Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Hamad Rashid Mohamed ni Waziri wa Kilimo wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na ni mbunge kutoka chama cha upinzani cha Alliance for Democratic Change. Mwanasiasa ameonyesha ukomavu mkubwa wa siasa baada ya kuamua kuweka siasa za kulalamika nyuma na kuamua kufanya kazi kama Waziri kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa maendeleo ya wazanzibari.
Tumeona chama cha CUF kikiwa na migogoro isiyokwisha inayosababisha wabunge wa chama hicho kushindwa kuwakilisha waliowachagua kikamilifu. Ni vizuri kwa wabunge wote wa upinzani kujifunza kutoka kwa mwanasiasa huyu mkomavu wa kisiasa kuwa baada ya uchaguzi tunatakiwa tuwe kitu kimoja kwa kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi hii. Natoa pongezi kwa viongozi wa ACT Wazalendo Kitila Mkumbo na Ana Maghwira kwa wao pia kuamua kufanya kazi na serikali ya awamu ya tano. Ni vyema kwa vyama vya siasa baada ya uchaguzi kuangalia vinawezaje kuchangia nini maendeleo ya taifa, demokrasia haimanishii kwa upinzani kuona chochote kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani ni mabaya na ni muhimu kwa vyama hivyo kuheshimu serikali iliyopo madarakani, Kama wabunge watashindwa kuwakilisha wapiga kura wao kikamilifu wajue mwaka 2020 watanzania watakuwa na maamuzi ya kuchagua watu makini wa kuwawakilisha.