Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 752
- 3,094
Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 14,2019 katika kijiji cha Kwekwale na hakuna kifo chochote kilichotokea.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Buffallo, Innocent Mauki kutoka kuyapita magari mengine mawili yaliokuwa mbele yake huku eneo husika likiwa na alama za kukataza gari kumpita mwenzake.
"Naliagiza jeshi la polisi kumtafuta dereva wa hili basi halafu ashitakiwa kwa kosa la ku over take sehemu ambayo alama haziruhusu kufanya hivyo," amesema Gondwe.
Lucas Karoli dereva wa gari ndogo yenye namba T 706 DPE amesema aliona dereva wa basi hilo akijaribu kuyapita magari mawili yaliokuwa mbele yake huku alama zikiwa haziruhusu na ndio akaligonga gari lake upande wa kulia.
Abiria waliokuwepo kwenye ajali hiyo wametafutiwa gari nyingine na kuendelea na safari.
Chanzo: Mwananchi