"Hamniwezi na kelele zenu hazininyimi usingizi", Lowassa awatambia maadui zake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Hamniwezi na kelele zenu hazininyimi usingizi", Lowassa awatambia maadui zake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jun 4, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwananchi
  Monday, 04 June 2012 08:39

  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amewapiga vijembe aliowaita maadui zake kisiasa wanaomchafua katika majukwaa mbalimbali akisema kuwa, hawamuwezi na hawamnyimi usingizi. Lowassa akitambia maadui zake, kambi yake nayo imezidi kujizatiti baada ya mshirika wake kisiasa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amefanikiwa kukalia kiti cha Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi hivyo kuzidi kuongeza nguvu kwenye bungeni.

  Jana, akiwa mkoani Arusha katika harambee ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Elaira, Lowassa alitumia sehemu ya muda wake kuwapiga vijembe maadui zake pasipo kuwataja majina akisema kamwe hawamnyimi usingizi. Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alitoa kauli hiyo, baada ya Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer kumtaka aendelee kufanya kazi ya Mungu licha ya baadhi ya watu kumkatisha tamaa.

  Akizungumzia kauli ya Askofu Laizer, Lowasa alisema mahasimu wake kisiasa wamekuwa wakimsema kupitia vyombo mbalimbali vya habari, lakini akatamba kwamba juhudi hizo hazitaweza kufua dafu kwake kwani kelele zao hazimnyimi usingizi. "Wanaonisema kwenye magazeti wala hawanisumbui, nasema hawaninyimi usingizi kwa kuwa mimi namtegemea yule anitiaye nguvu daima," alisema Lowasa, kitendo kilichosababisha kushangiliwa na waumini waliohudhuria kanisani hapo.

  Aliongeza kuwa yeye daima humtegemea Mungu amtiaye nguvu na kamwe hawezi kushindwa kulala usingizi kwa kusikiliza kelele zao za mara kwa mara. "Nakushukuru Baba Askofu kwa kunijibia, wale wote wanaonisemasema kwenye magazeti wala hawanisumbui na wala hawaninyimi usingizi," alisema Lowasa. Alisema kwamba yeye ataendelea kumtumikia Mwenyezi Mungu ambaye amtiaye nguvu siku zote bila kujali maneno ya mahasimu wake wa kisiasa.

  Kabla ya kuendesha harambee hiyo, Lowasa aliwaongoza waumini wa kanisa hilo kwa nyimbo zilizopo kwenye Kitabu cha Tenzi za Rohoni na kuibua shangwe kanisani hapo. Kambi yake yajizatiti Chenge ambaye ni mshirika mkubwa wa Lowassa kisiasa amechaguliwa katika kamati nyeti ya Bunge ya Fedha na Uchumi, akizidi kuongeza nguvu kwenye mhimili wa kambi hiyo.

  Lowassa mwenyewe anaongoza Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku mshirika wake mwingine, Peter Serukamba akiongoza Kamati ya Miundombinu. Katika uchaguzi wa juzi wa kamati hiyo uliotawaliwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa bila kuelezwa ilikuwa ikitolewa na kambi ipi, aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti ni Dunstan Kitandula ambaye ni mbunge wa Mkinga. Uchaguzi huo ulikuwa wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dk Abdallah Kigoda aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda hivi karibuni.

  Akizungumzia uchaguzi huo jana, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema, Chenge alipata nafasi hiyo baada ya kumshinda Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa. "Mwambalaswa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi kabla ya uchaguzi, hivyo aliamua kujiuzulu ili kugombea nafasi ya uenyekiti na Chenge, lakini akashindwa," alifafanua Dk Kashillilah.

  Alipotakiwa kuzungumzia mizengwe na rushwa iliyotawala kwenye uchaguzi huo, Dk Kashililah alisema hawezi kuzungumzia hilo kwa sababu hakuwepo kwenye mchakato wa upigaji kura. "Wanaoweza kuzungumzia hilo ni wale waliopiga kura ndiyo wanaweza kuelewa kama kulikuwa na mazingira ya rushwa lakini mimi sikuwapo," alisema.

  Tayari kambi ya Lowassa pia inaonekana kuwa na nguvu katika baadhi ya kamati kutokana na kuwa na washirika wenye msimamo wa wastani akiwemo Agustine Mrema wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) inayoongozwa na John Cheyo, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe na hata Kamati ya Bunge ya Katiba ya Sheria na Utawala inayoongozwa na Pindi Chana
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi sana kama ni mzima huyu mtu!
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tume ya katiba, magamba hayavuliki na Chenge naye apeta huko bungeni...namhurumia kijana fulani vuvuzela!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,845
  Trophy Points: 280
  Kanisa la lutheran bana
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wewe ndo waweza kuwa na matatizo kwa kuwa na wasiwasi na uzima wa mtu.
   
 6. m

  mabhuimerafulu Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hawakuwezi. Hadi sasa sioni kama ndani ya CCM kuna mgombea makini na madhubuti kumshinda Lowassa.
   
 7. s

  sverige JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hata huyu niwale wale watakao kuwa wenye mfumo kristo hatufai
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mungu yupo nawe Mh. Lowassa. Neno la Mungu linatukataza kuhukumu ili tusije tukahukumiwa.
   
 9. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakika muda uwaja lowasa anaweza akashangaza wengi LOWASA NJOO BOKO kanisa la lutheran tunahitajii harambee ya million 200 tumalize mjengo wetu ngojea nikampanga mchungaji akupe mualiko kweli wewe una karama ya uchangishaji mkuu
   
 10. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  Mamvi anadeal na makanisa tu...jamaa anajua kweli kupanda talanta
   
 11. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na vyombo vya sheria na hukumu zisitolewe kwa kuogopa tusije kuhukumiwa na sisi. Mafisadi wasiguswe! Change the way you think.
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Babu wa Loliondo?
   
 13. k

  kicha JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  wakuu naomba contact zake, huku kanisani kwetu lulindi tunamhitaji sana manake waumini choka mbaya
   
 14. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Lowasa ndio zuma wa tanzania wapende wasipende ur the hero and you wil always be the hero....tuko nyuma yako kamanda.
   
 15. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  watakuweza tu usitie shaka
   
 16. S

  Senator p JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aah jamani mie nlizan wabunge wanaimba hip hop na kubana pua 2,kumbe na mipasho.Yaan anakipaj cha kuimba taarabu km mzee yusuph,GAMBA NOMA!
   
 17. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwisha habari yake.
  Mgonjwa huyo.
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  lowasa ana roho ya paka na ni kauzu zaidi ya dagaa!
   
 19. koo

  koo JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunapiga kelele sana lakini sioni namna ccm itaweza kumzuia huyu mtu asigombee urais kwa tiketi ya ccm kinachoweza kumzuia kuwa rais ni umadhubuti wa chadema mungu mjalie afya njema na maisha marefu napenda kuona kitakacho tokea apite asipite kazi itakuwepo
   
 20. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kweli NyinyiEm hawamuwezi Lowassa huo ndio ukweli hata Nepi anajua hvyo na mkerere wake
   
Loading...