Hanitaki kisa nakula Nguruwe na ni dhambi, wakati yeye ni Mshirikina

Aug 8, 2013
29
16
Wadau, kuna dada mmoja namuelewa sana ni mzuri na tulishaanza mahusiano kwa mbali ila hatujafanya mapenzi. Tatizo aliniona nakula Nguruwe, kwa mbali akaanza kunikwepa nikimtafuta anachuna.

Siku moja akanitumia SMS tatizo Nguruwe 😃, nilimwambia basi kana tatizo ndo hilo nitajitahidi kuacha kidogokidogo, akakataa.

Sasa juzi niko kwenye gari natoka Studio naenda Mwananyamala nimemuona pale Garage usiku kama mida ya saa nne anavunja nazi nikamuita kabisa akageuka akakimbia 😲

Nikamtumia SMS nikimbembeleza tuwe pamoja, anasema tatizo nakula Nguruwe, nikamwambia mbona wewe unaenda kwa Waganga? Ananiambia eti anaweka mambo sawa tu .😃.
 
Hata wewe hovyo sana. Kwa nini unakula nguruwe?? Kula kiti moto bhanaa sio kula nguruwe. Tena ule kiti moto na ugali ndo utapata nguvu za kiume.

Usile nguruwe hata siku moja.
Tatizo lao ni kushindwa kutofautisha: Ukila huyo nguruwe asubuhi unaenda kumtoa kama mbolea. Mwili unapata afya tele na nguvu za kiume kumridhisha.

Yeye anaenda kwa mganga, anavuliwa nguo, anatomaswatomaswa na huyo mganga, genye zikimpanda anaambiwa ni mashetwani na dawa lazima aingiziwe huku amefumba macho. Anapatwa na ukimwi au mtoto aso na baba. Halafu dhambi anaifanya bila ridhaa.
Ni yupi bora? Mla kitimoto au mliwa bila ridhaa?

Wanawake ni wengi, achana naye hajitambui. Anaendaa garage kwani yeye ni gari bovu??
 
Siyo siri nimecheka baada ya kukuona akakimbia, ukilazimisha atakuvunjia na wewe nazi tena kwenye hilo dude lako, wanawake wote hawa, utapata tu mlaji mwenzako huyo akwendreeeeeeeee
 
.
tapatalk_1577093906393.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom