Handeni, Tanga: Polisi wadaiwa kushika nyeti za wanawake kwa nguvu bila ridhaa

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Mbona unamtetea huyo Magesa?,alitoa taarifa wapi kama yeye siyo miongoni mwao?...


Simtetei! Wala simjui!
Ni baadhi ya wananchi wamesema jamaa ametajwa kwa bahati mbaya labda kwa kuwa huwa anaambatana na wenzie na wakati mwingine huwa yeye anaendesha gari kuwabena hao wengine lakini Eti yeye huwa hafanyii wananchi ukatili wala ubaya wowote.

Kwa hiyo wakasema uchunguzi ukifanyika vizuri na kwa haki wataona jamaa hajamtesa yeyote!

Sasa ukweli utabainika kupitia uchunguzi iwapo ataonekana naye kuwa ni miongoni mwao basi watajua cha kuwafanya!

Cha muhimu wananchi wapewe mrejesho baada ya huo uchunguzi na hatua zitakazo chukuliwa.
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Nimeona hiyo video ya mkuu wa Wilaya akiongea na wananchi wakitoa malalamiko yao juu ya unyanyasaji wa Polisi,kuna wadada walipigwa mangumi na kuvimba nyuso,wangine wakitolewa kinguvu kwenye ukumbi wa disco na askari wenye siraha na kulazimishwa ngono,yaani inasikitisha aisee,mkuu Wilaya akawaambia wapige kura za siri wawataje hao Polisi,wakawataja,Mkuu Wa Polisi akaahidi kufuatilia apewe muda kwa sababu yeye mgeni wilaya hiyo.....


Ni kweli OCD nasikia ni mgeni.

Kuna OCD ambaye alipoteza maisha kwa ajali kule kule hivi karibuni.

Kuna mwingine akahamishiwa Songe nazani.
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Lile tukio la ile bar ya paradise wamewabutua wananchi kama mbwa!

Kisa Eti muda ulipitiliza saa 6 usiku kwa dakika chache tu,

Kuna wateja walikuwa wanamalizia vinywaji vyao ili kisha baa ifungwe.

Milango ikafungwa ili wasije wateja wapya .

Askari wakaja fungua milango nakwambia hekaheka wakaingia wakaanza kuwapiga kama mbwa

Imagine!

Mwenye baa ni mlipakodi na mtu akishalewa inabidi umbembeleze, Kwanini wanapigwa vile ?!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom