Hamisi Kigwangalla's Letter to Peter Ross Sullivan, CEO Resolute Mining Ltd

Ni uhaini kudhani tukiwaambia ma-capitalist kwamba sisi ni masikini watatuhurumia..... Tujifunze kunegotiate kwa hoja! Hii kujifanya haya mambo hatukuyaona ni kuendekeza upuuzi (hali ya kupuuzia maswala ya msingi).

Kiongozi mmoja (waziri wa madini) anashiriki kuunda sera ya madini, kiongozi huyo (waziri wa mambo ya nje) anatumika kuzunguka dunia nzima kualika kina Resolute, kisha kiongozi huyo anakuwa rais na kushangaa kwa nini sisi ni masikini na watanzania wanamsifia kuwa ni msikivu.....kama sio upuuzi ni nini??

After all ukiwa masikini huhitaji mapesa mengi hivyo mrahaba wa 3% unatutosha......hilo ndio fungu letu!!!!

Kilio cha kutaka huruma ni ishara ya UDHAIFU

Ndg zangu,

Nimeibuka kuwaambia tu kuwa haya mambo hamyajui sana kama mnavyofikiria, na pili hata ukinilaumu mimi leo, unanionea tu. Maana wakati mkataba unasainiwa mimi sikuwepo, nilikuwa nasoma sekondari wakati huo! Na hata hivyo mnailaumu CCM kwani ndiyo inasaini mikataba hii mibovu? Hao wanaofanya hivyo ni watanzania wenzenu watu wa madili hao na wengine wamo kwenye hivyo vyama vyenu mnavyovishabikia! Niwaambieni kuwa pia tuna taarifa za mambo ya hovyo ya kifisadi yanayofanywa na hao viongozi wa vyama vingine mnaowaamini sana nyie...mengi ni mambo ya aibu kwa watu kama mimi siwezi kuyataja hadharani kwa kuwachungia heshima wahusika...pia kwa kuwa siamini sana katika siasa za majitaka.

Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...
 
mkuu hapo kwenye kizungu cha kuchonga,umenena.yaani utazania sio daktari graduate jamani..aisee huyu jamaa nae sijui vipi..sijui kakurupuka..watu kama hawa wanatakiwa waalikwe na adam sumbeye kwenye kipindi chake cha this week in perspective tusikie wanavyo brag.

Kuna watu hamuwezi kuandika kama nilivyoandika mimi...mnajidai tu kukosoa hapa! Hebu semeni ni wapi nimeponda lugha nijifunze tuone...ama mnaona nimekosea tu...bila kusema kosa lenyewe?
 
Poor writing flow, the MP wrote as if he was addressing a political rally
 
Ndg zangu,

Nimeibuka kuwaambia tu kuwa haya mambo hamyajui sana kama mnavyofikiria, na pili hata ukinilaumu mimi leo, unanionea tu. Maana wakati mkataba unasainiwa mimi sikuwepo, nilikuwa nasoma sekondari wakati huo! Na hata hivyo mnailaumu CCM kwani ndiyo inasaini mikataba hii mibovu? Hao wanaofanya hivyo ni watanzania wenzenu watu wa madili hao na wengine wamo kwenye hivyo vyama vyenu mnavyovishabikia! Niwaambieni kuwa pia tuna taarifa za mambo ya hovyo ya kifisadi yanayofanywa na hao viongozi wa vyama vingine mnaowaamini sana nyie...mengi ni mambo ya aibu kwa watu kama mimi siwezi kuyataja hadharani kwa kuwachungia heshima wahusika...pia kwa kuwa siamini sana katika siasa za majitaka.

Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...

Mnafiki mkubwa wewe,umealikwa safari kadhaa na wewe ukajiona Presidential Material,Wanafiki kama nyie CCM Hakuna...eti upande wa pili sijui ndo zaidi,mlivo wazandiki nyie,na hasa wewe Dr wa kuungaunga mngekaa kimya?kingereza chenyewe kibovu,na libarua litaishia kunako dustbin...hauitaji huruma,bali mabadiliko ya sheria
 
Ndg zangu,

Nimeibuka kuwaambia tu kuwa haya mambo hamyajui sana kama mnavyofikiria, na pili hata ukinilaumu mimi leo, unanionea tu.

..ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...

Kaka umejibu kisiasa sana! Kama sisi hatujui ninyi mnaojua mmetusaidiaje??

ukinilaumu mimi leo, unanionea tu. Maana wakati mkataba unasainiwa mimi sikuwepo, nilikuwa nasoma sekondari wakati huo! Na hata hivyo mnailaumu CCM kwani ndiyo inasaini mikataba hii mibovu?
Ukweli mchungu ni kwamba huwezi kuitenganisha CCM na mazuri au mabaya kiuongozi katika nchi yetu..tunapomkumbuka baba wa taifa tunaikumbuka CCM ya wakati wake. CCM ndio wenye serikali inayokusanya kodi na kusaini mikataba kwa niaba yetu...sasa nani abebe lawama?? Ukiukubali ukweli huu itakusaidia sana kiuongozi.

Kusema kwamba wakati mikataba inasainiwa hukuwepo ni kuikana dhana ya taasisi. Unanikumbusha kanusho moja la ikulu kwamba 'jambo hili lilifanyika wakati Kikwete hajawa rais' kana kwamba urais uliondoka na Ben Mkapa au Mzee Mwinyi.
Kwa mfano nikubaliane na wewe kwamba hukuwepo, tuseme nini kwa waliokuwepo?? mfano mzuri ni mwenyekiti wako aliyekuwepo wizara ya madini, akazunguka dunia kualika wawekezaji kisha akawa rais..Kisha mwenyekiti wako naye anashtushwa na umasikini wa wanaNsega kama wewe ambaye hukuwepo unavyostuka.

Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika
Kaka wewe ni mkuu wa familia yako, na ukweli ni kwamba familia yako itakuwa bora kwa kiwango kilekile cha ubora ulichonacho wewe...hakuna miujiza.
Sisi ni wavivu na wazembe sababu hata baba ni mvivu...watovu wa nidhamu coz hata baba anamdhihaki mama mbele yetu.....hatuwajibiki kama baba asivyowajibika kwa matendo yake mwenyewe.....tunaendekeza umaskini maana hata baba anaamini umaskini wetu umeletwa na wageni, akienda kuomba ng'ambo na sisi tunaenda kuomba kwa jirani!!!

Kaka endapo huamini jaribu kufanya hayo uone kama watoto wako watafanya tofauti

Niwaambieni kuwa pia tuna taarifa za mambo ya hovyo ya kifisadi yanayofanywa na hao viongozi wa vyama vingine mnaowaamini sana nyie...mengi ni mambo ya aibu

Not from you....sasa kama wao wanafanya ufisadi inaondoaje wajibu wako binafsi??? Onyesha tofauti yako na wao nasi tutakuwa nyuma yako.

Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala

"Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi" (Dr. H Kigwangalla, 2013) ila tunahitaji uongozi wenye dhamira ya kweli kuleta mabadiliko.
 
Tuchambue hoja sio kuponda kiingereza chake kwani hamjaelewa alichokiandika?acheni ujinga cha msingi ameandika na ameeleweka tujadili hoja kwa kiingereza kitu gani hata kama angepiga broken mbovu kuliko hiyo kama umemuelewa jadili hoja acheni upuuzi huu pengine angeandika rais wa china angekosea zaidi!
 
Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...[/QUOTE]

Dr.HK hapo kwenye RED,
1.0 Kwa mtazamo wako hili tatizo limetokea kwa miujiza au kuna chanzo cha tatizo na ni kipi hicho?nitahitaji ufafanuzi.
2.0 Je mamlaka ina wajibu wowote kuondoa tatizo hilo na vipi inafanya vya kutosha?
3.0 Je ni nini wajibu wa chama kinachotawala kwa wananchi wake?
4.0 Kuna mkakati dhabiti wa kuondoa tatizo hilo unaloona na wapi pa kuanzia?

Dr.HK hapo kwenye Blue,
1.0 Haya matatizo yanaondoleka au ni ya asili?
2.0 Kama kiongozi mwenye dhamana kwa wapiga kura wako,nini mkakati wako...
3.0 Nani mwenye wajibu au aliyepewa wajibu kusimamia na kutekeleza mipango ya kuondoa/kupunguza hayo matatizo
4.0 Je unaamini kuna tiba yake na nini?
5.0 Mtazamo wako:Unaamini rasilimali za nchi hii zimetumika vizuri ukilinganisha na maendeleo tulionayo sasa?
 
Hivi Kigwangalla anaelewa maana ya neno "statesman"?

Naanza kusoma tu sijamaliza intro nataka kutapika.

Not sure I can stomach the full length of this imbecilic ignominy.
 
Daktari,una wazo zuri,lakini umechemka sana tu.,msomi kama wewe sikutegemea grama yakn kuwa mbovu kiasi hichi.alafu hapo umemdhalilisha hadi rais na taifa zima,kwamba wamekuwa weak sana kuingia mikataba mibovu..alafu sijui we are all aware our women and men sijui bla bla nyiingi za nini daktari? Ebu jaribu kucheki na spellings zako pia mkuu
atakujibu kwamba amesomea Sayansi hajasoma linguistic.
 
Kaka umejibu kisiasa sana! Kama sisi hatujui ninyi mnaojua mmetusaidiaje??

Ukweli mchungu ni kwamba huwezi kuitenganisha CCM na mazuri au mabaya kiuongozi katika nchi yetu..tunapomkumbuka baba wa taifa tunaikumbuka CCM ya wakati wake. CCM ndio wenye serikali inayokusanya kodi na kusaini mikataba kwa niaba yetu...sasa nani abebe lawama?? Ukiukubali ukweli huu itakusaidia sana kiuongozi.

Kusema kwamba wakati mikataba inasainiwa hukuwepo ni kuikana dhana ya taasisi. Unanikumbusha kanusho moja la ikulu kwamba 'jambo hili lilifanyika wakati Kikwete hajawa rais' kana kwamba urais uliondoka na Ben Mkapa au Mzee Mwinyi.
Kwa mfano nikubaliane na wewe kwamba hukuwepo, tuseme nini kwa waliokuwepo?? mfano mzuri ni mwenyekiti wako aliyekuwepo wizara ya madini, akazunguka dunia kualika wawekezaji kisha akawa rais..Kisha mwenyekiti wako naye anashtushwa na umasikini wa wanaNsega kama wewe ambaye hukuwepo unavyostuka.

Kaka wewe ni mkuu wa familia yako, na ukweli ni kwamba familia yako itakuwa bora kwa kiwango kilekile cha ubora ulichonacho wewe...hakuna miujiza.
Sisi ni wavivu na wazembe sababu hata baba ni mvivu...watovu wa nidhamu coz hata baba anamdhihaki mama mbele yetu.....hatuwajibiki kama baba asivyowajibika kwa matendo yake mwenyewe.....tunaendekeza umaskini maana hata baba anaamini umaskini wetu umeletwa na wageni, akienda kuomba ng'ambo na sisi tunaenda kuomba kwa jirani!!!

Kaka endapo huamini jaribu kufanya hayo uone kama watoto wako watafanya tofauti

Not from you....sasa kama wao wanafanya ufisadi inaondoaje wajibu wako binafsi??? Onyesha tofauti yako na wao nasi tutakuwa nyuma yako.

"Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi" (Dr. H Kigwangalla, 2013) ila tunahitaji uongozi wenye dhamira ya kweli kuleta mabadiliko.
Umechangia vizuri sana, hongera na nimekusoma. Tungekuwa tuna umakini kama wako, kwa hakika tungekuwa na mijadala mizuri sana na nina hakika tungekuwa na watu wengi zaidi wakijitokeza na kuleta mada zenye faida katika ujenzi wa Taifa...
 
atakujibu kwamba amesomea Sayansi hajasoma linguistic.

Nimegundua watu wengi mna tatizo kubwa sana la lugha na uelewa, na bahati mbaya sana hamuelewi kwamba hamuelewi...
Kuna methali moja ya mafundisho ya kiislamu ikisema 'mtu hawezi kujua ubora wa kitu bora kama yeye si mbora'. Nadhani methali hii na mantiki yake ina-apply sana kwa wengi mnaojaribu kujidhalilisha kwa kukosoa lugha yangu...ni bahati mbaya sana tu kwamba iko juu ya uwezo wenu wa kuelewa na ndiyo maana hamuielewi...Kuna wasomi wengi wamenipigia simu, kuni-PM, na hata kunitumia sms na email wakipongeza content, mtiririko na wakishangaa kuwa eti kuna watu wanaokosoa lugha...mara grama mara hakuna hoja...really???
 
Hivi Kigwangalla anaelewa maana ya neno "statesman"?

Naanza kusoma tu sijamaliza intro nataka kutapika.

Not sure I can stomach the full length of this imbecilic ignominy.

Umejaa vocabulary za kuchungulia kwenye kamusi nawe eti unadhani unajua lugha...hahahaaaaa...nimekufuatilia mara nyingi sana na kugundua you are not a writer wala nini...unanikumbusha enzi zile tukisoma secondary na kushiriki kwenye debate club ambapo tulikuwa tukishindana kwa 'mabomba'
 
Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...

Dr.HK hapo kwenye RED,
1.0 Kwa mtazamo wako hili tatizo limetokea kwa miujiza au kuna chanzo cha tatizo na ni kipi hicho?nitahitaji ufafanuzi.
2.0 Je mamlaka ina wajibu wowote kuondoa tatizo hilo na vipi inafanya vya kutosha?
3.0 Je ni nini wajibu wa chama kinachotawala kwa wananchi wake?
4.0 Kuna mkakati dhabiti wa kuondoa tatizo hilo unaloona na wapi pa kuanzia?

Dr.HK hapo kwenye Blue,
1.0 Haya matatizo yanaondoleka au ni ya asili?
2.0 Kama kiongozi mwenye dhamana kwa wapiga kura wako,nini mkakati wako...
3.0 Nani mwenye wajibu au aliyepewa wajibu kusimamia na kutekeleza mipango ya kuondoa/kupunguza hayo matatizo
4.0 Je unaamini kuna tiba yake na nini?
5.0 Mtazamo wako:Unaamini rasilimali za nchi hii zimetumika vizuri ukilinganisha na maendeleo tulionayo sasa?[/QUOTE]

Mambo uliyoandika ni makubwa na yanahitaji mjadala mrefu sana...na mimi huwa ninayajibu kwa njia ya makala, soma hapa JF 'Majawabu ya Kigwangalla' na utaona fikra na mtazamo wangu.

Pili, nimebaini hukuuliza kwa kuwa unataka kujua ama kuendeleza mjadala kisomi, bali umelenga kunitega na kunishambulia. Nimekoma kushindana na watu wenye nia hiyo maana ushindani haujanisaidia sana. Nimeamua kufanya kazi zangu na kutekeleza majukumu na wajibu wangu ipasavyo bila kujali wengine wanafikiria nini dhidi yangu, na ninajiona ni mwenye afya zaidi kuliko zamani.
 
Tuchambue hoja sio kuponda kiingereza chake kwani hamjaelewa alichokiandika?acheni ujinga cha msingi ameandika na ameeleweka tujadili hoja kwa kiingereza kitu gani hata kama angepiga broken mbovu kuliko hiyo kama umemuelewa jadili hoja acheni upuuzi huu pengine angeandika rais wa china angekosea zaidi!

Hata kiingereza wachambue basi waseme ni wapi nilipochapia...hakuna...wanatoa kashfa tu ambako ziko unfounded...ndiyo haya matatizo niliyoyasema ya wivu wa kisiasa...eti kwa kuwa barua hii imeandikwa na mtu wa CCM na itamuongezea umaarufu basi jealous zinawajaa na kuamua kuponda bila sababu...
 
Hii ni Speech au Letter? Ni malalamiko au maelezo? Ni ya kuomba kazi au Kuomba msaada? Aliyeandika ni google translator au Dr. Kingwangala au Dr Kingwangala? if so inabidi nianze kusoma kingoswe kabla sijaanza kusomea degree ya kwanza......No wonder aliachiwa kiti na Kaka mkuu...

Wewe nawe ndio walewale! Badala ya kubaki kwenye hoja ya Msingi unaanza kuponda ki-english! Shida iko wapi na kimombo hicho. After all why should try write perfect english while Im not British! Mimi Msukuma nimezaliwa usukumani huko kingelesa hii nimeikutia form one na nimefundishwa na mwl wa kibongo

There is this perception with Tanzanians, If you cant speak good english you are Kihio, It real makes sick to my stomach, it makes just wanna puke
If you want perfection with my language let me write in my mother tongue language
Mwone kwanza!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
If ur Government was concerned in helpin its people it would have been the one writting that letter..! The CEO will put ur letter in the dustibin.. because u r not privy to the contract..,why wud he giv a shit about ur letter while ur government embraces him and jubiliate wt him?
Push ur goverment..follow th right course..u right an authoritative letter while u hold no power..to me u sounded very cheap n baseless.,

What u gon do if he aint fulfill ur wishes? Tell ur people to strike? Pinda said already..u strike they kick ur butt..,

Mheshimiwa,if u realy meant to help ur people.,best would v been kuconvice wanaCCM wenzako bungeni to do the right thing , not coming here wt poems n wishful letter..

U can write all the letters u want..,but if u don follower the right path to xpress ur grivance u will always kiss ur resources in nzega goodbye...
 
Ndg zangu,

Nimeibuka kuwaambia tu kuwa haya mambo hamyajui sana kama mnavyofikiria, na pili hata ukinilaumu mimi leo, unanionea tu. Maana wakati mkataba unasainiwa mimi sikuwepo, nilikuwa nasoma sekondari wakati huo! Na hata hivyo mnailaumu CCM kwani ndiyo inasaini mikataba hii mibovu? Hao wanaofanya hivyo ni watanzania wenzenu watu wa madili hao na wengine wamo kwenye hivyo vyama vyenu mnavyovishabikia! Niwaambieni kuwa pia tuna taarifa za mambo ya hovyo ya kifisadi yanayofanywa na hao viongozi wa vyama vingine mnaowaamini sana nyie...mengi ni mambo ya aibu kwa watu kama mimi siwezi kuyataja hadharani kwa kuwachungia heshima wahusika...pia kwa kuwa siamini sana katika siasa za majitaka.

Niseme tu kuwa tuna tatizo kubwa zaidi kama Taifa na wala siyo chama kinachotawala...ni mtu mwenye miopic vision tu anayeona kuishia urefu wa pua yake ndiye anayeweza kushabikia kuwa eti kila kitu ni CCM...tuna tatizo la uvivu, uzembe, utovu wa nidhamu, na kuendekeza umaskini, majungu, wivu wa kijinga na kutowajibika...

Unaweza ukatuambia serikali iliyopitisha sheria ya madini ya sasa, na sera yake, iliyotoa leseni ya uchimbaji kwa hayo makampuni, iliyoingia mikabata ni ya chama gani? Pia mawaziri husika na Rais ni wa chama gani?
 
Pili, nimebaini hukuuliza kwa kuwa unataka kujua ama kuendeleza mjadala kisomi, bali umelenga kunitega na kunishambulia. Nimekoma kushindana na watu wenye nia hiyo maana ushindani haujanisaidia sana. Nimeamua kufanya kazi zangu na kutekeleza majukumu na wajibu wangu ipasavyo bila kujali wengine wanafikiria nini dhidi yangu, na ninajiona ni mwenye afya zaidi kuliko zamani.[/QUOTE]

Dr.HK,
Kwa point yako hapo juu nimeuliza kwa nia njema na ilibidi uelewe hivyo kwani ndo dhamira yangu kuendeleza mijadala kisomi.Ulichofanya ni ubinafsi wa kutotaka kushare ulichonacho na wenzako kuboresha mijadala na kukomaza uwezo wetu wa kufikiria na pia kuimarisha mitazamo yetu kwa yale tunayoyaamini.
Kumbuka HK hii ni jamii na ina watu wenye mitazamo na fikra tofauti usiache na wala usikome kuchangia au kuanzisha mijadala.
Naamini utajibu maswali yangu hapo juu kwa manufaa yetu sote.
 
Back
Top Bottom