Hanje amuomba Rais Magufuli kuzifuta kesi za uchaguzi mkuu 2020

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mbunge wa viti maalum, Nusrat Hanje amemuomba Rais John Magufuli kuzifuta kesi zote zinazohusu uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2020 ili wananchi wafanye shughuli za kuijenga nchi.

Hanje ni miongoni mwa wanawake 19 waliovuliwa Uanachama wa Chadema baada ya kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho.

Baada ya kufukuzwa Uanachama walikata rufaa na sasa kikao cha baraza kuu la Chadema kinasubiriwa kusikiliza rufaa yao na kutoa uamuzi.

Licha ya Chadema kutowatambua, waliapishwa na Spika Job Ndugai na sasa wanashiriki vikao vya Bunge la 12 vinavyoendelea mjini Dodoma

Hanje aliapishwa kuwa mbunge siku moja baada ya kutoka mahabusu alikoishi kwa siku 133. Yeye na wenzake walishtakiwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali, kudhihaki wimbo wa Taifa, kujaribu kuvujisha siri za halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida na kutoa lugha za kuudhi.

Novemba 23, 2020 walitoka gerezani baada ya kufutiwa mashtaka na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga.

Akizungumza bungeni leo Jumatano Februari 3, 2021 katika mjadala wa hotuba ya ufunguzi wa Bunge ya Rais Magufuli aliyoitoa mwishoni mwa 2020, Hanje amesema wanasiasa kuendelea kwenda mahakamani wakati uchaguzi umekwisha hakutoi taswira nzuri kwa mataifa mengine.

Amewataja baadhi ya wanasiasa wenye kesi mahakamani kuwa ni naibu katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui na kada wa Chadema, Salome Makamba.

"Yaani mtu umemchukulia mke wake halafu bado unataka kumuua hilo jambo siyo sawa kabisa, ufike wakati wahusika watambue hilo ili watu wakae kupanga namna ya kulijenga taifa lao," amesema Hanje.

Amesema anao uzoefu wa vitendo kwa maisha ya gerezani kutokana na muda aliokaa mahabusu kwa sababu za kisiasa.

Amebainisha kuwa maisha ya gerezani hayafai hasa katika kipindi hiki ambacho kuna tishio la ugonjwa wa Uviko 19.

Kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 amesema kila mmoja anajua ndani ya moyo wake kilichotokea.

CHANZO: MWANANCHI
 
Kwamba Rais ana uwezo wa kuamua kufuta kesi??

Ndiyo maana USA waliona ni bora waongozwe na chizi Trump ili kumuepuka mwanamke Clinton..
 
Hakuna kesi ya uchaguzi hata moja zilizopo ni za kihalifu tu labda mtu kuchoma mali za serikali nk sio za uchaguzi .Haeleweki anaongea nini
 
Bunge limevamiwa.

Hii nchi kuna watu walipoteza maisha yao, kuna watu walifungwa, kuna watu walipoteza kila kitu chao kupambana ili kuwe na utawala wa kisheria na haki. Halafu kuna watu ndani ya muda mfupi wanajitoa akili ili kuirudisha nchi miaka 60 iliopita.
 
Back
Top Bottom