Huenda wanapekua mabomu ya kutega, si unajua taifa limeingiliwa na magaidi.Jeshi la Polisi Handeni linalalamikiwa kushika Nyeti za wanawake Wilayani Handeni mkoani Tanga kwa nguvu bila ridhaa ya wanawake hao.
View attachment 1920373
Nimeona hiyo video ya mkuu wa Wilaya akiongea na wananchi wakitoa malalamiko yao juu ya unyanyasaji wa Polisi,kuna wadada walipigwa mangumi na kuvimba nyuso,wangine wakitolewa kinguvu kwenye ukumbi wa disco na askari wenye siraha na kulazimishwa ngono,yaani inasikitisha aisee,mkuu Wilaya akawaambia wapige kura za siri wawataje hao Polisi,wakawataja,Mkuu Wa Polisi akaahidi kufuatilia apewe muda kwa sababu yeye mgeni wilaya hiyo.....Yani Handeni wananchi wananyanyasika sana na askari Polisi.
Wanawapigapiga, wanawafanyia hila .
Ni wazi kuwa kuna tatizo kubwa sana.
Kuwa askari nimgawanyo wa majukumu kwamba wengine wawe madaktari, Walimu , wakulima n.k.
Kwanini askari wanajiona miamba?
Kwanini wanataka kuogopewa?
Kinachotakiwa ni kuheshimiana mkubwa kwa Mdogo !
Kama kuna wahalifu wapelekeni mahakamani na isiwe kwa kuwabambikia au visasi.
Wengine Eti visasi vya wanawake askari anapeleka ofisini anatumia nafasi yake vibaya kukomoa watu.
Polisi Handeni kuangaliwe kuna tatizo gani?
Je upande wa wananchi kuna tatizo gani?
Upande wa wananchi uangaliwe na upande wa Polisi uangaliwe.
Mbona unamtetea huyo Magesa?,alitoa taarifa wapi kama yeye siyo miongoni mwao?...Kwenye lile list ya walotaja wananchi baada ya DC kuwaambia wawataje hata kwa kuandika majina tu kuna mmoja tu ni kama kaponzwa na mkumbo.
Yeye saingine huwa ni dereva wa gari wa hicho kinachoitwa kikosi kazi.
Lakini yeye unaambiwa hanaga tabia za kupiga wananchi wala kuwanyanyasa.
Sema kwa kuwa mara nyingi huwa anakuwa nao ndio maana lakini kwa haki kabisa huyo Magese sijui Magesa siyo mtesaji hana ubaya na mtu!