Vision 2030
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 407
- 250
"Mrejee na Joshua Nasari Paskali"Wanabodi,
Kwanza sote tunalaani kwa dhati kabisa, kitendo alichofanyiwa Mhe. Tundu Lissu cha kumiminiwa risasi 38 na watu wasiojulikana, kati ya hizo risasi 16 zikampata!, kitendo ambacho kimefanywa mchana kweupe, tena akiwa kwenye eneo ambalo ni secure area!, maeneo ya waheshimiwa, ambayo yanalindwa wakati wote.
Kwanza tumshukuru Mungu, kumponya, maana kumiminiwa risasi 16 na kuendelea kuishi, ni muujiza wa Mwenyeezi Mungu tuu kwa sababu risasi moja tuu huwa inatosha kuondoa uhai wa binadamu, washambulizi wa Lissu, walidhamiria kumtoa uhai, wakapiga risasi 38 na bado Lissu aka survive, huu ni uthibitisho, Lissu ni mpango wa Mungu.
Wakati tukiendelea kusubiria taarifa rasmi ya ni nini haswa kilichotokea, na taarifa ya uchunguzi wa kipolisi wa jeshi letu la polisi, na tukiendelee kumtakia uponyaji wa haraka Mhe. Tundu Lissu, tukio hili linapelekea sisi watu wa kuhoji tuanze kuimulikia Chadema kwa kuiangazia baadhi ya trends zake kwa namna inavyoshughulikia issues serious kama hizi za security threats, jee Chadema ndio kingekuwa ikulu yetu, hivi ndivyo namna ambavyo wangeendesha nchi yetu.
Angalizo Muhimu Kabla Hujasoma Bandiko Hili!.
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa trends reading.
Trend Reading ni Nini?.
Trend Reading ni elimu au ujuzi wa observation jinsi mtu, kitu, taasisi inavyo behave kwenye a certain situation, hivyo kufanya prediction, kama huu ndio mwenendo wake katika situation hii, then ingekuwa hivi, hiki kingetokea.
Elimu ya Trend Reading, Inafundishwa Wapi?
Haifundishwi popote, hii ni acquired knowledge ya observation tuu, ila msingi wake mkubwa ni somo la Historia, ambalo is the study of the past, in relation to the present, hivyo to determine the future kwa kufuatilia hulka, maneno na matendo ya mtu, kitu au taasisi husika.
Tukio la Shambulizi kwa Lissu Limepelekea Sisi Trend Readers Kosoma Trends za Chadema.
Trends za Chadema kabla ya tukio, zinapelekea sisi wengine kuanza kujiuliza kama huu ndio utendaji wa Chadema, ingelikuwaje kama ndio wangeshika nchi ile 2015?. Kabla hatujakwenda kwenye trends za Chadema, naomba niwape mfano rahisi wa Trends za Rais Magufuli.
Trends za Rais Magufuli.
Mfano hai wa hizi trends ni huu utawala wa sasa wa rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli tangu ukiwa waziri, wakati huo hana mamlaka na hana katiba, kama ni kweli, na ilithibitishwa kuwa alionyesha ukabila na upendeleo kwa kugawa nyumba za serikali kwa ndugu zake hadi ... wake, sasa akiwa ni rais wa JMT, nini kitamzuia au kitamfanya asifanye upendeleo kwa kutoa vyeo kwa ndugu zake, jamaa zake, rafiki zake au kabila lake as long as wana sifa, vigezo na wana uwezo?, on top of that katiba inamruhusu kumteua mtu yoyote, kutoka popote, kwa sababu zozote au bila sababu zozote?.
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi ...
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Kama akiwa waziri aliwahi kutoa maamuzi kwa ubabe, uvunjifu wa sheria, na baadhi ya maamuzi yalilitia hasara taifa letu kwa kulipishwa fidia, sasa huyu ndiye rais wetu, mwenye mamlaka na mwenye katiba, na mwenye sheria, does he expected to act and behave differently now? . What do you expect of him na utawala wake?, nini kitamzuia asiundeleze ule ule ubabe na kufanya maamuzi magumu ya kibabe, hata kama mwisho wa siku, yatalitia taifa hasara, si tutalipa tuu fidia, kama huku nyuma tulilipa, nini kitatufanya sasa tusilipe?.
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...
Hivyo wote wanaopiga kelele kuwa rais Magufuli ni dikiteta, sio good trend readers, trends za Magufuli, sisi wengine trend readers, tuliwawekea humu
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Lakini pia hakuna ubishi, sote tulikubaliana hata humu JF, kuwa Tanzania hapa mahali tulipofika, tulimuhitaji sana mtu kama Magufuli ambaye ni dikiteta Mzalendo
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Vivyo hivyo kwa Chadema, kama wameshindwa
Kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kushughulikia hili jambo, what are the chances kuwa wangekuwa kwenye ikulu yetu, wangefuata?.
Sasa just imagine kwa trends hizi za Chadema, kama ndio wangekuwa ikulu, hali ingekuwaje?.
Kama wewe sio trends reader, naomba kwenye bandiko hili, uishie hapa, huku ndani zaidi usiingie, kutakuchanganya bure asante.
Ma trend readers karibuni tuendelee tukate issues.
A Way Forward Kwa Usalama wa Wabunge Wetu na Viongozi Wetu.
Wakati tukisubiri taarifa rasmi, naomba kuchukua nafasi hii kutoa mapendekezo yangu ya way forward.
Hitimisho
- Serikali, Idara ya Usalama na Jeshi letu la polisi wasipuuzie tena kitisho kinachotolewa na mtu yoyote, iwe ameripoti rasmi kituo cha polisi au hakuripoti, they should take it very serious. Ingekuwa hili tukio limetokea enzi za Nyerere, saa hizi watu wangeishafukuzwa kazi!. Mtu hawezi kusema anafuatiliwa, akataja number ya gari, halafu they did nothing!.
- Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, visiendele kutumia neno "watu wasiojulikana" kama chaka la kufichia uzembe wa vyombo vya dola katika ufuatiliaji, kama ilivyo kwa yule mtu asiyejulikana, aliyemtishia Nape bastola, naye alikuwa akitumia gari aina ya Nissan nyeupe, picha zake zipo, video zipo, lakini ni mtu asiyejulikana!.Vyombo vya ulinzi vikisikia tishio, vifanye rapid response, hii ya watu wasiojulikana huku wanawajua fika, its not gonna last long!.
- Kila mbunge analipwa fedha za kumlipa dereva na msaidizi, Wabunge waishinikize serikali, kuziongeza fedha hizo ili madereva wote wa wabunge, wawe ni wale ni ma body guards wao waliopitia mafunzo na wawe ma pro ikiwemo kuwa armed.Kama Dereva wa Lissu angekuwa ni pro, nadhani tusinge fika hapa tulipofika.
- Wabunge na viongozi wetu wote, wapewe mikopo minene, ya kununua magari imara ya kisasa ya deraya, yasiyopenya risasi na yana GPS na IP camera mbele na nyuma na ndani, na kurekodi kila movements kwa command tuu, huku savers zikiwa at safe place na wawezeshwe kufunga IP-CCTV camers kwenye nyumba zao, na kwenye starehe zao, waache kwenda vichochoroni, wakazifanyie kwenye hoteli zinazoeleweka, CCTV cameras hadi kwenye parking!.
- Viongozi wote ambao wana hisi usalama wao uko mashakani, wawe armed, wavae BP kwenye publics na kuwa na high security alert. Ile hoja kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani, imeanza kuwa ni historia, leo imetokea kwa Lissu, hatuwezi kujua, kesho itakuwa ni zamu ya nani.
- Chadema kama chama kihakikishe kinafuata sheria, taratibu na kanuni katika kushughulikia mambo yake pia kiwafundishe kufuata sheria taratibu na kanuni na kuwafuatilia kuhakikisha kwenye kila jambo wabunge wake wanafuata sheria, taratibu na kanuni, vingenevyo kuna baadhi ya malamiko ya Chadema kutotendewa haki na serikali yetu ila ukichunguza kwa makini unakuta ni uzembe, ujinga na mapuuza tuu ya kutokufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni.
Jambo hili la Chadema kupuuzia au kutofuata sheria, taratibu na kanuni, nitaendelea nalo baada ya hali ya Tundu Lissu kutengamaa na kurejea ulingoni ili nisionekane sina utu na ubinaadamu, badala ya kuwafariji Chadema katika kipindi hiki kigumu, sisi ndio kwanza tunazidi kuwasimanga, na kuwasakama, no!, hapa ni kutoa tuu angalizo, kwa sababu hata katika kulishughulia hili la Lissu, bado kuna sheria taratibu na kanuni za kufuata katika kumuuguza.
Kwa sasa naomba sote tuungane tuwe kitu kimoja katika kumuombea Mhe.Tundu Lissu uponaji wa haraka na kurejea katika majukumu yake, ndipo turejee humu tuambiane ukweli, kama Chadema ni serious party kinachohitaji kukabidhiwa nchi come 2020, then lazima kibadilike, kinjiondoe kwenye chama cha Siasa cha kiharakati na kugeuka chama kweli cha siasa kinachojiandaa kutawala nchi, msingi mkuu wa utawala ni kufutwa
kwa sheria, taratibu na kanuni.
School mate, Mhe. Tundu Lissu Get Well Soon!.
Paskali