mshambuliaji mmoja ambaye nafanya naye mazungumzo, ameniambia wazi kwamba anataka mshahara wa Dola 2500 lakini akatuambia kama atamaliza mechi yoyote bila kufunga bao yuko tayari akatwe Dola 500(Shilingi milioni moja) katika mshahara wake huo, mtu wa namna hii anaonyesha wazi anajiamini na kazi yake,”alisisitiza Hanspoppe.

Kiongozi huyo licha ya kwamba hakuweka wazi jina la mchezaji huyo lakini alisema kwamba watamnunua mchezaji huyo na watamlipa kiasi hicho cha fedha alete raha Simba na kurudisha imani kwa wenye timu na kuziba ngebe za Yanga.

“Kwasasa kitu cha kwanza mimi nafikiri tutawaondoa karibu wachezaji wote wa kigeni labda tutabaki na Majabvi (Justice) na huyu kipa Angban, hawa wengine hatuoni kitu, mtu kama Kiiza tulimtoa kijiweni hakuwa na timu zaidi ya mwaka sasa safari hii tunataka kutafuta watu wa kweli acha tutumie pesa lakini tupate kweli wachezaji wenye kitu cha ziada,”alisema Hanspoppe.

“Kwasasa kigezo cha kwanza tutakachotumia katika kutafuta mchezaji awe anachezea timu yake ya taifa au awe anatoka timu ambayo inaongoza katika ligi ya kwao.” Kwa mujibu wa tajiri huyo mwenye mchango mkubwa wa noti ndani ya Simba, safari ya Kiiza, Raphael Kiongera,Emily Nimubona na Bryan Majwega imeiva na kama wanaweza kupiga simu kabisa kwa madereva wao wa bajaji wakae mkao wa kuondoka.

MIKATABA YAFUMULIWA

Ametamka kwamba msimu ujao watafumua mikataba yote ya wachezaji wao kwa kuwabana washambuliaji ambao wamekuwa butu kwa kushindwa kufunga nao wakatwe mishahara.

“Pia tunataka kubadilisha mkataba, mchezaji anagoma kwa mshahara wake kuchelewa kwa siku mbili lakini anagoma tena kibaya anagoma wakati timu imetoka kufungwa haya mambo ni lazika TFF wayaangalie upya na pande zote zibanwe, mchezaji hafungi halafu anagoma mambo kama haya hayazitendei haki klabu lazima tuweke mikataba ambayo itawawajibisha wachezaji.

“Straika asipofunga goli atakatwa mshahara, hatutakuwa na masihara kabisa,”aliongeza kwamba wanajipanga pia kuwa na benchi la maana la ufundi. Wakati Hanspoppe akiyasema hayo juu ya usajili, imebainika pia kocha wao wa sasa Jackson Mayanja naye amekuwa na jitihada za kuleta wachezaji wapya ambao tayari wapo nchini wakitokea nchi za Cameroon na Ivory Coast kwa ajili ya majaribio.

Ingawa mmoja wa viongozi amedai nafasi ya wachezaji hao walioletwa kwa mafungu kusajiliwa ni finyu.


Chanzo: Mwanaspoti


Kama ni ya kweli naomba Hans amuombe radhi Kiiza kwa sababu si ya kimicheo kabisa mtu ana goli 19 unasema tulimuokota ............hapana japo mimi ni simba damu
 
Nyingine Hii Hapa..........

Kocha wa Yanga asema, Manji akiondoka timu inakufa

658414.jpg

Kikosi cha Yanga Tuesday, December 30, 2008 6:56 PM
KOCHA wa Yanga, Profesa Dusan Kondic, amesema kutokana na hali ilivyo katika klabu ya Yanga kwa sasa, anahisi siku mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji akijitoa kuwafadhili, ni wazi timu hiyo itakufa ndani ya kipindi cha wiki moja
KOCHA wa Yanga, Profesa Dusan Kondic, amesema kutokana na hali ilivyo katika klabu ya Yanga kwa sasa, anahisi siku mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji akijitoa kuwafadhili, ni wazi timu hiyo itakufa ndani ya kipindi cha wiki moja.

Kondic alisema analazimika kuhisi hali hiyo, kutokana na ukweli kwamba kila kitu kuhusu huduma za klabu anaachiwa mfadhili huyo, ambaye sasa anaihudumia timu kwa hali na mali.

Alisema hali huwa ngumu inapotokea mfadhili huyo amesafiri nje ya nchi, huku Yanga ikihitaji fedha za kutekeleza majukumu fulani. “Ni ngumu kuwa na uongozi ambao hata kuwanunulia wachezaji mlo wa mchana wa siku moja hawawezi, hatuwezi kukuza soka kwa hali kama hii.

“Nahisi ikitokea mfadhili (Manji) amejitoa kutufadhili, Yanga itakufa ndani ya wiki moja na mafanikio yote haya yatabaki kuwa ndoto za mchana, hakuna mikakati mingine ya kuweza kupata watu mbadala wa kuihudumia klabu,” alisema Kondic.

Alisema Manji analipia kila kitu katika hoteli ya Lamada ambayo wachezaji wa kigeni wa Yanga wanaishi kwa sasa, huku wakiitumia hoteli hiyo kuweka kambi kwa kipindi kirefu cha ushiriki wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

Kondic alisema udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro ni mzuri, lakini hauwezi kukidhi shughuli za Yanga kama anavyotoa Manji.

Kocha huyo alikuwa akizungumzia mazingira ya Yanga kutoweka kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu mzunguko wa pili na ushiriki wa klabu yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, ambapo mpaka sasa timu hiyo haijaingia kambini.

Manji amekuwa akiifadhili Yanga kwa muda mrefu na kuiwezesha timu hiyo kusajili wachezaji kutoka Kenya, Serbia na Malawi. Wachezaji hao ni George Owino, Boniface Ambani, Maurice Sunguti, Ben Mwalala, Mike Barasa, John Njoroge na Joseph Shikokoti (Kenya), Obren Cuckovic (Serbia) na Wisdom Ndhlovu wa Malawi.
 
Viongozi wa mpira wa vilabu vya simba na yanga ni wapiga dili.. Wanahamisha udhaifu wao kwa either kocha au wachezaji.. Hao ndo wanaolaumiwa.. Hanspope na kundi lake (Aveva included) sio viongozi wa soka.. ni wapiga dili kupitia mpira.. Na as long as hawa watakuwapo kwenye uongozi, Simba itegemee kuendelea kuitwa timu ya matopeni..
 
Viongozi wa mpira wa vilabu vya simba na yanga ni wapiga dili.. Wanahamisha udhaifu wao kwa either kocha au wachezaji.. Hao ndo wanaolaumiwa.. Hanspope na kundi lake (Aveva included) sio viongozi wa soka.. ni wapiga dili kupitia mpira.. Na as long as hawa watakuwapo kwenye uongozi, Simba itegemee kuendelea kuitwa timu ya matopeni..
sosoliso siku nyingi sana sijakuona
 
Akionyesha kiwango, mwaka unafuata anaenda Yanga au Azam. Hawezi kuendelea kukaa feeder club kama wa matopeni!
Viongozi wa Simba hawajifunzi kamwe.. Hivi unasajili wachezaji ndiyo utafute kocha au unapata kocha kwanza aseme wachezaji gani atahitaji?
Dalili za Serunkuma mwingine hizo.
 
Kiiza anaonekana si lolote leo eti kisa aliwadai stahiki zake!!!! Napata picha kuwa hata yule dogo anaependwa sana sasa hivi pale Simba Mohamedi Tshabalala atakuwa anapigwa cha juu na viongozi wake ndio maana anapendwa, siku nae akija kuzitambua haki zake tutasikia ya kusikia
 
hii inaonyesha dhahiri kabisa viongozi wa simba ndiyo wanaompangia kocha wachezaji
 
Simba mmefika mahali pabaya, viongozi wanawadanganya ili muendelee kuwaamini. Kiza ni miongoni mwa wachezaji kipenzi cha Simba leo mnasema katokea kijiweni? Watu wasio na shukrani hawapati baraka za mola, simba hiyo ni dalili ya kuharibikiwa miaka mingine mitatu mbele. Kila kilicho bora mungu akikupa sema asante.
 
Huyo foward ataekuwa anatupia kila game anatoka dunia gani!!!! Basi kama kweli ana uwezo huo hata Ronaldo na Messi hawamfikii.
Hujaelewa. Kuna tofauti kati ya kusema akatwe hela asipofunga bao na kusema atafunga bao kila mechi
 
Huyo foward ataekuwa anatupia kila game anatoka dunia gani!!!! Basi kama kweli ana uwezo huo hata Ronaldo na Messi hawamfikii.
Mshahara wenyewe dola 2,500, kwa mwezi timu inacheza mechi angalau 4 hivyo akikatwa dola 500 kila mechi atakuwa amekatwa dola 2,000 kwa mwezi, ataishije? Hapo mikia inakwenda kuingia mkenge mwigine mithili ya akina Sserunkuma na Ndaw. Huyo ni muongo, hakuna mchezaji mwenye uwezo wa kufunga kila mechi duniani kote.

Anataka apewe mkataba kisha mikia yenyewe itaamua kuuvunja kama mikataba ya watangulizi wake.
 
Simba mmefika mahali pabaya, viongozi wanawadanganya ili muendelee kuwaamini. Kiza ni miongoni mwa wachezaji kipenzi cha Simba leo mnasema katokea kijiweni? Watu wasio na shukrani hawapati baraka za mola, simba hiyo ni dalili ya kuharibikiwa miaka mingine mitatu mbele. Kila kilicho bora mungu akikupa sema asante.
Namshauri Pluijm amchukue Kiiza asaidiane na Ngoma kucheza namba hiyo maana mpaka sasa hatuna substitute ya maana kwa Ngoma akipata tatizo.
 
Simba mmefika mahali pabaya, viongozi wanawadanganya ili muendelee kuwaamini. Kiza ni miongoni mwa wachezaji kipenzi cha Simba leo mnasema katokea kijiweni? Watu wasio na shukrani hawapati baraka za mola, simba hiyo ni dalili ya kuharibikiwa miaka mingine mitatu mbele..
Mkuu, maisha ya kambini yana mambo mengi ya siri. Huku nje mnaweza kumuona mtu amapiga mabao lakini akiwa kambini anashawishi migomo. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa soka ya mataifa ya Africa, basi utakumbuka kuwa Samuel Eto'o, Emmanuel Adebayor na Benni McCarthy kwa vipindi tofauti waliwahi kuachwa kuitwa kwenye vikosi vya mataifa yao kwa sababu za kuchochea migomo ya posho, lakini wote hao walikuwa wachezaji mahiri wanaopachika mabao. Sasa itakuwa Kiiza?
 
Kiiza anaonekana si lolote leo eti kisa aliwadai stahiki zake!!!! Napata picha kuwa hata yule dogo anaependwa sana sasa hivi pale Simba Mohamedi Tshabalala atakuwa anapigwa cha juu na viongozi wake ndio maana anapendwa, siku nae akija kuzitambua haki zake tutasikia ya kusikia
I can imagine isingekua magoli ya kiiza sijui simba ingeishia nafasi ya ngapi, namuheshimu sana Hans ila kwa hali yoyote kama kiongozi ni muhimu kuwa makini na kauli.............hata aveva naye kumtumbua kessy haikua stahiki ilihali krossi nyingi za kessy zilizaa mabao and i can also imagne krosi za kesst Tambwe atafunga sana....time will tell....unajua hata Phiri ananukuliwa kusema Tambwe si straika wa aina yake..........
 
Back
Top Bottom