Hamad rashid mohamed : Maalim seif ana hatia, afungwe jela..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad rashid mohamed : Maalim seif ana hatia, afungwe jela.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Aug 20, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake wameendelea kuwang'ang'ania wadhamini wa Chama cha Wananchi (Cuf), wakiiomba Mahakama Kuu iwatie hatiani na kuwafunga kutokana na kitendo cha kufukuzwa kwao uanachama.


  Licha ya wadhamini hao, wengine ni wajumbe wa Baraza Taifa la Uongozi la chama hicho akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad. Januari 10, mwaka huu Rashid na wenzake 10 waliwasilisha mahakamani hapo maombi wakitaka iwaite wadhamani wa chama chama hicho, wajieleze sababu za kutotiwa hatiani na kufungwa kwa kosa la kupuuza amri ya mahakama.


  Maombi hayo yalitokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho wa Januari 4, mwaka huu kuwafukuza uanachama wa chama hicho na kuwasimamisha wengine. Pia, katika maombi hayo wanaomba mahakama ibatilishe uamuzi wa Baraza hilo wa kuwavua uanachama kwa madai kwamba walikiuka Katiba ya Cuf.


  Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, Hamad na wenzake katika hoja zao za maandishi walizoziwasilisha mahakamani kupitia kwa Wakili wao, Augustine Kusalika wanadai baraza hilo liliwafukuza uanachama wakati tayati likiwa na amri ya mahakama kuzuia kuwafukuza.


  Amri hiyo ya mahakama ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari mwaka huu kufuatia maombi waliyoyawasilisha Januari 3, chini ya hati ya dharura.

  MY TAKE:

  Nampa heshima Hamad Rashid kwa kuendelea kupigania haki yake, asiwe kama Kafulila ambaye baada ya kuona anaupoteza ubunge kaanza kuomba wakae meza moja na watawala ambao yeye mwenyewe anawaita kuwa ni wabovu.

  Source: Mwananchi
   
 2. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,892
  Trophy Points: 280
  kafulila hakuishia kuomba tu alipiga magoti na kuanza kuomba asmehe huku akilia! hao ndio vijana eti wana ndoto za urais, kweli kiti cha urais kimekuwa so loose kiasi kila mjinga anahisi anaweza kukikalia!
   
 3. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Waacheni Wafu Wazikane
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sasa inaanza kudhihirika kuwa Maalim Seif ni mhalifu wa kisiasa.
   
Loading...