Hamza Aziz na karabai za misikiti ya Kariakoo 1940s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,081

Hamza Aziz

Taa ya chemli

20180328_201328.jpg

Msjid Nur Magomeni Mapipa ukimulikwa na taa ya chemli

Hamza Aziz alikuwa mzee wangu na rafiki pia. Nilipokuwa Tanga akinipigia simu kunisalimia tu na mwisho huishia kunipa mwaliko nende kwake nikja Dar es Salaam.

Nyumba yake ilikuwa baharini kabisa na kule ufukweni alijenga kibanda cha makuti kwa ajili ya kupumzika na kupunga upepo.

Hapa ndipo ilipokuwa barza yetu tukikaa muda mrefu sisi wawili tu tukizungumza.

Kwa hakika yalikuwa mazungumzo lakini mzungumzaji khasa alikuwa yeye mimi nilikuwa msikilizaji na wakati mwingine muulizaji maswali.

Nilikuwa wakati mwingine nikumvurumishia maswali mazito. Basi yeye atacheka kisha ataniambia, ‘’Mohamed unajua mimi nina umri wa miaka 74 nimekula kiapo kutunza siri wakijua nimesema watanifunga mimi.’’

Juu ya haya yote Hamza Aziz alikuwa mwingi kazi ya polisi alianza toka akiwa kijana mdogo wakati wa ukoloni hadi kufikia kuwa Inspector General of Police (IGP).

Wakati mwingine nilikuwa nikiwasindikiza watu waliokuwa wakitaka kuja kumuona Hamza Aziz kwa hili ama lile.

Nakumbuka Mzee Kanyama Chiume ni mmoja wa watu ambao nilipata kukaanae pamoja na Hamza Aziz katika kile kibanda cha makuti ufukweni

Katika kibanda hiki siku moja Hamza Aziz alinihadithia maisha yake ya utotoni katika miaka ya 1940 na kazi aliyopewa na baba yake ya kupeleka karabai katika misikiti yote ya Karikaoo.

Miaka ile misikiti ilikuwa haina umeme. Hamza Aziz. Hamza Aziz alinieleza kuwa baba yake siku alipofariki mwaka wa 1951, gazeti la Tanganyika Standard lilitangaza kifo chake kwa kusema kuwa, ‘’Mjenzi wa misikiti amefariki.’’

Hamza Aziz akanambia kuwa karibu misikiti yote ya Dar es Salaam iliyojengwa mwanzo wa miaka ya 1900 alijenga baba yake kwani baba yake alikuwa ‘’Building Contractor,’’ yaani mjenzi wa majumba.

Kwa ajili ya mapenzi haya ya baba yake katika dini Hamza Aziz alikabidhiwa na baba yake Aziz Ali jukumu la kuweka taa katika misikiti yote ya Kariakoo kuanzia sala ya Maghrib.

Hamza Aziz alikuwa akiziwasha karabai nyumbani kwao kisha kuzipeleka misikitini na ikimalizika sala ya Isha anazipitia kuzirejesha nyumbani kwa ajili ya kuziwekea mafuta na kuziwasha siku ya pili zipelekwe tena misikitini.

Hii ndiyo iliyokuwa kazi yake na hii ndiyo ilikuwa hali ya misikiti ya Kariakoo nyakati zile.

Nakumubuka msikiti wa Manyema wa zamani ambao ulijengwa mwaka wa 1912 ukiwa na kisima cha kuteka maji.

Msikiti wa Badawy Kisutu ulikuwa msikiti mdogo ingawa ulikuwa na historia kubwa sana kati ya misikiti yote ya Dar es Salaam.

Hapo palikuwa moja ya misikiti ambayo Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa akisomesha darsa zake za tafsir ya Qur’an na akisomesha masheikh na wanafunzi wengine wadogo, masheikh vijana wanaoinukia.

Darsa nyingine alikuwa akisomesha Sheikh Hassan bin Ameir ni Msikiti Ngazija, msikiti uliokuwa mjini kabisa.

Huu msikiti wa Ngazija ndiyo nadhani ulikuwa kati ya misikiti midogo sana Dar es Salaam ingawa kwa pale ulipojengwa usingewezwa kuitwa msikiti uliokuwa Kariakoo.

Ukija msikiti wa Kiblatein uliokuwa Mtaa wa Aggrey wakati ule (sasa Mtaa wa Max Mbwana), Msikti wa Makonde, Shadhuly yote ilikuwa midogo ambayo kufikia miaka ya 1970 ikawa haitoshi tena kuchukua umma wa Waislam wa Dar es Salaam si sala ya Ijumaa wala ya Eid na ukiondoa hayo hata huduma nyingine zilikuwa hazikidhi haja tena.

Msikiti mkongwe kupita yote Kariakoo ni Msikiti wa Kisutu ulio na umri wa zaidi ya miaka 150.
Msikiti huu sasa unajulikana kama Msikiti wa Mwinyikheri Akida.

Huu ulibaki kwa muda mrefu kama ulivyokuwa ulipojengwa na ni mmoja katika ya misikiti miwili ambayo ilichelewa sana kujengwa upya, huo na Msikiti wa Makonde.

Mwalimu wangu wa historia ya mji wa Dar es Salaam na watu wake Sheikh Ali Abbas alipata kunambia kuwa ikiwa nataka kuona misikiti ilivyokuwa katika miaka ya 1950 nende kusali Msikiti wa Makonde.

Hamza Aziz hii yote ilikuwa misikiti yake akiingia na kutoka katika utoto wake na ikamfanya ajulikane sana ukiachilia mbali kuwa alikuwa mtoto wa Aziz Ali, Mwafrika tajiri na maarufu mjini Dar es Salaam.

Kuanzia miaka ya 1970 misikiti mingi ya Kariakoo ilianza kufanyiwa matengenezo na mingine kuvunjwa kabisa na kujengwa upya na kufanywa ya gorofa mbili hadi tatu.

Hii ilitokana si zaidi ya uchakavu wa misikiti yenyewe bali hii misikiti ilikuja kuwa midogo haitoshi na siku za Ijumaa ikawa watu wanaswali nje juani kwa kutandika majamvi na kufunga barabara na mitaa.

Ikiwa mvua inanyesha hali ilikuwa ngumu sana kwa Waislam na hii ilikuwa adha kubwa.
Lakini ukweli pia ni kuwa misikiti ile ilipitwa na wakati kwa mbali sana.
Imekuwa kawaida siku hizi hapa msikitini petu kusali kiza kwa huku kukatika umeme kwa mara kwa mara kiasi tumeamua kununua taa ya chemli ambayo tunaiweka mbele kibla tunapokuwa hatuna umeme.

Ninapoangalia ile hali ya kiza ndani ya msikiti wakati tunaswali huwa inanijia picha vipi misikiti ya zamani ilivyokuwa hapa Dar es Salaam wakati umeme ulipokuwa bado.

Hapo ndipo huwa namkumbuka marehemu Hamza Aziz na karabai zake.
 
Mungu awasemehe madhambi yao na awerehemu na aifanye pepo kuwa makazi yao, awaepushe na adhabu za kaburi.
 
Mzee Mohamedi, huyu Azizi, ndiye wa Kilwa road unapoelekea Mbagala?
Ule mtaa maarufu na kituo cha kwa Aziz Ali?
 
Mpaka sasa waongo wanaoshikilia rekodi hap JF ni wewe na Yeriko
Kidudu,
Hapana katika dunia yangu uongo ni mfano wa gharika.

Ikijulikana kama mimi ni muongo na maisha yangu kama mtafiti ndiyo itakuwa
mwisho wake.

Yote ninayoandika ni kweli na ikiwa kuna mahali unahisi nasema uongo niulize
nikupe ushahidi wa kauli yangu.
 
Hamza Aziz

Taa ya chemli

20180328_201328.jpg

Msjid Nur Magomeni Mapipa ukimulikwa na taa ya chemli

Hamza Aziz alikuwa mzee wangu na rafiki pia. Nilipokuwa Tanga akinipigia simu kunisalimia tu na mwisho huishia kunipa mwaliko nende kwake nikja Dar es Salaam.

Nyumba yake ilikuwa baharini kabisa na kule ufukweni alijenga kibanda cha makuti kwa ajili ya kupumzika na kupunga upepo.

Hapa ndipo ilipokuwa barza yetu tukikaa muda mrefu sisi wawili tu tukizungumza.

Kwa hakika yalikuwa mazungumzo lakini mzungumzaji khasa alikuwa yeye mimi nilikuwa msikilizaji na wakati mwingine muulizaji maswali.

Nilikuwa wakati mwingine nikumvurumishia maswali mazito. Basi yeye atacheka kisha ataniambia, ‘’Mohamed unajua mimi nina umri wa miaka 74 nimekula kiapo kutunza siri wakijua nimesema watanifunga mimi.’’

Juu ya haya yote Hamza Aziz alikuwa mwingi kazi ya polisi alianza toka akiwa kijana mdogo wakati wa ukoloni hadi kufikia kuwa Inspector General of Police (IGP).

Wakati mwingine nilikuwa nikiwasindikiza watu waliokuwa wakitaka kuja kumuona Hamza Aziz kwa hili ama lile.

Nakumbuka Mzee Kanyama Chiume ni mmoja wa watu ambao nilipata kukaanae pamoja na Hamza Aziz katika kile kibanda cha makuti ufukweni

Katika kibanda hiki siku moja Hamza Aziz alinihadithia maisha yake ya utotoni katika miaka ya 1940 na kazi aliyopewa na baba yake ya kupeleka karabai katika misikiti yote ya Karikaoo.

Miaka ile misikiti ilikuwa haina umeme. Hamza Aziz. Hamza Aziz alinieleza kuwa baba yake siku alipofariki mwaka wa 1951, gazeti la Tanganyika Standard lilitangaza kifo chake kwa kusema kuwa, ‘’Mjenzi wa misikiti amefariki.’’

Hamza Aziz akanambia kuwa karibu misikiti yote ya Dar es Salaam iliyojengwa mwanzo wa miaka ya 1900 alijenga baba yake kwani baba yake alikuwa ‘’Building Contractor,’’ yaani mjenzi wa majumba.

Kwa ajili ya mapenzi haya ya baba yake katika dini Hamza Aziz alikabidhiwa na baba yake Aziz Ali jukumu la kuweka taa katika misikiti yote ya Kariakoo kuanzia sala ya Maghrib.

Hamza Aziz alikuwa akiziwasha karabai nyumbani kwao kisha kuzipeleka misikitini na ikimalizika sala ya Isha anazipitia kuzirejesha nyumbani kwa ajili ya kuziwekea mafuta na kuziwasha siku ya pili zipelekwe tena misikitini.

Hii ndiyo iliyokuwa kazi yake na hii ndiyo ilikuwa hali ya misikiti ya Kariakoo nyakati zile.

Nakumubuka msikiti wa Manyema wa zamani ambao ulijengwa mwaka wa 1912 ukiwa na kisima cha kuteka maji.

Msikiti wa Badawy Kisutu ulikuwa msikiti mdogo ingawa ulikuwa na historia kubwa sana kati ya misikiti yote ya Dar es Salaam.

Hapo palikuwa moja ya misikiti ambayo Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa akisomesha darsa zake za tafsir ya Qur’an na akisomesha masheikh na wanafunzi wengine wadogo, masheikh vijana wanaoinukia.

Darsa nyingine alikuwa akisomesha Sheikh Hassan bin Ameir ni Msikiti Ngazija, msikiti uliokuwa mjini kabisa.

Huu msikiti wa Ngazija ndiyo nadhani ulikuwa kati ya misikiti midogo sana Dar es Salaam ingawa kwa pale ulipojengwa usingewezwa kuitwa msikiti uliokuwa Kariakoo.

Ukija msikiti wa Kiblatein uliokuwa Mtaa wa Aggrey wakati ule (sasa Mtaa wa Max Mbwana), Msikti wa Makonde, Shadhuly yote ilikuwa midogo ambayo kufikia miaka ya 1970 ikawa haitoshi tena kuchukua umma wa Waislam wa Dar es Salaam si sala ya Ijumaa wala ya Eid na ukiondoa hayo hata huduma nyingine zilikuwa hazikidhi haja tena.

Msikiti mkongwe kupita yote Kariakoo ni Msikiti wa Kisutu ulio na umri wa zaidi ya miaka 150.
Msikiti huu sasa unajulikana kama Msikiti wa Mwinyikheri Akida.

Huu ulibaki kwa muda mrefu kama ulivyokuwa ulipojengwa na ni mmoja katika ya misikiti miwili ambayo ilichelewa sana kujengwa upya, huo na Msikiti wa Makonde.

Mwalimu wangu wa historia ya mji wa Dar es Salaam na watu wake Sheikh Ali Abbas alipata kunambia kuwa ikiwa nataka kuona misikiti ilivyokuwa katika miaka ya 1950 nende kusali Msikiti wa Makonde.

Hamza Aziz hii yote ilikuwa misikiti yake akiingia na kutoka katika utoto wake na ikamfanya ajulikane sana ukiachilia mbali kuwa alikuwa mtoto wa Aziz Ali, Mwafrika tajiri na maarufu mjini Dar es Salaam.

Kuanzia miaka ya 1970 misikiti mingi ya Kariakoo ilianza kufanyiwa matengenezo na mingine kuvunjwa kabisa na kujengwa upya na kufanywa ya gorofa mbili hadi tatu.

Hii ilitokana si zaidi ya uchakavu wa misikiti yenyewe bali hii misikiti ilikuja kuwa midogo haitoshi na siku za Ijumaa ikawa watu wanaswali nje juani kwa kutandika majamvi na kufunga barabara na mitaa.

Ikiwa mvua inanyesha hali ilikuwa ngumu sana kwa Waislam na hii ilikuwa adha kubwa.
Lakini ukweli pia ni kuwa misikiti ile ilipitwa na wakati kwa mbali sana.
Imekuwa kawaida siku hizi hapa msikitini petu kusali kiza kwa huku kukatika umeme kwa mara kwa mara kiasi tumeamua kununua taa ya chemli ambayo tunaiweka mbele kibla tunapokuwa hatuna umeme.

Ninapoangalia ile hali ya kiza ndani ya msikiti wakati tunaswali huwa inanijia picha vipi misikiti ya zamani ilivyokuwa hapa Dar es Salaam wakati umeme ulipokuwa bado.

Hapo ndipo huwa namkumbuka marehemu Hamza Aziz na karabai zake.
Allah (s.w) amrehem
 
Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom