Handeni, Tanga: Polisi wadaiwa kushika nyeti za wanawake kwa nguvu bila ridhaa

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Yani Handeni wananchi wananyanyasika sana na askari Polisi.
Wanawapigapiga, wanawafanyia hila .

Ni wazi kuwa kuna tatizo kubwa sana.

Kuwa askari nimgawanyo wa majukumu kwamba wengine wawe madaktari, Walimu , wakulima n.k.

Kwanini askari wanajiona miamba?

Kwanini wanataka kuogopewa?
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Askari ni watumishi wa wananchi , jukumu Lao ni kuwalinda wananchi na mali zao.

Sasa kwanini tena iwe tatizo.?
 

Vi rendra

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
3,051
2,000
Ni tabia yao, kuna siku mmoja alitaka kuondoka na simu yangu kitemi nikamwambia chukua tu.. wana tabia za ajabu ajabu sana
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Yani tukiwa bado katika kutafakari tukio lile la juzi Salender bridge huku kuna askari wanasemekana kuwatenda vibaya wananchi?! Kweli?!
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Mimi ni mojawapo ya watetezi wa Polisi ninaposikia tuhuma na malalamiko ya wananchi kama hivyo huwa nasikitika sana!

Kuna baadhi ya askari wanasababisha good image ya jeshi la Polisi isiwe Nzuri machoni pa jamii.
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,021
2,000
Halafu ni ajabu naona sababu ya maendeleo ya utandawazi huenda ndio maana siku hizi mambo ya kimila yameachwa au kupungua.

Zamani wazigua uwafanyie mambo ya hiyana? Thubutu!

Ukisalimika utarudi kwenu na nguo za mwilini mwako na begi la nguo utaagiza uletewe stendi ya basi!

Nimewapongeza sana kwa kuwa na subira na kuachana na mambo yetu yaleeee!

Kuna mba-dala ambao wangeweza kufanya ambao hautumii mapanga wala bunduki!
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
12,177
2,000
Yani Handeni wananchi wananyanyasika sana na askari Polisi.
Wanawapigapiga, wanawafanyia hila .

Ni wazi kuwa kuna tatizo kubwa sana.

Kuwa askari nimgawanyo wa majukumu kwamba wengine wawe madaktari, Walimu , wakulima n.k.

Kwanini askari wanajiona miamba?

Kwanini wanataka kuogopewa?

Kinachotakiwa ni kuheshimiana mkubwa kwa Mdogo !

Kama kuna wahalifu wapelekeni mahakamani na isiwe kwa kuwabambikia au visasi.

Wengine Eti visasi vya wanawake askari anapeleka ofisini anatumia nafasi yake vibaya kukomoa watu.

Polisi Handeni kuangaliwe kuna tatizo gani?

Je upande wa wananchi kuna tatizo gani?

Upande wa wananchi uangaliwe na upande wa Polisi uangaliwe.
Nimeona hiyo video ya mkuu wa Wilaya akiongea na wananchi wakitoa malalamiko yao juu ya unyanyasaji wa Polisi,kuna wadada walipigwa mangumi na kuvimba nyuso,wangine wakitolewa kinguvu kwenye ukumbi wa disco na askari wenye siraha na kulazimishwa ngono,yaani inasikitisha aisee,mkuu Wilaya akawaambia wapige kura za siri wawataje hao Polisi,wakawataja,Mkuu Wa Polisi akaahidi kufuatilia apewe muda kwa sababu yeye mgeni wilaya hiyo.....
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
12,177
2,000
Kwenye lile list ya walotaja wananchi baada ya DC kuwaambia wawataje hata kwa kuandika majina tu kuna mmoja tu ni kama kaponzwa na mkumbo.
Yeye saingine huwa ni dereva wa gari wa hicho kinachoitwa kikosi kazi.

Lakini yeye unaambiwa hanaga tabia za kupiga wananchi wala kuwanyanyasa.

Sema kwa kuwa mara nyingi huwa anakuwa nao ndio maana lakini kwa haki kabisa huyo Magese sijui Magesa siyo mtesaji hana ubaya na mtu!
Mbona unamtetea huyo Magesa?,alitoa taarifa wapi kama yeye siyo miongoni mwao?...
 

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,409
2,000
Huko Handeni si ndio wanakoishi Wazigua.
Wawaroge tu hao polisi uchwara.
Tumechoka kuishi na watu madomo zege hata kutongoza hawajui huku wana mishahara.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
125,013
2,000
1630685255660.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom