Hamad sio kichwa maji, kwa mbumbumbu ni vigumu kumuelewa.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130



maalim-181-564x272.jpg

Na. B.OLE,
Ni muda mfupi tokea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar huku Maalim Seif akiwa anaandika tena historia mpya ya kuwa Makamu wa kwanza wa Serikali ya umoja wa kitaifa hapa petu Zanzibar.Tukumbuke kwamba Maalim Seif aliwahi kushika nafasi tofauti katika mfumo wa chama kimoja, ambapo utendaji wake unaeleweka na wengi Visiwani.
Ni ukweli usiopingika kwamba tumeona na kusikia mengi hadi kufikia leo hii badala ya Serikali ya Mapinduzi iliozoeleka na wengi kusikika nyimbo mpya zinazorindimba na kuashiria kuwepo kwa muundo mpya wa Serikali ya pamoja.
Ukweli wa mambo ni kwamba safari haikuwa ndogo hasa ukidhingatia kwamba Jahazi tulilokuwa tukisafiria lilikuwa la mbao na kusi alikuwa katanda huku mawimbi yakiashiria shari tupu,na kuwapa abiria wakati mgumu huku mioyo yao ikirapa na kuhangaika kwa machungu na mateso ya bahari.
Jicho lote lilikuwa ni kwa Nahodha wa chombo hicho ambae kwa upande wake alikuwa ni mdhoefu na stadi wa bahari yenye kiza na kina kirefu cha maji, ndie alietupa moyo mkunjufu hadi kufikia leo vinywa vyetu vimejaa matusi na kebekh kwa vile tumeshavuuka kimbunga kile.
Tokea kuundwa kwa Serikali hii kumekuwepo na propaganda nyingi, ambazo mimi binafsi sifikirii kwamba ni za kujenga umoja wa Wazanzibar bali nahisi inawezekana ni ajenda Maalum ya kuwabagua Wazanzibar ambao kihistoria wamegaiwa ili watawaliwe daima. Mara nyingi kuna watu hutoa ruma kwamba Maalim Seif haelewani na Rais Shein na Makamu mwenzake, sasa tuwaulize hawa watu wanaopakaza habari hizi wamezipata wapi ? Maalim sio mbumbumbu ni mweledi na hashindwi kuja hadharani kueleza hilo kama ni kweli. Mara ngapi amefanya hivyo, huku akijua kwamba Wananchi walio wengi wangeshindwa kumuelewa kwa muda mfupi na wengine wangeweza kupinga maneno yake lakini kwa vile anajua anachokifanya basi yeye anakuwa sio moga wa kutamka hadharani.
Ni nani kati yetu aliefikiria kwamba Maalim atatoka ndani ya Serikali ya Mapinduzi enzi hizo hata harufu ya vyama vingi haikuwepo, huku yeye akiwa mtu wa pili katika serikali hiyo ? Lakini kama hilo halikumbukwi, kuna mtu yeyote aliefikiria kwamba iko Siku Kiongozi huyu atasimama kwenye kiriri na kada mnasi ya Wazanzibar kumtambua Mh. Aman kama Rais huku akijua na kila mtu akifahamu kwamba yeye ndie alie dhulumiwa ?
Hata hivyo kama hilo halitoshi kumekuwa na baadhi ya watu sijui kwa chuki zao binafsi, au kukosa hoja mahahsusi wamekuwa wakimuandama Makamu wa Rais Maalim Seif kama yeye ndie Rais wa Zanzibar.Huku wengine wakifikiria kwamba maendeleo yatakuja kama mvua ya masika, bila kuelewa kwamba hata sisi wenyewe Wananchi tunashindwa kujielewa tunahitaji msasa kwanza.
Sote tunaelewa kwamba Maalim Seif ni miongoni mwa Viongozi wanaongoza Serikali hii mpya, lakini sio vyema kumpa majukumu na kumbambikizia lawama ambazo sio zake. Yeye kama Makamu wa Rais kiitifaki ni kwamba anaongozwa na Boss wake ambae ni Rais wa Zanzibar, kwa maana hiyo shutma kama zipo basi ni vyema kulengwa huko kwani Dr Shein ambae ndio Rais mteule wa Zanzibar kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi.
Hata hivyo ningependa kutoa nasaha zangu kwa Wazanzibar wenzangu kwamba Maalim Seif sio kwamba ni kichwa maji kama sisi, anajua anachokifanya kwa maslah ya Wazanzibar wote. Tuvute subra tuone wapi tutaelekea, huku tukijua kwamba hii hatua tuliofikia ni kubwa tukilinganisha na huko tulikotoka .
Ni iman yangu kwamba kwa wale wachache wenye akili zao waki angalia vyema historia ya kiongozi huu wataelewa kwamba ni moto wa kuotea mbali,na kweli nuru mpya ya maendeleo imeshaanza kuchomoza Visiwani, kwani hakuna refu lisilo na mwisho.
Ni vyema tukavuta subira ili tuone ni wapi Nahodha huyu atatupeleka Wazanzibar na wapenda maendeleo kwa jumla, kuliko kupwaya kwa maneno yasio leta tija badala ya kulijenga Taifa letu ambalo limeathirika kwa muda mrefu,na tukawa sasa sisi ni vinara wa kubomowa.
Maalim Seif hayupo kwenye madaraka kwa ajili ya ulwa kama baadhi ya watu wengine walivyo na mawazo finyu katika hilo, ni vyema tukamuangalia historia yake ya uongozi wapi ametokea na msimamo wake ni upi kwa Wazanzibar na Zanzibar kwa ujumla.
Mimi kama Mzanzibar sijakata tamaa, nafarijika sana kuona kwamba chini ya uongozi wa Maalim Seif Wazanzibar leo hii wamepata sauti ya kutoa madukuduku yao, tusisahau historia ya huko nyuma hali ilivyokuwa.Iko siku kwa wale mbumbumbu na wenye chuki binafsi na Maalim Seif watamuelewa na kujua ukweli halisi kwani hata enzi za Mitume na masahaba yaliowapata tumeyasoma kwenye vitabu, lakini mwisho hadi leo hii tunafaidika na matunda yao.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom