Hamad Rashid Mohammed naye kuondoka CUF!

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Katika hali inayoonekana kuwa hali si shwari katika chama cha wananchi(CUF), mmoja wa wanachama na kiongozi nguli kabisa wa chama hicho, ndugu Hamad Rashid Mohammed, mbunge wa WAWI kule Pemba na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anafikiria kuachana na chama hicho kwa kile anachodai kuwa kuwa ni kuwa uongozi wa chama hicho kukosa mikakati thabiti ya kukiongoza, na hata kukifanya kupoteza umaarufu wake wa awali.

Imethibitika kuwa bado kuna mazungumzo anafanya na uongozi wa juu wa chama hicho ambao kama hautabadilika atafuata nyayo za aliye kuwa naibu katibu mkuu wake mh. Wilfred Rwakatare aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Kama mh. Hamad naye atajiengua basi hili litakuwa pigo lingine kubwa kwa CUF.
 
Katika hali inayoonekana kuwa hali si shwari katika chama cha wananchi(CUF), mmoja wa wanachama na kiongozi nguli kabisa wa chama hicho, ndugu Hamad Rashid Mohammed, mbunge wa WAWI kule Pemba na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni anafikiria kuachana na chama hicho kwa kile anachodai kuwa kuwa ni kuwa uongozi wa chama hicho kukosa mikakati thabiti ya kikiongoza, na hata kukifanya kupoteza umaarufu wake wa awali.

Imethibitika kuwa bado kuna mazungumzo anafanya na uongozi wa juu wa chama hicho ambao kama hautabadilika atafuata nyayo za aliye kuwa naibu katibu mkuu wake mh. Wilfred Rwakatare aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

Kama mh.Hamad naye atajiengua basi hili litakuwa pigo lingine kubwa kwa CUF.

EPA zinafanya kazi iliyokusudiwa haya lete vitu tupo sie wasikilizaji
 
Je hii habari imethibitishwa mkuu au bado iko kwenye stage ya tetesi?
Hata ikiwa ni tetesi. Mimi nampongeza Bw. Hamad Rashid kama atachukua hatua hiyo. Anaweza kuwa kiongozi wa "the alternative Party" na tukaiendeleza Zanzibar (ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) . Ni Mwanasiasa mahiri sana huyo!
 
Last edited:
Nafikiri habari hii ni ya kutunga tu.

PEMA na CHADEMA ni sawa na KURA ZA MARUANI
 
Hata ikiwa ni tetesi. Mimi nampongeza Bw. Hamad Rashid kama atachukua hatua hiyo. Anaweza kuwa kiongozi wa "the altenative Party" na tukaiendeleza Zanzibar (ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) . Ni Mwanasiasa mahiri sana huyo!

Naimani jamaa zanzangu SMZ &MBM watasoma haya maoni yako leo unawambia kuwa mutawaendeleza zanzibar ?ama kweli sasa umewachoka, kina kaka karume kwa kwetu hapa zanzibar hayo ni matusi ya nguoni, ni sawa kumwambia mtu mzima avuwe nguo zake zote na kwenda (kutembea)uchi kutokea mji mkongwe hadi mazizini. Umesha sahau mheshimiwa ALI bin JUMA Bin shamuna huko nyuma alishawahi kusema hawajaa wanatuarau na kutuona sisi ni wajinga (kumbuka jaraha likitoweka kovu itakukumbusha)
 
Last edited:
Kama ni kweli itakuwa ni fedha za RA zimeanza kuwasambaratisha. Wanasiasa makini wa upinzani wa kweli hawawezi kukubali kuishi kwa kufadhiliwa na fisadi RA.
 
Kama ni kweli itakuwa ni fedha za RA zimeanza kuwasambaratisha. Wanasiasa makini wa upinzani wa kweli hawawezi kukubali kuishi kwa kufadhiliwa na fisadi RA.

Mimi mbona nilisikia tetesi kama Zito Kabwe anataka kufuata nyayo za God Father wake the Mighty Aman Kaborou. Maana Kaburu ndio chachu ya Zitto kwenda Chadema.

Hata hii ya kung'atuka kugombea ubunge ni janja tu. anajiandaa kurudi nyumbani. Believe me.
 
Mkuu hapo juu sijaongelea Zitto wala Chadema. Thread inahusu Hamad Rashid Mohammed kuondoka CUF!
 
Kama ni kweli itakuwa ni fedha za RA zimeanza kuwasambaratisha. Wanasiasa makini wa upinzani wa kweli hawawezi kukubali kuishi kwa kufadhiliwa na fisadi RA.

kama zilivyo msambaratisha Lwakatare na kumpeleka Chadema!
 
Mimi mbona nilisikia tetesi kama Zito Kabwe anataka kufuata nyayo za God Father wake the Mighty Aman Kaborou. Maana Kaburu ndio chachu ya Zitto kwenda Chadema.

Hata hii ya kung'atuka kugombea ubunge ni janja tu. anajiandaa kurudi nyumbani. Believe me.

1. Nilijiunga CHADEMA kabla ya Kabourou. Mimi nilijiunga mwaka 1993, nikiwa kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Kigoma. Yeye alikuja mwaka 1994 kugombea Ubunge kuziba nafasi ya Marehemu Rajabu Omar Mbano.
2. Sijawahi kuwa mwanachama wa CCM na hivyo hakuna kitu kurudi nyumbani. Toka nimekuwa na umri wa kujiunga siasa nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu CHADEMA na ninamwomba sana Mungu uhai wangu uishie katika chama hicho tu. Inshaallah
3. Kutangaza kwangu kutogombea hakuhusiani na hata kidogo na uzushi wako hapo juu. Nimeshasema ni kwa nini niliamua kutoomba kipindi kingine cha Ubunge. Hata hivyo, kwa kuwa ni maamuzi yangu ninaweza kubadili msimamo wangu huo na kugombea tena na kushinda. Nipo huru kuamua ninachoona inafaa!
 
Hamad namshauri ajiunge Chadema ili wagombee Urais pamoja na Slaa 2010 tutawapa,nyota zenu zinang'aa.
 
Back
Top Bottom