Hamas na Jihadul Islami: Lengo letu ni kuifuta kabisa Israel. Je, wataweza?

kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
4,101
Points
2,000
Age
34
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
4,101 2,000
Makundi ya muqawama Palestina: Lengo letu ni kuufuta kabisa utawala haramu wa Israel
Mei 15, 2019 14:13 UTC

Wawakilishi wa harakati za muqawama wa Palestina nchini Iran, wamesema kuwa lengo la makundi ya wanamapambano wa Kipalestina ni kuufuta kabisa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye uso wa dunia.

Khalid al-Qaddumi, Mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya HAMAS mjini Tehran ameyasema hayo Jumatano ya leo katika kikao kilichofanyika kwa mnasaba wa 'Siku ya Kuporwa Ardhi za Palestina' (NAKBA) na kuongeza kuwa makundi ya muqawama wa Palestina yataendelea kupinga mpango wa Marekani unaoitwa 'Muamala wa Karne' hadi mwisho wa tone lao la damu.

Aidha Khalid al-Qaddumi amebainisha kwamba Wapalestina wanajifakharisha kwa kuenzi Siku ya NAKBA (ya kuporwa ardhi zao.) Tarehe 14 Mei ilisadifiana na miaka 71 ya kuondolewa malaki ya Wapalestina katika ardhi zao asilia.

Aidha tarehe 15 Mei inakumbushia miaka 71 ya kuundwa utawala bandia wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina siku ambayo inatambuliwa kwa jina la 'Siku ya NAKBA.'

Mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya HAMAS mjini Tehran Khalid al-Qaddumi ameongeza kuwa, makundi ya muqawama wa Palestia yako imara zaidi kuliko wakati uliopita ambapo yanaweza kusambaratisha njama zote za mabeberu.

Kwa upande wake Nasser Abu Sharif, Mwakilishi wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina sambamba na kubainisha kwamba Marekani inataka kulitwisha eneo la Asia Magharibi mpango wake wa 'Muamala wa Karne' amesema kuwa, makundi ya muqawama wa Palestina yamejiandaa kikamilifu kupambana na utawala haramu wa Israel na kuutimua utawala huo kutoka katika ardhi za Palestina.

Mpango wa 'Muamala wa Karne' wa Rais Donald Trump wa Marekani umebuniwa kwa kuzishirikisha baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia.
Tags
ISRAEL

My take:jee wataweza bila kujiimarisha?
 
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2018
Messages
2,980
Points
2,000
Richard irakunda

Richard irakunda

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2018
2,980 2,000
Hawataweza hata wafanye nini sana watazidi kupigwa na kunyakuliwa
 
M

Msego

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2019
Messages
248
Points
250
M

Msego

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2019
248 250
Makundi ya muqawama Palestina: Lengo letu ni kuufuta kabisa utawala haramu wa Israel
Mei 15, 2019 14:13 UTC

Wawakilishi wa harakati za muqawama wa Palestina nchini Iran, wamesema kuwa lengo la makundi ya wanamapambano wa Kipalestina ni kuufuta kabisa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye uso wa dunia.

Khalid al-Qaddumi, Mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya HAMAS mjini Tehran ameyasema hayo Jumatano ya leo katika kikao kilichofanyika kwa mnasaba wa 'Siku ya Kuporwa Ardhi za Palestina' (NAKBA) na kuongeza kuwa makundi ya muqawama wa Palestina yataendelea kupinga mpango wa Marekani unaoitwa 'Muamala wa Karne' hadi mwisho wa tone lao la damu.

Aidha Khalid al-Qaddumi amebainisha kwamba Wapalestina wanajifakharisha kwa kuenzi Siku ya NAKBA (ya kuporwa ardhi zao.) Tarehe 14 Mei ilisadifiana na miaka 71 ya kuondolewa malaki ya Wapalestina katika ardhi zao asilia.

Aidha tarehe 15 Mei inakumbushia miaka 71 ya kuundwa utawala bandia wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina siku ambayo inatambuliwa kwa jina la 'Siku ya NAKBA.'

Mwakilishi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya HAMAS mjini Tehran Khalid al-Qaddumi ameongeza kuwa, makundi ya muqawama wa Palestia yako imara zaidi kuliko wakati uliopita ambapo yanaweza kusambaratisha njama zote za mabeberu.

Kwa upande wake Nasser Abu Sharif, Mwakilishi wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina sambamba na kubainisha kwamba Marekani inataka kulitwisha eneo la Asia Magharibi mpango wake wa 'Muamala wa Karne' amesema kuwa, makundi ya muqawama wa Palestina yamejiandaa kikamilifu kupambana na utawala haramu wa Israel na kuutimua utawala huo kutoka katika ardhi za Palestina.

Mpango wa 'Muamala wa Karne' wa Rais Donald Trump wa Marekani umebuniwa kwa kuzishirikisha baadhi ya nchi za Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia.
Tags
ISRAEL

My take:jee wataweza bila kujiimarisha?
Tu-assume kwamba wataweza kuifuta Israel,sasa:
-watapata faida gani?
-kuna uwezekano wa kuwaua wayahudi pekee bila warabu wa Israel?
-kwenye harakati za kuifuta Israel,wao watakuwa salama kiasi gani?
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
3,567
Points
2,000
Age
55
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
3,567 2,000
Huyo gaidi hana lolote ni bangi tu zinamsumbua pamoja na damu za wahanga aliyowaua na ndoto ya kuwaza wale "72 Mythical Virgins of The Imaginary Paradise".
 
Forum statistics

Threads 1,296,486
Members 498,655
Posts 31,249,945
Top