Hamasa kwa wananchi kutumia umeme sana kwenye kuwekeza

MATEGUZYO

Member
Sep 5, 2019
44
17
Tumieni umeme kuanzisha miradi ya maendeleo – Dkt. Kalemani

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaasa wananchi wa Kitongoji cha Mwamagili, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kutumia umeme aliowawashia rasmi Juni 30, 2019 kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na wananchi hao muda mfupi kabla ya kuwasha umeme katika nyumba ya mkazi wa kitongoji hicho, Kashonele Kagodoro, Dkt. Kalemani aliwaambia endapo watautumia ipasavyo, hali zao za maisha zitakuwa bora zaidi.

“Umeme huu siyo kwa ajili ya kuwasha taa peke yake.

Anzisheni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo mashine za kukoboa na kusaga nafaka, saluni za kike na kiume na miradi mingine mbalimbali ili kuinua kipato chenu hivyo kuboresha maisha yenu.”

Aidha, Waziri Kalemani ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo (Chato), aligawa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa nyumba zote 38 za kitongoji hicho, ambazo zilikuwa bado hazijaunganishiwa umeme ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi husika kulipia gharama ndogo ya shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe nishati hiyo.

“Kwa kutumia kifaa hiki cha UMETA, mtaepuka gharama za kutandaza nyaya katika nyumba zenu. Niwaombe na kuwahamasisha muendelee kulipia kwa sababu bei ya kuunganishiwa umeme ni ndogo sana; shilingi 27,000 tu,” asisitiza Waziri.

Katika hatua nyingine, Waziri alilipia gharama za kuunganisha umeme katika Kanisa lililopo eneo hilo, ambayo pia ni sehemu ya kuhamasisha viongozi wa taasisi mbalimbali za umma kulipia gharama za umeme ili ziunganishwe.

Wananchi kadhaa waliopata fursa ya kueleza maoni yao mbele ya Waziri Kalemani, walipongeza jitihada za Serikali katika kuwapelekea nishati ya umeme.

“Hii ni ndoto kwangu. Sikutegemea. Tangu nizaliwe nilikuwa nikiona umeme maeneo ya mijini nilikowahi kutembelea.

Sikuwahi kuwaza kuwa iko siku umeme utawashwa kijijini kwetu, tena katika nyumba yangu,” alisema Kagodolo.

Waziri Kalemani alikuwa Chato kwa ziara ya kazi.
 
Back
Top Bottom