HANDENI: Serikali yapiga marufuku wakulima kuuza mahindi yakiwa mashambani

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
Serikali wilayani Handeni imewapiga marufuku wakulima kuacha kuuza Mahindi yakiwa shambani ili waweze kutumia vyema fursa ya mavuno ya msimu wa mvua za masika.

Pia kujiwekea chakula badala ya kuitegemea serikali kuwapelekea chakula cha bei nafuu kutoka hifadhi ya taifa ya chakula.
9054d95fe8124773e8fe987b72d4b95a.jpg

Wilaya ya Handeni kwa sasa inaongozwa na Mh. Godwin Gondwe
cee9e7de65d57a3c76b9ccb3939a7d4c.jpg


SOURCE: ITV
 
Wapeni msaada sasa, kama hela hawana kwanini wasiuze ili waweze kukizi mahitaji mengine.
 
Ndio tatizo la kila mtu kujiona anafanya maamuzi sahihi kwa watu.
Sasa hayo mahindi watakula bila mboga? Au watapata wapi pesa za matumizi?
 
Mh Gondwe usipokuwa makini na kuwashirikisha wanainchi wenyewe hayo mahindi yatavunwa usiku na kuuzwa asubuhi shamba jeupe.
 
Mimi ninalima Handeni. Hakuna jinsi utamkataza mkulima asiuze mahindi mabichi au kulazimisha mahindi kukauka mapema kwa kuanika. Watoto wadogo hawawezi kula mahindi ya kuchoma au kuchemsha. Inabidi wauze wapate hela wanunue unga angalau kidogo kwa ajili ya wtt wadogo. Zaidi ya hilo lzm wapate pesa kwa mahitaji mengine. Kuna watu wengine wamelima kwa ajili ya biashara leo unampangia . Serikali fikirieni kabla hamjatoa maamuzi.
 
Back
Top Bottom