Hamu ya kula

BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,474
4,022
Nini kinasababisha kukosa hali ya kula chakula? Na nitawezaje kuwa na hamu ya kula?
Naona kula kama adhabu siku hizi na imeanza ghafla tu.

Asanteni kwa ushauri.
 
Mbona hujafafanua hamu ya kula ipi :hungry: ?
mmmh chichemi kitu, subiri utajibiwa leo mwanzo wa wiki watu wapo fresh..........
 
Mbona hujafafanua hamu ya kula ipi :hungry: ?
mmmh chichemi kitu, subiri utajibiwa leo mwanzo wa wiki watu wapo fresh..........

Chakula cha kawaida,lol..umeenda mbali mkuu he he

Yani nimekosa appetite ya msosi.
 
Inawezekana kabla ya hali hii kuanza umepitisha siku au masaa mengi bila kula na kwahiyo umejikondition. Chagua chakula unachodhani unahamu nacho leo na ule kwa wingi
 
Wewe ni Me au Ke?
Kama ni Ke, kacheck UPT Urine Pregnancy test... yawezakuwa kitu kimejipa!!! mpira ndani ya nyavu..
 
Kama unapata kinywaji,ebu jaribu kunywa sinzano tot kama mbili hivi kisha siklilizia kesho(Hii ni kwa mjibu wa mazoea na inasaidia)

au unaeza kumuona daktari atausadia kwani kuna dawa za kuongeza hamu ya kula baada ya kudhibitisha kuwa hauna tatizo kubwa la kiafya
 
Inawezekana kabla ya hali hii kuanza umepitisha siku au masaa mengi bila kula na kwahiyo umejikondition. Chagua chakula unachodhani unahamu nacho leo na ule kwa wingi

Kweli kuna siku kadhaa zimepita na kuacha mlo mmoja au hata miwili kwa siku.
Nashukuru, acha leo nitafute chakula ninachokipenda.
 
pengine una mawazo au jambo linalokusibu so linakusababishia hiyo hali,
 
Wewe ni Me au Ke?
Kama ni Ke, kacheck UPT Urine Pregnancy test... yawezakuwa kitu kimejipa!!! mpira ndani ya nyavu..

Mimi ni Fem..usiniambie, subiri nikimbie pharmacy kuhakiki hali ila naamini sina.
 
Kama unapata kinywaji,ebu jaribu kunywa sinzano tot kama mbili hivi kisha siklilizia kesho(Hii ni kwa mjibu wa mazoea na inasaidia)

au unaeza kumuona daktari atausadia kwani kuna dawa za kuongeza hamu ya kula baada ya kudhibitisha kuwa hauna tatizo kubwa la kiafya

Mathias sijumii kilevi, hiyo tot sitoiweza. labda niende hospital kupata vipimo. kiafya najiona niko njema lakini hamu ya kula tu imeponyoka
 
Lucky you.

Mimi hamu ya kula full speed. Ningefurahi ikitoweka occasionally - labda na uzito ungepungua.
 
pengine una mawazo au jambo linalokusibu so linakusababishia hiyo hali,

Mkuu inaweza kweli mana kichwa nacho kina mlundiko wa mambo..nitapunguzaje mawazo?

Halafu ulimi una kama ukakasi kwa mbali.
 
Lucky you.

Mimi hamu ya kula full speed. Ningefurahi ikitoweka occasionally - labda na uzito ungepungua.

Nakuonea raha mana mwili wako unakuwa na nguvu..labda kwa hali yako ungeweza kujiwekea kiasi cha kula ili usipitilize mana naona appetite yako inakuletea na uzito pia..

I envy your appetite.
 
Wakati mwingine na rangi ya kupakaaa kwenye midomo(lipstick) ikizidi ina-neutralize appetite...........tehe tehe :A S kiss::A S 465:
 
Wakati mwingine na rangi ya kupakaaa kwenye midomo(lipstick) ikizidi ina-neutralize appetite...........tehe tehe :A S kiss::A S 465:

mkubwa hilo swala ni ukweli? mana jinsi hamu ya kula inavyonisumbua sina budi kuacha rangi ya mdomo..Nieleweshe uhusiano
 
Belinda huyo Jr tu unatuletea :D

Au labda unahitaji vacation ya kuondoka hapo ulipo kwa japo siku mbili.
 
Back
Top Bottom