Elections 2010 Hamad Rashid kuwania Uspika wanachadema ni nani ?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Hamad Rashid kuwania Uspika


Salim Said
ALIYEKUWA Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed, amesema huenda akachukua fomu ya kugombea kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatua hiyo inafuatia tetesi kwamba, huenda akachukua fomu kuwania kiti hicho ambacho kimekuwa kikishikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza kwa simu kutoka kisiwani Pemba jana, Hamad alisema hawezi kuthibitisha moja kwa moja, lakini uwezekano wa kuchukua fomu ni mkubwa.
"Ni kweli huenda nikachukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge, lakini kwanza naangalia upepo unavovuma," alisema Hamad na kuongeza:
"Chama changu bado hakijafungua milango ya kuchukua na kurejesha fomu. Ukitaka kufanya jambo lolote lazima upime upepo kama ni mzuri ndio unafanya, kwa hiyo bado napima."
Hamad amejijengea jina na sifa katika siasa za Tanzania kutokana na nafasi yake ya kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni kwa umakini na umahiri mkubwa kwa miaka mitano iliyopita.
Pia, ni mmoja mwa wabunge wa upinzani ambao wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuisimamia kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Hatua ya kujitosa kwa Hamad kwenye kinyang'anyiro hicho, kunasababisha kuwepo ugumu kwa mgombea atakayesimamishwa na CCM licha ya kuwa na wabunge wengi, wamegawanyika kwenye makundi.
Hamadi ameshika nyadhifa mbalimbali nchi kabla ya mfumo wa vyama vingi kurejea mwaka 1992, zikiwemo Naibu Waziri wa Fedha na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
do.net
source Mzalen
 
Chadema tutamchagua huyu

kikwete+lipumba+seif+3.JPG
 
Yes anaweza kuongoza lakini si mnaujua muundo wa bunge letu? halina demokrasia kwa maana wabunge wa CCM watampigia mtu wao hata kama wanajua hana uwezo wa kuongoza
 
Yes anaweza kuongoza lakini si mnaujua muundo wa bunge letu? halina demokrasia kwa maana wabunge wa CCM watampigia mtu wao hata kama wanajua hana uwezo wa kuongoza

Ni kweli kabisa umenena Mkuu, hata CHADEMA wapo wapiganaji kama akina Baregu, Marando, Kahigi na wengineo wengi. Tatizo ni uwingi wa wabunge wa ccm ndiyo kitakachofanya CHADEMA wasimteue mtu.
 
sidhani kama mafisadi watamwachia maana trhis time wana hasira na upinzani hasa chadema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom