Hamidu Bobali mwenyekiti mpya wa jumuiya ya vijana CUF

Kilaza

JF-Expert Member
Feb 28, 2013
3,324
1,377
JUVICUF ni JUMUIYA YA VIJANA WA CUF.

Natambua kwamba jana kulikuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa katika hoteli ya Lamada - Dar Es Salaam ambapo vijana zaidi ya 300 wawakilishi wa mikoa na wilaya za Bara na Zanzibar walikusanyika kwa ajili ya kukamilisha uchaguzi wa viongozi wa vijana wa CUF taifa.

Nitumie fursa hii kumpongeza comrade Hamidu Bobali kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Vijana wa CUF Taifa (JUVICUF). Natumai atatumia weledi wake,elimu yake, uzoefu wake, kujitolea kwake ndani ya chama na kila juhudi ili kuifanya JUVICUF isonge mbele. Niwapongeze pia wagombea wote waliochaguliwa na ambao hawakuchaguliwa.

Na kwa mwendo huu wa UKAWA, lazima kila chama kiwe na Jumuiya ya vijana mahiri,yenye ujuzi na uwezo na itakayoongeza chachu wakati nchi inaelekea mwaka 2015 ambapo vijana wengi watakuwa wabunge,madiwani na katika nyadhifa zingine za maamuzi. Na ili hilo lifanyike, jumuiya za vijana lazima zihamasishe vijana wajiandikishe na wapige kura kuchagua mabadiliko hasa CUF na UKAWA.

Wakati viongozi wa kitaifa hawalali wanaitangaza CUF, nawe NA WENZAKO msilale katika kuitangaza JUVICUF kwenye ngazi ya taifa na kimataifa.

Vunjeni timu zenu za kampeni na makundi (kama yapo) kisha ingieni mzigoni.

Si mnawaona BAVICHA wanavyoitoa roho UVCCM.
 
Back
Top Bottom