Handeni: Basi la Buffalo lagongana na gari dogo, abiria 47 wanusurika kifo

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
746
3,058
pic+ajaliiii.jpg

Abiria 47 waliokuwa wakisafiri kutoka Mkoa wa Arusha kwenda Dar es Salaam nchini Tanzania wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya kampuni ya Buffalo kugongana na gari ndogo na kupinduka.

Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 14,2019 katika kijiji cha Kwekwale na hakuna kifo chochote kilichotokea.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Buffallo, Innocent Mauki kutoka kuyapita magari mengine mawili yaliokuwa mbele yake huku eneo husika likiwa na alama za kukataza gari kumpita mwenzake.

"Naliagiza jeshi la polisi kumtafuta dereva wa hili basi halafu ashitakiwa kwa kosa la ku over take sehemu ambayo alama haziruhusu kufanya hivyo," amesema Gondwe.

Lucas Karoli dereva wa gari ndogo yenye namba T 706 DPE amesema aliona dereva wa basi hilo akijaribu kuyapita magari mawili yaliokuwa mbele yake huku alama zikiwa haziruhusu na ndio akaligonga gari lake upande wa kulia.

Abiria waliokuwepo kwenye ajali hiyo wametafutiwa gari nyingine na kuendelea na safari.

Chanzo: Mwananchi
 
Pole kwa abiria ambao hawajapata madhara, huyo Dereva atafutwe na sheria ichukue mkondo wake
 
Huu mwezi balaa
Jana ajari imetokea eneo la msaginya mpanda KATAVI .Abiria kadhaa wamenusurika kufa wakitokea mpanda kwenda Tabora baada ya gari walililokuwa wakisafiria kupata ajari.
 
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Buffallo, Innocent Mauki kutoka kuyapita magari mengine mawili yaliokuwa mbele yake huku eneo husika likiwa na alama za kukataza gari kumpita mwenzake.


Hawa ndiyo madereva waliosomea na wana vyeti kama inavyosisitiziwa na waziri Lugola, na zaidi ya yote wanakaguliwa kila kukicha
 
Huyu dereva anatakiwa aende jela moja kwa moja watu wa mabasi wanazalau sana gari ndogo utakuta wanatanua pasipo staili alafu utakuta wako watatu wanafukuzana ukijifanya kuwakazia wanakuua kama walivyomfanya huyo jamaa
 
Back
Top Bottom