Hamisi Kigwangalla juu ya Boda Boda Arusha!

Le Grand Alexei

Senior Member
Nov 9, 2011
116
83
tumetoka kushuhudia picha ya Januari Makamba akiwa ndani ya Bajaji, leo sasa kuna kali ya mwaka Mbunge wa Nzega ame-post kwenye ukurasa wake wa FB picha akivinjari mitaa ya A-town kusaka ATM kwa kutumia usafiri wa Pikipiki, pamoja na kutaka kujionyesha wako karibu na maisha ya kila siku ya wananchi, nadhani Mbunge huyu amehatarisha maisha yake kwa kiasi kikubwa kwa kutokuvaa protective gears, hebu cheki mwenyewe hapa chini:

12210_10151534580468243_1030950183_n.jpg
 
Afu mbona kavaa flip flops?
Sifa za kijinga. Ukaribu na wananchi wakati yeye ndo kapanda for the first time wakati wenzio tunapanda everytime we can afford it!
 
Unafiki mtupu huo!

Kama wanasafiiri kwa bodaboda au pikipiki za kukodi basi warudishe zile milioni themanini walizopewa kununulia mashangingingi. Kisheria pesa zile walipewa ili zitumike kununulia magari imara yatakayowafikisha popoe walipo wapiga kura wao; na wala hazikuwa zawadi kwao kutumia watakavyo kama wabunge.

Iwapo walitumia pesa hizo nje ya malengo yake ya kisheria basi inatakiwa washtakiwe kwa kuvunja sheria inayotawala matumizi ya pesa hizo.
 
No ni uongo hakuwa anatafuta ATM, NILIONA TUKIO ZIMA. YEYE ALIKUWA NA MAMBO YAKE MTAA WA MNAZI MMOJA KARIBU NA BENKI YA NBC ILIYOKO KATIKA JENGO LA MEGA COMPLEX NA SIM ALIYOTUMIA NI BLACKBERRY ALIKUTANA NA DEREVA TOYO UNAYEMWONA HAPO KAMA DEREVA AKAONGEA NAE KUWA ANATAKA KUPIGA PICHA AKIWA KWENYE PIKIPIKI NA MWENYE TOYO AKAMKUBALIA NDIPO AKAIPIGA HIYO PICHA. MUDA HUO ULIKUWA NI MAJIRA KATI YA SAA KUMI NA MOJA NA NUSU HADI SAA KUMI NA MBILI JIONI
 
Hii ni sehemu gani Arusha?
Afu mbona sio the so called Kigwangalla?
 
... kama vile amejiandaa kupigwa picha! Ngoja niinote ID ya mleta mada, huenda ametumwa na Kigwangwalla kuja kuuza sifa za kijinga humu!
 
Kichuguu

kweli ni vema Mnyika akazitumia walau milioni mbili kutengeneza madawati katika shule ya Mashujaa
 
Last edited by a moderator:
Sifa za kijinga!

Ingekuwa ni Tundu Lissu picha ingesifiwa sana tatizo la wanaharakati kila linalofanywa na mtu wa CCM kwenu ni sumu; mimi binafsi siwezi kupanda boda boda ila kama mbunge ameamua kwa utashi wake kupanda boda boda huo ni uamuzi wake; hamuoni hapa amemuwezesha kijana wa watu kupata riziki yake? inawezekana boda boda huyo ni mwana CDM; riziki ya mtu ipo mikononi mwa mtu
 
mimi najiuloza na uwauliza pia... So angetumia shangingi lake kwenda kutafuta hio ATM?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom