Hamad Rashid Mohamedi na kamati za Bunge kubadili sheria za madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid Mohamedi na kamati za Bunge kubadili sheria za madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanyanga, Jul 18, 2011.

 1. k

  kanyanga Senior Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika kuchangia hotuba ya Ngeleja, Mh.Hamad Rashid amewataka wabunge wenzake kubadili sheria za madini kwa kutumia kamati za bunge ambazo zimepewa mamlaka hayo kisheria.Wazo hilo la Hamad Rashid limekuja baada ya kuongelea mkataba wa hovyo sana katika mgodi wa Mwadui Shinyanga.Nashindwa kuelewa hizi sheria nyingine zinazopigiwa kelele na hawa wabunge,zinaonekana za ajabu kana kwamba hazikupita hapo mjengoni.Nchi hii inazo sheria nyingine nzuri sana lakini kuna sheria nyingine za hovyo kuliko maelezo ya kawaida, na hawa viongozi tuliowapa dhamana ya kuongoza nina hakika wengi wao wanatumia KAMASI badala ya UBONGO katika kufikia maamuzi,na mara nyingi hupenda kutumia zile sheria za hovyo ili kufikia malengo yao.

  Ndugu zangu suala la katiba mpya ni muhimu sana, kwa kuwa huo UPUMBAVU na UJINGA wanaotufanyia viongozi hao unaweza kukomeshwa kwa kila kitu kuwekwa kwenye katiba na Sheria zikabadilishwa ili kuwadhibiti WAHUNI hao.Nasema ikidhihirika kwamba kuna MUHUNI ametuzidi akili kwa muda fulani ana akafanikisha UFISI-ADI, hiyo issue tusimwachie Mh.CJ Chande pekee yake kupekua adhabu kwa kutumia Torch,adhabu itamke wazi kabisa kwamba UTANYONGWA NA KUTOA KINYESI HADI ROHO IACHE MWILI.Ule ujanja wa kumwachia President mamlaka ya kubadili adhabu ufutwe ili kutoa fursa ya kuwashuglikia hawa WAHUNI.

  Haiwezekani kila siku watu wazima na akili zetu tuzungumze jambo moja kana kwamba hakuna shuguli nyingine za kufanya.Kamati ya Mwakyembe kuhusu Richmond ilipendekeza kwa Serikali kukoma kukodisha maitambo ya kufua umeme.Leo hii tunashugulika na mjukuu wa Richmond (Symbion) sasa kama huku si kulogwa ni nini.Nchi hii haiwezi kushindwa kununua mitambo, lakini kwa kuwa WAHUNI wanajua kuna Pesa wanavuta kutokana na kukodisha mitambo hawataki ushauri wa mtu.Wana JF tukomae na mchakato wa katiba mpya.
   
Loading...