Hamis Talatale: Sijamtoa kafara mke wangu ili nipate ubunge, nilimpenda sana haina mfano!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,586
Mbunge wa Morogoro kusini mashariki mh Hamis Taletale aka Babu Tale akijibu swali la mtangazaji Salama Jabir wa Eatv kama kuna ukweli wowote wa habari zilizoeneaga kwamba amemtoa kafara mkewe ili apate ubunge Taletale amesema huo ni uzushi mtupu na alishaupuuza.

Babu Tale amesema hizo zilikuwa ni propaganda tu za maadui zake wa kisiasa lakini wamefeli kwani yeye ni mbunge aliyepita bila kupingwa na ameshaapishwa na sasa anapigiwa saluti na askari wenye nyota mabegani.

Mh Taletale amesema kwa sasa amefocus kuliletea maendeleo jimbo lake ambalo lina matatizo makubwa ya miundombinu ya barabara na ameshamwomba Rais Magufuli amsaidie.

Chanzo: Eatv

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa namna Uchaguzi Mkuu wa 2020 ulivyoandaliwa na kwa tuliyoyaona hadi kuyasikia nikiona Mtu 'anajitapa' kuwa alishinda kweli ninamshangaa.
Mkweli usiyetaka unafiki umerudi,
Nataka nikukumbushe kwamba ndugu yako aliyekuwa anasifika kwa kutokuwa mnafiki (johnthebatist) siku hizi ana Masters ya Unafiki aliyohtimu Chuo kikuu cha Chattle.
 
dear, mbunge au kiongozi yeyote wa kisiasa anapigiwa salute na askari wa majeshi yote hii ni sheria kabisa, kuna kipindi hata ndugai aliizungumzia
Mbunge anapigiwa saluti na askari wa jeshi mwenye nyota 3?

Nakataa kabisa Yohana mbatizaji!
 
Back
Top Bottom