HAMAS yapongeza jitihada za kupokonywa Israel uanachama wa AU

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
HAMAS yapongeza jitihada za kupokonywa Israel uanachama wa AU

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imepongeza na kuunga mkono jitihada zinazoendelea za kuupokonya utawala wa Kizayuni wa Israel kibali cha kuwa mwanachama mtazamaji wa Umoja wa Afrika (AU).

Kiongozi mwandamizi wa HAMAS, Basem Naim alisema jana Jumapili katika taarifa kuwa, harakati hiyo ya muqawama imekaribisha kwa mikono miwili hatua ya Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika ya kuakhirisha mpango wa kuiidhinisha Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa AU.

Katika Mkutano wa 39 wa Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, yalipo makao makuu ya AU, baraza hilo lilitangaza habari ya kuakhirishwa mpango huo hadi Februari mwakani.

Uamuzi wa upande mmoja uliochukuliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU mwezi Julai mwaka huu wa kuupatia utawala wa Kizayuni wa Israel hadhi ya kuwa mwanachama mtazamaji katika taasisi hiyo kuu ya bara la Afrika umelaaniwa ndani na nje ya bara hilo.

[https://media]Musa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU

HAMAS imesema uamuzi huo wa AU si tu utaupa uhalali utawala ghasibu wa Israel wa kuendelea kupora ardhi zaidi za Wapalestina, lakini pia utaushajiisha na kuupa nguvu utawala huo haramu ya kuendelea na njama yake ya kutaka kufuta haki za Wapalestina.

Harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina inasisitiza kuwa, kuuidhinisha utawala pandikizi wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa taasisi hiyo kubwa zaidi ya kibara ni sawa na kuubariki utawala huo uendeleze jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina.
 
Sjui,lakini naamini taasisi kama AU hawawezi kukwepa uhusiano na Israel,wakati mataifa kama Saudia , Morocco na wengine wanaona ni wakati sahihi kuwa na uhusiano na Israel.

Mgogoro wa Israel na palestina haimaanishi wengine tuwe adui wa mmoja wapo au rafiki. Kikubwa ni Au itafaidika na nini kwa Israel kuwa na uanachama wa aina hiyo, au watu wake watafaidika na nini.

Hayo mambo ya Israel ni adui eti kwa ajili ya mgogoro na wapalestina yameanza kupitwa na wakati.
 
Wenyewe wa Africa wanamigogoro mchana na usiku haishi,,
Ukweli huwa unaudhi sometimes lakini inabidi tuukubali.Huwezi kuiita Israel kwamba Ni dola dhalimu,lile taifa liliundwa kwa azimio la umoja wa mataifa la mwaka 1947,kwa hiyo mbele ya sheria za kimataifa lile Ni taifa halali na linalindwa na sheria zote kuanzia mkataba wa umoja wa mataifa.Kwamba imekalia ardhi na haki za watu wengine,Ni jambo baya lakini Kuna taratibu za kufuata ili kutatua hiyo migogoro.Sheria hizohizo zinaipa Israel haki ya kujilinda kwa hiyo kauli na matendo dhidi yake ndiyo yanaipa uhalali wa kutenda inayoyatenda.Kinachotakiwa Ni kuitambua Kama Ni dola halali halafu Sasa taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria zifuatwe ili haki za Wapalestina zipatikane kwa njia za amani.
 
Wangekubali kuja Uganda je? Wangebaki tu hukohuko walipokua ....hapo tayari kulikua na watu wanamiliki hilo eneo , hio UN na mabepari walichokifanya ni ubabe tu......ni kama leo tuseme Wangoni wakalilie kipande cha ardhi Afrika kusini kisa mababu zao walitokea huko
 
Wasingekubali kuja Uganda,pale walikuwa wanapadai toka miaka ya 1880s hivyo walikuwa determined kurudi wanapoamini ni nyumbani kwao.Kuna wengine walizaliwa pale mfano ni Moshe Dayan .Wakati vita ya dunia ya Kwanza ilipoisha maeneo ya miliki ya Ottoman yakawa mikononi mwa Uingereza na Ufaransa na mengine zikaundwa himaya mpya za kiarabu,baada ya vita ya pili maeneo hayo yakawa chini ya udhamini wa UN.Mwingereza mwenyewe alipata taabu Sana alijaribu kuwazuia wayahudi kuhamia pale na Kuna Wakati makao ya serikali ya Uingereza pale Jerusalem yalilipuliwa .Sasa wakati mwingereza anataka kuondoka ilibidi eneo lile lipate serikali na jamii hizi mbili zikidai haki ya kujitawala lkn wakiwa na ugomvi mkubwa ndipo mwingereza akalipeleka UN na eneo likagawanywa kuwa nchi mbili.Huenda Kama nchi za kiarabu zingekubaliana ,historia ingechukua mkondo tofauti,walipoungana na kutaka kuifuta Israel ndo zikaibuka vita ambazo zilizaa matatizo mengi na muendelezo wa yaliyokuwepo.Kilichopo Sasa ni kuangalia tianzie wapi lkn kutaka kuifuta Israel bado kutaleta matokeo ya uharibifu zaidi.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom