Hamahama zinapoepusha kiama: CHADEMA kuimarika maradufu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,071
2,000
Leo, tarehe 5/12/2017, kwa mara ya kwanza tangu kuanza 'kuchalenjiwa' na mwanangu wa Chuo Kikuu, nimekubaliana naye. Alinipigia simu ya nidhamu na kunisalimu. Leo hakunilaumu. Anajua sishiriki katika mikiki inayotiki ya kuhamahama kinafiki bila urafiki. Akanipongeza kwa kutoshiriki kwangu na kunisihi kubaki na wajihi huohuo.

Mwanangu, anayemalizia Shahada yake ya kwanza ya Sheria, akaniambia jambo la maana. Nimekubaliana naye. Amenidokeza na kukoleza kuwa hii hamahama inayoendelea kutoka upinzani hasa CHADEMA kwenda CCM ni kuepusha anguko la CHADEMA na upinzani kwa ujumla. Akanikumbusha figisu za uchaguzini ambapo wagombea mamluki wanapojitoa katika kugombea katika muda wa lala salama.

Mwanangu akaniambia kuwa, yeye anaamini, wanaohama sasa CHADEMA kwenda CCM walikuwa mamluki wetu CCM. Sasa wanarudi nyumbani. Ni bahati kuwa wanarudi kabla ya uchaguzi. Wanarudi kwa wanachokiamini na kukitumikia. Mwanangu akaniongezea kuwa wanaohama sasa 'walihamia' CHADEMA wakati uliopita. Hoja yake ya haja mwanangu ni kuwa mamluki lukuki wanaotisha kuliko bunduki au mkuki wanarudi wakijaa chuki kuliko weupe wa chaki.

Tukakubaliana kiungwana kuwa hamahama inaepusha kiama na dhahama kwenye vyama. Inasafisha CHADEMA na kuchafua CCM. Kwakuwa, kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Mwanangu akanichokoza kidogo. Eti, nipeleleze hata dau linalotumika kufanya usajili wa kimwili katika siasa za kisasa zinazosafisha kama msasa. Amini nawaambia, CHADEMA itaimarika maradufu.

Kujenga hoja bila bunduki itapendeza sana! Mambo ya expansion joints hayo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
 
Tony antony

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
4,987
2,000
Tukakubaliana kiungwana kuwa hamahama inaepusha kiama na dhahama kwenye vyama. Inasafisha CHADEMA na kuchafua CCM. Kwakuwa, kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Mwanangu akanichokoza kidogo. Eti, nipeleleze hata dau linalotumika kufanya usajili wa kimwili katika siasa za kisasa zinazosafisha kama msasa. Amini nawaambia, CHADEMA itaimarika maradufu.
kwanini tunazungumzia upande mmoja tuu,toka 2015 hadi leo inamaana hakuna waliohamia CHADEMA kutoka CCM??Nyalandu,Lowassa.Sumaye. inamaana hawa walihamia CHADEMA ni afadhali zaidi ya wanaohamia CCM?inamaana waliohamia CHADEMA wameenda kukijenga chama ila waliohamia CCM wameenda kukibomoa chama?
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,087
2,000
Mzee Tupatupa! Kama hao hamahama wa Chadema ni mamluki na walishika nyadhifa kubwa, basi Chadema ifanye sensa upya ya kiitikadi kuwapata wafia chama.
La sivyo, mamluki bado wengi. Ulipo tupo je wamuweka kundi gani miongoni mwa mamluki?
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Hit song "expansion joint"

Single imeuza sana na inarndelea kuuza kwa kuvunja rekodi.
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,312
2,000
kwanini tunazungumzia upande mmoja tuu,toka 2015 hadi leo inamaana hakuna waliohamia CHADEMA kutoka CCM??Nyalandu,Lowassa.Sumaye. inamaana hawa walihamia CHADEMA ni afadhali zaidi ya wanaohamia CCM?inamaana waliohamia CHADEMA wameenda kukijenga chama ila waliohamia CCM wameenda kukibomoa chama?
Jamaa wamejazana ufipa wanajiliwaza wakati jumba linaporomoka. Eti VUTA-NKUVUTE ha ha ha, Mzee Tupa Tupa wa Ufipa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom