Hamna Haja ya Uchaguzi 2020

Ab5

Senior Member
Dec 3, 2017
151
99
Kama mnavyo fahamu hakuna kitu expensive kama vile uchaguzi mfano uchaguzi wa jimbo la kinondoni peke yake unakadiriwa kugharimu sio chini ya TSH Bilioni moja, Hilo ni jimbo moja tu kwenye hiyo bilioni moja ongeza na damu za watu wasio na hatia zilizo zilizomwagika including ya mwanachuo huyu binti mdogo akwelina mungu ampuzishe pema....
so just imagine Tanzania ina majimbo mangapi afu yote yafanye uchaguzi na hali iwe kama hii ya kinondoni
hii ni 2018 so baada ya miaka miwili tunarudi tena kwenye gaharama zilezile, wakati wapo watoto wamsikini wamekosa mikopo ya vyuo kikuu kwa kuwa hawasomi education, wakati hosipitali za serikali hazina dawa, wakati shule za elimu bure hazina vitabu, wakati vijana wasio na ajira na shahada zao haoni dalili za kuajiriwa wakati wakati hakuna pesa za kuona bunge live

ipo wazi tunarudi kwenye monopartysystem sioni ishara yeyote ya upinzani kuchua hata kata moja ya udiwani ukiiangalia kwenye uchaguzi wamarudio wa madiwani ccm walishinda kata zote isipokuwa moja tu, na huu wa siha na kinondoni wameshinda ccm kwa kishindo..kwani watakuja na mbinu gani mpya???? wakishapoteza kata na majimbo yote tutabakiwa na chama gani?

pia hata muamko wawatu kupiga kura ni mdogo saaana wana hofu ya machafuko na wanaona kura zao hazibadlishi chochote.

hivyo kuliko kuingia kwenye gharama na machafuko huku tukiwa tunajua mshindi ni nani bora tuache....
 
Back
Top Bottom