Hamna kitu kinaniuma kama watu kuendelea kuamini kuwa kuna uchawi hapa ulimwenguni

Sijui Ni uwoga na hofu sijui Ni ujinga na kukosa maarifa sijui Ni kutomuamini MUNGU sijui kwa kweli shida Ni Nini hasa mpaka mtu anashidwa kujua kanuni zinazoongoza ulimwengu mpaka Sasa hivi..iko hivi sio uchawi tu hata shetani yenyewe hakuna hiko kitu isipokuwa Kuna UJINGA basi.ukitaka kuamini hakuna uchawi chukua Watu 10000 wakalishe chini waambie wakuelezee matatizo yao makubwa mawili yanayowasumbua,wote watakwambia Ni magonjwa na umaskini yaani hawana hela hakuna hata mmoja ambaye atakwambia Kuna mtu anamloga usiku pengine anamsumbua usiku au anamchezea hizo waga Ni stori tu za kijiweni..nakuhakikishia mpaka unakufa hutakuja kuona mtu anapotea,mtu anaruka na ungo n.k.....kila jambo Lina jibu lake tayari ukifa unapimwa Kama ulikufa kwa pressure tunakwambia kabisa kwa hiyo hizo stori za sijui kafa alikuwa mzima zinabakia mdomoni na masikioni kwa wajinga..
Kuna tofauti Kati ya unachokiona na unachokisikia
Hivi hujishangai liuzi lote hilo hauna like hata moja alafu wanao coment wana likes kibao??
 
Yule naibu waziri aliyeshindwa kuapa sio misumari kweli ile
Yule Naibu waziri lazima kapigwa kipapai; yaani ameshindwa kusoma kabisa kiapo? Mtu mwenye Msc Finance anashindwa kusoma Kiapo cha kiswahili?? Kiswahili?? Hatari sana...Inaonekana kuna mtu wa Lindi anaitaka ile nafasi.... Nitamshauri aje kutembelea huku Pemba, wasije wakauchukua na Ubunge wake pia, Maana Unaibu waziri ameshaukosa sasa..
 
Uchawi upo tena saaana! Yaani hata vitabu vya Mungu vinasema uchawi upo na ni kazi za Shetani.
Unless otherwise una Yesu Kristo huwezi kupambana na uchawi.
 
Mkuu shukuru Mungu bado hujafanyiziwa na wachawi!
1.Kuna watu tumelimishwa mashamba na wengine kubebeshwa tofali usiku tanuli zima la tofali 20,000
2.Kuna watu mimba zinachomolewa kila ikifikisha miezi 6, wapo pia ambao kila akizaa mtoto anakufa!
3.Wapo watu kila anapolala usiku bati linaanza kupigwa na nyundo mithili ya fundi anayeezeka paa wakati wewe umelala ndani, alafu mbaya zaidi wakati hayo yanatokea kwako majurani zako wote kimya hakuna anayesikia kitu!
4.Wapo watu wanateseka na magonjwa ya kupewa kwa uchawi kama vile majipu na upele wa kuwasha.

Mkuu ogopa sana mchawi asikukanie kwa chuki za kibinadamu, ni kheri upate mkosi mwingine lakini sio ule wa kuandamwa na wacahwi!
Namba 3 hapo.

inawezekana ni Psychiatric Disorders na Hallucinations.

Temporal Lobe na Auditory Cortex katika Ubongo zikiwa distorted zinaweza kukufanya usikie Sauti za kufikirika ambazo hazipo (imaginary sounds)

Zipo Disorders na Natural Stimulants mbalimbali zinazoweza kupelekea mtu akapata hitilafu ya kusikia sauti za kufikirika (imaginary voices), Tena stimulants zingine ni natural chemical smell zinazotoka kwenye mimea.

Temporal Lobe na Auditory Cortex katika ubongo ndizo hufanya kazi ya kuchanganua sauti.

Mtu akiathiriwa kwa Disorders au Stimulants zozote zinazoathiri Temporal Lobe na Auditory Cortex, basi bila shaka mtu huyo atakuwa analalamika kuwa anasikia sauti wakati kiuhalisia hizo sauti hazipo.

Namba 4:
Sayansi ya Tiba haijawahi kufika mwisho, hivyo siyo kila ugonjwa utatibika au kugundulika kwa teknolojia ya tiba iliyopo sasa hivi.. ila baada ya miaka mingi pengine karne kadhaa zijazo basi magonjwa yasiyofahamika vizuri hivi sasa, yatafanyiwa tafiti na yatatibika baadae miaka mingi ijayo.

Tukumbuke hata TB na Cholera (kipindupindu) zilkuwa hazitibiki miaka mingi iliyopita, ila hivi sasa zinatibika.

Kuna magonjwa mengine hapo kabla yalikuwa hayana Tiba wala Chanjo ila kadri miaka inavyozidi kwenda watu wanazidi kufanya uchunguzi na kugundua namna ya kutibu.

Sisi Waafrika wengi ideology zetu na culture yetu sisi tangu utotoni tumekuzwa tukiamini kuwa kitu ambacho hatukifahamu tunakimbilia kusema ni Uchawi.

Kuna magonjwa hivi sasa hayatibiki ila baada ya miaka 80 ijayo yatatibika. Sayansi ndo ipo hivyo katika Tiba. inachukua muda hata kama ni miaka 200 lakini inaleta majibu.

Watu wanafanya majaribio na kuandika Data, wengine wanazipitia data na kufanya majaribio tena na tena, wanakufa wanaacha Data vizazi vingine vinapokea na kuendelea walipoishia mpaka jibu linakuja kupatikana.

Maarifa ambayo wanadamu tunayo kuhusu DNA bado ni madogo sana. Siku binadamu akiweza kumudu DNA ya cells zote za mwili wa binadamu kwa angalau 95% basi magonjwa karibu yooooote yatatibika kirahisi.

Maana mgonjwa yanaharibu seli (cells) za binadamu, na seli za mwili zimeundwa kwa DNA.
ili kuimudu sayansi ya tiba katika ngazi ya DNA itahitaji miaka mingi sana, pengine karne kadhaa.
 
Mkuu shukuru Mungu bado hujafanyiziwa na wachawi!
1.Kuna watu tumelimishwa mashamba na wengine kubebeshwa tofali usiku tanuli zima la tofali 20,000
2.Kuna watu mimba zinachomolewa kila ikifikisha miezi 6, wapo pia ambao kila akizaa mtoto anakufa!
3.Wapo watu kila anapolala usiku bati linaanza kupigwa na nyundo mithili ya fundi anayeezeka paa wakati wewe umelala ndani, alafu mbaya zaidi wakati hayo yanatokea kwako majurani zako wote kimya hakuna anayesikia kitu!
4.Wapo watu wanateseka na magonjwa ya kupewa kwa uchawi kama vile majipu na upele wa kuwasha.

Mkuu ogopa sana mchawi asikukanie kwa chuki za kibinadamu, ni kheri upate mkosi mwingine lakini sio ule wa kuandamwa na wacahwi!
namba 1 hapo ni hizo ni stori tu, hakuna kitu kama hicho bali hizo ni Fairytale, Folklore na Hearsay tu.

Kamchukue Donald Trump basi ukamlimishe mashamba na kumbebesha tofali 20,000. Trust me utapata utajiri au ukwasi mkubwa sana ukimpeleka Middle East kule na maeneo ya Persian Gulf.

Au mchukue huyo anayekuambia anaweza kulimisha watu ili amchukue Governor wa Benki Kuu na mkamlimishe hayo mashamba.

Nasema hiviiiiiiiii.. Kama hayo yote yangewezekana basi watu wasingehangaika kuwekeza billions of dollars katika kutengeza Rockets na Jet-fighters, Software, Machine etc.
 
Kwenye vitabu vya dini uchawi umetajwa. Wewe nan upinge?
Dini ni imani. Na imani ni kuamini.

Hivyo mtu anachagua kuamini au kutokuamini.

Sitaki kuingilia sana masuala ya kidini, amini kile unachokiamini katika maandishi yoyote ya vitabu vya kidini yaliyoandikwa.

Cha muhimu ni UPENDO (Upendo kati yako na Muumbaji wa Ulimwengu na Upendo kati yako na Wanadamu wenzio)

Pia zipo dini nyingi sanaaaa duniani. Na pia yapo maandishi mengi sana ya kidini yaliyoandikwa na binadamu pia.

Tukumbuke kuwa, siyo kila mtu anaamini katika BIBLIA, TANAKH, BHAGAVAD GITA au QURAN.

Narudia kusema kikubwa ni Upendo. Na hapo ndipo ninapozipendea hizi dini za Mashariki ya Kati, huwa zinahimiza upendo.

Hata zile Amri 10 za hizo dini za mashariki ya Kati ukizichunguza vizuri zile Amri 10 zote zinahimiza Upendo (upendo kati ya Muumba na mwanadamu, na Upendo kati ya Mwanadamu na Mwanadamu).

Uchawi ni fikra ya kufikirika ambayo watu wamekaririshwa tangu utotoni.

Pengne ndiyo maana Dini za Mashariki ya Kati zinawakataza kuamini sababu zinajua fika hakuna kitu kama hicho, zinamuokoa mwanadamu katika kupoteza muda kuamini kitu ambacho ni fikra tu na hakipo.

Na mara nyingi mtu akipata matatizo au majanga kama vile Misiba (vifo), Magonjwa, Kufeli au Kupata Hasara, Ajali etc. ndiyo hukimbilia na kusema karogwa.

Watu tunasahau kuwa matatizo (majanga na changamoto) yapo kwa kila mwanadamu.

Kila mtu anayo matatizo (changamoto) yake, Haijalishi uwe ni Tajiri, Mtu wa Uchumi wa Kati au Masikini.

Tunatofatiana tu aina na uzito wa matatizo (majanga, ajali na changamoto) ila kila mwanadamu anayo matatizo.

Na hapo kwenye matatizo ndipo watu hukimbilia kusema wamefanyiwa uchawi.

Watu tunafurahisha sana.

Sana sana watu Masikini na Watu wa Uchumi wa Kati ambao tumekulia Vijijini au Uswahilini Mijini ndiyo wengi wetu tunaamini tunarogwa au kufanyiwa uchawi.

Kwa ajili za hivyo, aisee acha tu Afrika tuendelee kutawaliwa!
 
Mkuu shukuru Mungu bado hujafanyiziwa na wachawi!
1.Kuna watu tumelimishwa mashamba na wengine kubebeshwa tofali usiku tanuli zima la tofali 20,000
2.Kuna watu mimba zinachomolewa kila ikifikisha miezi 6, wapo pia ambao kila akizaa mtoto anakufa!
3.Wapo watu kila anapolala usiku bati linaanza kupigwa na nyundo mithili ya fundi anayeezeka paa wakati wewe umelala ndani, alafu mbaya zaidi wakati hayo yanatokea kwako majurani zako wote kimya hakuna anayesikia kitu!
4.Wapo watu wanateseka na magonjwa ya kupewa kwa uchawi kama vile majipu na upele wa kuwasha.

Mkuu ogopa sana mchawi asikukanie kwa chuki za kibinadamu, ni kheri upate mkosi mwingine lakini sio ule wa kuandamwa na wacahwi!

Nitafute mm Mnganga No 1 watakuheshimu
 
Sijui Ni uwoga na hofu sijui Ni ujinga na kukosa maarifa sijui Ni kutomuamini MUNGU sijui kwa kweli shida Ni Nini hasa mpaka mtu anashidwa kujua kanuni zinazoongoza ulimwengu mpaka Sasa hivi.

Iko hivi sio uchawi tu hata shetani yenyewe hakuna hiko kitu isipokuwa Kuna UJINGA basi.ukitaka kuamini hakuna uchawi chukua Watu 10000 wakalishe chini waambie wakuelezee matatizo yao makubwa mawili yanayowasumbua,wote watakwambia Ni magonjwa na umaskini yaani hawana hela hakuna hata mmoja ambaye atakwambia Kuna mtu anamloga usiku pengine anamsumbua usiku au anamchezea hizo waga Ni stori tu za kijiweni.

Nakuhakikishia mpaka unakufa hutakuja kuona mtu anapotea,mtu anaruka na ungo n.k.....kila jambo Lina jibu lake tayari ukifa unapimwa Kama ulikufa kwa pressure tunakwambia kabisa kwa hiyo hizo stori za sijui kafa alikuwa mzima zinabakia mdomoni na masikioni kwa wajinga.

Kuna tofauti Kati ya unachokiona na unachokisikia
Ngoja nitie timu hapa
 
Nitafute mm Mnganga No 1 watakuheshimu
kama wewe ni mganga namba 1 kweli basi ifute account ya Maxence Melo humu JF.

Pia nenda ukaisaidie Sheffield United FC ili ichukue Ubingwa wa EPL msimu huu wa 2020/21. Hapo utapiga pesa mingi sana..

Waganga wapiga ramli ni matapeli kama matapeli wengine, Kama kweli ramli zao zinasaidia basi wangesaidia Watoto zao wapige Division 1 za maana huko sekondari.. Waswahili tunasema, "Akili kumkichwa "

kuna sehemu nilikutana na Bango la Mganga anajinadi anaweza kusaidia Mtu kupata Utajiri na pia anasaidia Wanafunzi kufaulu Masomo yao. Daaahh! Nikacheka sanaaaa..
 
Ndo matatizo ya watoto waliozaliwa na kukulia mjini uku wakifungiwa ndani au geti Kali, mkuu tembea uione dunia. Kuna siku utarudi kwenye huu Uzi na kutuomba msamaha. Pia usitumie logic kuelewa mambo ya uchawi na imani
 
Sasa kwa mtu Pagan ambae haamini ktk Maandiko Matakatifu unawezaje kumsaidia aweze kuamini maana anakuwa hana msingi wa Mafundisho ambayo yameainisha uwepo wa uchawi.

Haamini ktk Biblia wala Koran Takatifu!
 
Mkuu shukuru Mungu bado hujafanyiziwa na wachawi!
1.Kuna watu tumelimishwa mashamba na wengine kubebeshwa tofali usiku tanuli zima la tofali 20,000
2.Kuna watu mimba zinachomolewa kila ikifikisha miezi 6, wapo pia ambao kila akizaa mtoto anakufa!
3.Wapo watu kila anapolala usiku bati linaanza kupigwa na nyundo mithili ya fundi anayeezeka paa wakati wewe umelala ndani, alafu mbaya zaidi wakati hayo yanatokea kwako majurani zako wote kimya hakuna anayesikia kitu!
4.Wapo watu wanateseka na magonjwa ya kupewa kwa uchawi kama vile majipu na upele wa kuwasha.

Mkuu ogopa sana mchawi asikukanie kwa chuki za kibinadamu, ni kheri upate mkosi mwingine lakini sio ule wa kuandamwa na wacahwi!
Mwambie huyo, au anafikiria wote walioa hao wanawake waliwapata hivi hivi

Au anafikiria hao anaowakenulia meno na kuwafurahia ni jambo la kawaida

Uchawi upo kwenye nyanja nyingi mkuu upo uchawi wakupendanisha na kufarakanisha pia ndiyo maana unashangaa ktk ndoa hakuna amani kumbe kuna mtu kafanya yake tayari

Mkuu asikwambie mtu hii Dunia inavioja hii dunia ina siri nzito watu wanafanya mambo ya kutisha ili mradi pesa isipotee, watu wamejawa roho za ukatili sana
 
ila sishangai maana mtu tangu utotoni mpaka sasa yupo umri wa miaka 20s muda wote huo miaka yoooote hiyo amekuwa akisikia na kuambiwa stori za wachawi.

Hivyo kumbadilisha akili mtu wa hivyo ni kazi kubwaaaa sana ambayo kwa asilimia 96% kuna uwezekano utashindwa.

Hebu fikiria mtu tangu utotoni amejengwa kiakili na watu kuwa ndege Bundi ni uchawi, Fisi ni uchawi..

Mtu anaamini kabisa kuwa watu wanapaa kwa kutumia Ungo. Hapo huwa nacheka sanaaaa.

Hivi kweli makampuni makubwa ya Aviation (avionics) kama LOCKHEED, BOEING, AIRBUS, EMBRAER, BOMBADIER etc. kwa nini yawekeze billions za dola katika kufanya tafiti na kutengeneza ndege kama kweli mtu anaweza kupaa kwa ungo kirahisi na kufumba na kufumbua akatokea nchini China au Uholanzi katika mji wa Amsterdam.

Honestly, mimi natafuta mtu wa Ungo huyo ili tupeleke hiyo teknolojia Airbus kule tupate mabilioni, au tuanzishe Kampuni yetu ya Ungo Aviation Engineering Limited tuwatoea Boeing na Lockheed kwenye soko.

Afrika vichekesho ni vingi!
Fairytale watu wameziamini na kufanya ni ukweli.

Mtu anajiita mtu wa dini na anadai anamuogopa Mungu, lakini ukifuatilia stori zake vizuri utagundua anaogopa imani potofu sana kuliko imani ya dini aliyonayo.

Shetani wa kwenye vitabu vya dini hana nguvu kihivyo, kama angekuwa na nguvu hizo kama watu wanazodai anazo basi Binadamu wote tungekuwa tushafutika katika Uso wa dunia miaka mingi iliyopita.

Shetani ni ile nia ovu mtu aliyonayo.

USA, CHINA, RUSSIA zisingekuwa na budgets kuuuubwa hivyo ya mabilioni katika MILITARY OPERATIONS na NATIONAL DEFENSE & SECURITY, badala yake zingewekeza katika Uchawi na Kuroga.

NB: Neno langu siyo sheria, hivyo amini unachokiamini. Imani ni kuamini.

ila chondechonde, usifundishe watoto kuwa hakuna kufanikiwa au kufaulu katika mambo mbalimbali ya shuleni na kiuchumi bila kushiriki katika imani potofu.

Tangu na tangu katika Ulimwengu, watu wanaofanikiwa na kuwa Top of the Game huwa ni wachache, that is a balance of nature.

Utajiri na Kufanikiwa Ni kama kupata "A" ya Pure Mathematics vile, siyo kila mtu atapata ila tusichoke kupambana kutafuta Mafanikio na Utajiri.

Back
Top Bottom