kovai tamil taiga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 1,036
- 1,417
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Sc ya Dar es salaam,Zacharia Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi,Yanga Sc wameingia mkenge kumsajili Emmanuel Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa nani mtani jembe pekee,lakini zaidi ya hapo hatacheza jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.Kapteni huyo wa zamani wa JWTZ amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoille du Sahel ya Tunisia na hawezi kuchezea Yanga."Mimi sina wasiwasi.naangalia tu sarakasi zao nikiwa najua wataangukia wapi,yule mchezaji yanga wameingizwa mkenge na FUFA(shirikisho la soka Uganda).Kwa sababu Etoille walimtoa kwa mkopo Sc Villa na ndiyo maana hata FUFA walipotaka kumtumia katika CHAN,wakaambiwa haiwezekani kwa kuwa yule ni mchezaji wa Etoille"alisema Hans Poppe.
Mmmh Shughuli ipo!!! pole kwa atakayepoteza!
Mmmh Shughuli ipo!!! pole kwa atakayepoteza!