Hamu ya kula

Belinda huyo Jr tu unatuletea :D

Au labda unahitaji vacation ya kuondoka hapo ulipo kwa japo siku mbili.

Gaijin, unanitisha mweeh! ikiwa hivyo ni majaliwa, acha nithibisishe japo najua sijanasa lol

Idea ya vacation nayo ni nzuri, subiri nitafute muda. Shukrani mkuu
 
Mwazo yanaweza kuchangia, jaribu kujipa muda wa kupumzika na kutafakari mambo yako bila usumbufu.. Jitahidi kutokujilazimisha kufanikisha mambo mengi kwa wakati mmoja kwa sababu hali hii hupelekea kuwa na Stress ambazo zitakufanya usijisikie kula.

Pia jitahidi kunywa maji kwa wingi pamoja na kula matunda kwa wingi ambayo yatakupatia nguvu wakati unapambana na tatizo la kukosa hamu ya kula. Usihofu, hilo tatizo humtokea karibu kila mtu kutokana na sababu tofauti tofauti. Kubwa ikiwa Mawazo au Kuwa na hofu juu ya jambo fulani.
 
mkubwa hilo swala ni ukweli? mana jinsi hamu ya kula inavyonisumbua sina budi kuacha rangi ya mdomo..Nieleweshe uhusiano
tehe tehe kidding nilivyoona hiyo avata yako nikasema kwa hali hii huwezi kuwa na hamu ya kula unashiba hizo lipstick. Ila niliwahi kusikia hizi rangi na mafuta tunayopaka midomoni kadri tunavyoyalamba ndivyo yanavyoleta matatizo hasa kwenye kizazi. Natumaini wataalamu wanaweza kutuhabarisha zaidi. Ila kwa hamu ya kula It was just a joke. ila kama kuna uhusiano sifahamu.

Pengine kwa ushauri kama wapendwa walitangulia, ni vizuri kufuata ratiba ya kula, na chakula cha jioni kama unaweza jitahidi kula mapema izidi saa mbili za jioni na tena kiwe chakula chepesi kinachoweza kusagwa kwa urahisi ukiwa umelala. jitahidi angalau saa moja au mawili yapite baada ya mlo wa jioni ndio ulale. usilale mara tu umalizapo kula. si vizuri kwa afya.

wakati wa mchana kula ushibe na pia pendelea kula matunda kwa wingi. Kila siku unapoamka tumia kijiko kimoja cha chakula cha asali (mbichi ni nzuri zaidi) pamoja na maji ya moto ya kawaida kabla hujaswaka hii itafanya tumbo lako kuwa fresh na kusaidia katika usagaji wa chakula. pendelea pia kutumia juis ya ukwaju mara kwa mara inasaidia kukuepusha na constipation na gesi tumboni.

Punguza vyakula vya nyama nyekundu pendelea kuku na samaki kama wewe ni mpenzi sana wa nyama. nyama nyekundu haisagwi kwa urahisi hasa usiku hivyo kupelekea chakula kuchacha tumboni mara kwa mara matokeo ni kuwa na gesi, constipation, kukosa hamu ya kula na mengineyo mengi.
 
Gaijin, unanitisha mweeh! ikiwa hivyo ni majaliwa, acha nithibisishe japo najua sijanasa lol

Idea ya vacation nayo ni nzuri, subiri nitafute muda. Shukrani mkuu

Ukiamua vacation njoo kwangu nikupikie vyakula vya kinyamwezi Dear najua utakula tu ,vyakula vya asili lakini utamu kujing'ata kidole
 
au bj umeconceive?
well, tumia vidonge vya vitamin b-complex!
 
nikiunganisha ile sredi yako ya ile njemba unyoizimia kazini na hii , naelewa ni kwanini apetaiti limepotea. matatizo yakizidi nione daktari. ww ni spesheli customer cheti chako nitaandika kwa kiingreza.
 
siku nyingine fafanua kabisa hamu ya kula chakula hiki cha kawaida. maana wadau walishaenda mbali sanaa. nadhan umeshapata solution.
 
Back
Top Bottom