Hans pope:'' Wanasimba msipowachagua Kaburu na Aveva naondoka siwezi poteza muda na pesa zangu tena.

Hans pope alipaswa kutokuwa wazi ni mgombea gani anayemtaka na kuacha demokrasia ichukue mkondo wake. Nina uhakika wa asilimia 100% kuwa wanasimba hawatarudia makosa kwani miaka minne ya maumivu kila mpenzi wa simba anaijua. Sio siri mpira sasa hivi unahitaji pesa. Cha msingi ni wanachama kuweka utaratibu ambao kutakuwa na kipindi cha mpito kwa hizi kilabu mbili kubwa simba na yanga kutoka mikononi kwa matajiri na kuanza kujitegemea. Na uwezo wa hizi timu kujitegemea upo kukiwa na misingi mizuri ya kukusanya kodi ya majengo na kuanza kuuza vitu kama jezi, skafu, na matangazo mbalimbali. Baada ya rage na manji kushindwa kuzifanya simba na yanga zianze kujitegemea sioni kiongozi mwingine mwenye uwezo huo kwa siku za karibuni.
 
Mtazamo dhaifu kabisa huo

wewe ndiye mwenye mtazamo dhaifu na mvivu wa kufikiri...dunia ya leo hakuna michezo ya ridhaa kama zamani...how can you own something you haven't paid for? wenye simba ni wale wanaowekeza simba, wewe ni shabiki tu wa simba kama walivyo wengi wa yanga. But you are not owners! Live with it.
 
Mi naona kaongea sawa haiwezekani anatoa mahela kila siku yanaishia kwa viongozi wajinga wajinga tu, timu kila siku inavurunda tu ndio maana msomali alituita mbumbumbu FC.
 
wewe ndiye mwenye mtazamo dhaifu na mvivu wa kufikiri...dunia ya leo hakuna michezo ya ridhaa kama zamani...how can you own something you haven't paid for? wenye simba ni wale wanaowekeza simba, wewe ni shabiki tu wa simba kama walivyo wengi wa yanga. But you are not owners! Live with it.

Unajua maana ya kuwekeza? Au unabwabwaja 2, Manji mwenyewe pamoja na pesa zake hajawekeza yanga anatoa msaada ndo maana kesho akiondoka yanga itabaki maskini , usikariri kuwa kila mwenye pesa nyingi anafaa kuwa kiongozi japo mpira unaitaji pesa, simba na yanga zinaitaji viongozi watakao wenye mazingira ya kuvutia kwa wawekezaji ili waje kuwekeza
 
Kuna watu walikuwa wanamponda sana Manji,now naona ya Manji kuliko huyo Hans Pope
 
Back
Top Bottom