Hans pope:'' Wanasimba msipowachagua Kaburu na Aveva naondoka siwezi poteza muda na pesa zangu tena.

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
????????Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa ,Msimbazi Simba sc wameshamaliza mazungumzo na
wachezaji wawili kutoka nchi za Uganda na Kenya na kinachosubiriwa
ni safu mpya ya uongozi itakayopatikana juni 29 mwaka huu baada ya
kufanyika uchaguzi.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba sc, Keptein wa zamani wa Jeshi la wananchi la Tanzania, (JWTZ), Zacharia Hans Poppe ameuambia
mtandao huu jioni hii kuwa tayari wamepata `jembe` moja la kazi
kutoka Uganda na lingine kutoka Kenya ( hakutaja majina).
Kuhusu wachezaji waliokuwa nao msimu uliopita, mwanajeshi huyo
wa zamani wa JWTZ alisema kuwa wameamua kuwabakisha wachezaji
13. “Wachezaji wa zamani tuliobaki nao ni 13 tu, kwahiyo tutachukua
wengine 12 wa hapa nchini na hao wawili kutoka nje”.
“Sisi tunaendelea vizuri na usajili, kimsingi nawaasa wenzangu
waingize timu nzuri ya Uongozi ambayo tunaweza kufanya nayo kazi”
“Wawe makini kwasababu wachezaji hawa tunaowasajili ni kwaajili
ya msimu ujao. ‘Waangalie viongozi ambao tutakubaliana kimawazo na sisi,
kwasababu tunaweza kuwa na malumbano tena”.
Poppe aliongeza kuwa wagombea wengi wanaowania nafasi za
uongozi walishawahi kuwa viongozi wa Simba, hivyo wanachama
waangalie ni nani alikuwa na mafanikio katika kipindi chake.
“Binafsi najua Aveva ni kiongozi mzuri na akiwa na makamu wake Kaburu, basi timu itakuwa nzuri na tutatengeneza gurudumu la Simba”.
“Nikianza na Kaburu, mtu huyu aliweza kuitengeneza timu ya U20
ambayo imezaa wachezaji kama Ramadhani Singano `Messi`, Harun
Chanongo, Said Ndemla na wengineo. Haya ni matunda yanayotokana
na jitihada kubwa alizofanya Kaburu”.
“Aveva alikuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wakati ambao Simba alikuwa na mafanikio ambayo hayajapatikana mpaka leo”.
“Ni kipindi ambacho Simba iliweza kuwa na makombe nane. Ni kipindi
ambacho alikuwepo Kassim Dewji aliyejenga jengo ambalo
linawaingizia kipato viongozi wa sasa”.
“Timu ya Aveva na Kaburu nadhani inaweza kuleta matokeo ambayo
yalipatikana kipindi kile, ambayo hayajapatikana mpaka leo. Kwahiyo nafikiri hawa ni watu ambao wanaweza kuleta maendeleo bila tatizo”.
Alisema Poppe.
Akimzungumzia Jamhuri Kiwhelo na Richard Wambura, Poppe alisema
hawajawahi kupata mafanikio katika uongozi wao.
“Wambura alipata mafanikio gani wakati wa uongozi wake. Mimi sioni
kama kuna kitu alifanya akiwa Simba. Wadau waseme hawa walifanya A,B C, D. Mimi nimesema Aveva na Kaburu walifanya nini”.
“Julio anagombea umakamu mwenyekiti, sijui amefanya nini. Yeye kazi
yake ilikuwa ukocha na alikuwa analipwa mshahara. Wasichague mtu
kwasababu tu ana wafuasi wengi, eti wanampenda sura au maneno
yake. Sisi tunataka uhalisia, je, alifanya kitu gani?”. Alihoji Poppe.
Poppe aliweka wazi msimamo wake kuwa endapo wanachama hawatawachagua Aveva na Kaburu itakuwa juu yao, lakini yeye
hatakuwepo katika uongozi wa Simba tofauti na safu ya hao wawili.
“Msimamo wangu nausema wazi. Sitaweza kufanya kazi na viongozi
tofauti na hao wawili. Kwasababu naelewa uongozi wowote tofauti na
hao wawili hautaleta mabadiliko yoyote”.
“Sipo tayari kupoteza tena muda wangu na pesa zangu kama nilivyofanya kipindi kilichopita”. Alisisitiza Poppe.
Uchaguzi wa Simba sc utafanyika jijini Dar es salaam juni 29 mwaka
huu ambapo Rais mpya , makamu wa rais na wajumbe wapya wa
kamati ya utendaji watapatikana tayari kwa safari nyingine ya miaka
minne ya uongozi.
Nini maoni yako mdau ukizingatia muda wa kampeni bado? Kuna demokrasia kweli hapa?
 
Huyu binadamu mbona anaharibu tena, licha ya kuwa amefanya kazi nzuri kipindi kilichopita?

Sikubaliani naye kabisa
 
Huyu binadamu mbona anaharibu tena, licha ya kuwa amefanya kazi nzuri kipindi kilichopita?

Sikubaliani naye kabisa

Hata mimi sijamuelewa kwanini kafanya ivi wakati anajua heshima alionayo kwa wanasimba
 
bora tuchague watu wenye hela,tukichagua wenye njaa watakuja kutokea hapohapo uongozini. Mimi huwa siwaamini wagombea maskini hapa Afrika,bora tajiri atapiga kidogo kujazilishia,ila maskini ndo atakuja kuanza moja wadau,au nyie mnaonaje? Naunga mkono hoja ya Hans pope.
 
hans pope sasa analeta makundi simba sc,kama vipi haondoke na pesa zake atuachie simba yetu
 
japokuwa umechapia chapia lakini nimekuelewa,wambura hakuna kitu pale,kaifanyia nin tff miaka yote aliyokuwa katibu mkuu?

Ingawa mimi ni yanga lkn nashauri demokrasia ichukue mkondo wake. Kusema humtaki fulani na unamtaka Fulani sio vizuri. Huko ni kuleta makundi ambayo mwisho wa siku yanaleta migogoro klabuni. Kikubwa katiba na taratibu zifuatwe watani zangu.
 
Ingawa mimi ni yanga lkn nashauri demokrasia ichukue mkondo wake. Kusema humtaki fulani na unamtaka Fulani sio vizuri. Huko ni kuleta makundi ambayo mwisho wa siku yanaleta migogoro klabuni. Kikubwa katiba na taratibu zifuatwe watani zangu.

Demokrasia bongo?
 
Huyu pimbi kweli..ai awachukue hao wawili wakamaaidie kazi za nyumbani kwake
 
Kaburu tena ndani ya wana Msimbaziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
japokuwa umechapia chapia lakini nimekuelewa,wambura hakuna kitu pale,kaifanyia nin tff miaka yote aliyokuwa katibu mkuu?

Hivi huyu Wambura ndo mdau mkubwa wa kugombea kila nafasi kwenye soka? Au ndo mwenye haki zaidi ya kugombea? Huyu jamaa ni forcer ila nyota yake uwa haingai! Ni bora ifikie hatua akagange njaa kwingine aachane na uongozi wa soka.
 
Kama JK amesema kwake serikali tatu katu aiwezekani, ZHP nae kaweka lake la moyoni ataki kufanya kazi na MKURYA.
 
Muachiwe mna hela nyie?
Unasema simba yako wakati hata hujaenda kufyeka kule bunju.

Simba na Yanga zinapaswa kujitegemea na si kutegemea watu wenye pesa maana wakiondoka wanaondoka na pesa zao klabu inabaki kuwa maskini , anatakiwa mtu atakaejenga misingi ya klabu kujitegemea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom