Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,829
- 4,167
Leo. Saa 3 usiku.
Channel 10.
Channel 10.
Waulizeni CHADEMA kama kabla ya walkout yao bungeni waliwauliza wapiga kura wao kwanza, au walijiamulia wenyewe tu.
Waulizeni CCM kwa nini waliitisha primaries kutaka kujua matakwa ya wanachama wao, halafu baada ya kupata Bashe mshindi na Kigangwalla mshindi wa tatu, wakaamua kumchukua Kigangwalla awe mgombea wao.
Waulize CUF kama kabla ya kusaini muafaka walipata baraka za wapiga kura wao.
Naamini majibu ya maswali haya matatu kutoka vyama vikubwa vitatu Tanzania yatakupa jibu kama vyama vyetu vinakwenda kidemokrasia au la.
Mimi ni mpiga kura wa chadema na wabunge waliomsusia Mkwere ni wawakilishi wangu.
Sihitaji kwenda mjengoni kujadiliana nao. Vinginevyo neno 'wawakilishi' halina maana.
Ninawapongeza kweli kwa uthubutu wao.
Siyo lazima uwe unachangia mkuu hata kama huna points kwani kwa kufanya hivyo unajishushia heshima yako.Swali si kwamba ni wawakilishi wako au si wawakilishi wako, zaidi ya uwakilishi wa jumla, walitaka kupata maoni yako kuhusu hilo swala au wamekuamulia tu kwa sababu mmeungana kwenye paja moyo wako ukipiga wanausikia?
Kwa sababu leo wataamua hilo, kesho wataamua kodi ipande asilimia 75% ili kuchangia mishahara yao, utasemaje?
Representative democracy is supposed to represent the peoples views, si ndiyo mna mbiu ya "people's power" ?
Unajua wapiga kura wangapi wa CHADEMA wanakubaliana na hili, wangapi hawakubaliani ?
Siyo lazima uwe unachangia mkuu hata kama huna points kwani kwa kufanya hivyo unajishushia heshima yako.
Ubaya wa demokrasia ni neno "uwakilishi". Viongozi wa chama fulani wanaweza kuamua jambo kwa wingi wa kura moja tu, na maamuzi yao yakawa yanatosha kuwawakilisha wapiga kura wao. Vivyo hivyo kwa Waziri au Rais, pale wanapokwenda kujifua majuu kwa "kuwawakilisha" raia wao. Mimi wasiwasi wangu ni kuwa hakuna demokrasia ya kweli hata pale panapofanyika uchaguzi wa haki wakashinda walioshinda kwa 50.10%. Sasa hawa walioshindwa kwa 49.90% hawana kauli? Hii ndiyo demokrasia.
Kwa maelezo ya Chadema ni kuwa uamuzi wao wa kutoka nje ya bunge ulipitishwa kwenye kikao halali na uamuzi ulikuwa wa kidemokrasia, pengine kwa tafauti ya kura moja tu. Baya zaidi ni pale inapotokea kuwa viongozi wanaokubali uwamuzi fulani ama ni waoga, waramba nyayo au wanaweka mbele masilahi yao binafsi.
Mimi naamini kuwa kuwasimamisha Maalim Seif na Lipumba mara nne si uamuzi wa wana CUF wote, wakati wapo wengine vijana kwa wazee wenye haiba ya uongozi kuwashinda wao, lakini kwa kuwa baraza lao la uongozi limeshaamua, ndiyo hivyo tena. Kwa ufupi, hakuna demokrasia bali "domo-krasia", yaani bla, bla, bla.
Swali si kwamba ni wawakilishi wako au si wawakilishi wako, zaidi ya uwakilishi wa jumla, walitaka kupata maoni yako kuhusu hilo swala au wamekuamulia tu kwa sababu mmeungana kwenye paja moyo wako ukipiga wanausikia?
Kwa sababu leo wataamua hilo, kesho wataamua kodi ipande asilimia 75% ili kuchangia mishahara yao, utasemaje?
Representative democracy is supposed to represent the peoples views, si ndiyo mna mbiu ya "people's power" ?
Unajua wapiga kura wangapi wa CHADEMA wanakubaliana na hili, wangapi hawakubaliani ?
Hawezi kuwa wabunge wa chadema kwahili hata CUF/NCCR/TLP/UDP hawawezi fanya, Ni CCM tu nduo wanao weza kwa akili zao finyu.