Hamtakiwa kiwannda cha Saruji Kanda ya Ziwa kwa nongwa zenu!

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Sababu kutojengwa kiwanda cha saruji Mwanza zaelezwa
Halima Mlacha, Dodoma
Daily News; Tuesday,June 17, 2008 @00:05

SERIKALI imesema hadi sasa kuna ugumu wa kujenga kiwanda cha saruji katika moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni pamoja na Mwanza kutokana na kuwapo kwa tatizo la upatikanaji na gharama kubwa za malighafi ya kuzalishia saruji.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu alisema serikali imekuwa na lengo la kujenga kiwanda cha saruji Mwanza tangu miaka ya 1970 bila mafanikio.

Alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Magu Mjini, Dk. Festus Limbu (CCM), aliyetaka kujua kama kuna uwezekano katika Jiji la Mwanza kuanzishwa viwanda vya bia, saruji na bati kuwapunguzia wakazi wa jiji gharama za kununua bidhaa hizo.

Alisema tatizo kubwa ni malighafi kuu za kutengenezea saruji zilizoko katika mikoa hiyo kuwa hafifu ambazo ni madini aina ya chokaa, udongo mwekundu na jasi na kwamba katika kila tani moja ya malighafi ya kutengenezea saruji asilimia 75 hadi 80 ni madini aina ya chokaa.

“Utafiti uliofanywa kwa kuchukua sampuli kutoka katika mashimo zaidi ya 300 ambayo yalichimbwa katika maeneo ya Bushora, Mwamala, Nyabeho, Mirinuma na Nyamisengeza umedhihirisha kuwa chokaa iliyopatikana haina ubora unaofaa kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na kwamba inaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha madini asilimia 16 aina ya silica ikilinganishwa na kiasi kinachohitajika ambacho ni chini ya asilimia nane,” alisema Nagu.

Alisema ili kuitumia chokaa hiyo ni lazima kuisaga na kuichekecha na baadaye ichanganywe na chokaa yenye ubora zaidi ndipo itumike katika kutengeneza saruji, hivyo mchakato huo pekee ukitumika kutengenezea saruji katika mikoa hiyo, saruji yake itakuwa na bei kubwa kiasi kwamba itakuwa haiuziki.

Hata hivyo, Nagu alisema kwa vile umuhimu wa kujenga kiwanda cha saruji katika Kanda ya Ziwa bado upo, serikali itaendelea na utafiti kubaini maeneo yenye chokaa bora, hali ambayo itapelekea wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza katika kanda hiyo.

Akizungumzia kiwanda cha bati, alisema ili kutengeneza bati mkoani Mwanza, malighafi aina ya ‘hot rolled Colis’ itabidi iagizwe kutoka nje ya nchi hadi Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hali ambayo itafanya gharama ya kusafirisha malighafi hiyo hadi Mwanza iwe kubwa ilinganishwa na malighafi hiyo inapoishia Dar es Salaam.

Ingawa kuna soko kubwa la bati, wawekezaji hawajahamasika kujenga viwanda vya kutengeneza bati Mwanza kwa sababu ya gharama kubwa za kuzalisha bidhaa hiyo ambayo watatakiwa kuiuza kwa bei kubwa hivyo kutoshindana na bei ya bati zinazozalishwa Dar es Salaam na kuuzwa Mwanza.
....................................................

Roho ya kifisadi ni ya Kifisadi tu, mnaona kikijengwa kiwanda Kanda ya Ziwa ambako kuna karibu robo ya Watanzania wote, na mahali kwenye utajiri Mkubwa - ( soko la Uhakika) mtakosa pa kuuzia kwa kuwa biashara ya Saruji mmeimiliki na mnaiendesha na kupanga bei mnavyotaka. Serikali mmeiteka nyara, mmejidai mtapunguza bei lakini mpaka leo hii hakuna kitu. Hivi Chokaa iliypo Meatu, Shinyanga Mjini na Isaka ambayo inadaiwa kuwa nyingi na ya ubora mnaisemaje. Hebu rejeeni kumbu kumbu za Bunge la 1995 - 2000, wakati ambapo ufisadi ulikuwa haujaoota mizizi, licha kuwa ni kipindi hicho ambapo aliibuka fisadi wa Kwanza Tanzania kwa mawazo, ambaye kwa bahati hata uwaziri kanyimwa safari hii.
 
Siku hizi hakuna somo la Jiographia?
 
Kweli fisadi ni fisadi, hata mara moja hafikiri vinginevyo kinyume na atafisadi vipi. Jiulize ni mbinu zipi zinazo fanya bia, soda na sigara zisiwe hivo kwa saruji, bati na misumali. Kwa nn kusiwepo ruzuku ya bidhaa hizo? Kweli, Iko haja ya rais kutoka kanda ya ziwa na asiwe ccm.
 
Back
Top Bottom