MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wahenga walisema, Vita vya panzi furaha ya kunguru na wengine walisema hasira ya mkizi furaha ya mvuvi!
Uamuzi wa CUF kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar unaofanyika Machi 20 mwaka huu unapelekea kukinufaisha CHAMA kipya cha siasa nchini, Alliance for Democratic Change (ADC), ambacho kwa sasa kinakaribia kuweka historia mpya ya kisiasa Zanzibar endapo mgombea wake wa urais, Hamad Rashid Mohamed, atafanikiwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Ikumbukwe kuwa, kwa takribani miaka 30 iliyopita, Hamad Rashid alikuwa swahiba wa kisiasa wa aliyekuwa mgombea urais wa CUF, Seif Shariff Hamad, kabla ya kutofautiana mwaka 2010.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Zanzibar, chama kilichoshinda katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kama chama hicho kimepata walau asilimia kumi ya kura za Urais zilizopigwa au chama chochote cha upinzani kilichotokea cha pili kwa wingi wa viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi.
Kwa kawaida, chaguzi zilizopita za Zanzibar zilikuwa na upinzani mkali; huku tofauti kati ya mshindi na aliyeshindwa ikiwa ni chini ya asilimia tano na katika hali ya kisiasa ya sasa ya Zanzibar, vyama hivyo viwili ni CCM na CUF. Lakini, kujitoa kwa CUF kwenye uchaguzi huo (na hiyo ni kama itabaki hivyo hadi Machi 20 mwaka huu), Zanzibar inaweza kujikuta ikiwa na Makamu wa Rais kutoka katika chama ambacho hakikuwa kinapewa nafasi ya kupata wadhifa huo.
Hamad Rashid ni mzaliwa wa Wawi, Pemba na ni mmoja wa wanasiasa wakongwe walio katika vyama vya upinzani hivi sasa. Amewahi kuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Wawi.
Alijenga jina lake akiwa miongoni mwa waliokuwa wakifahamika kama “The Young Turks”, ambalo lilikuwa ni kundi la wanasiasa vijana na wenye elimu waliopata fursa ya kusomeshwa na kupata maarifa wakati wa uongozi wa Rais Aboud Jumbe Mwinyi wa Zanzibar.
Wakati wa enzi ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume, watu hawakuruhusiwa kusoma kufikia kiwango cha chuo kikuu visiwani humo (ikielezwa kuwa wahafidhina walikuwa na hofu ya wasomi) na amri hiyo iliondolewa wakati wa Jumbe.
Hamad Rashid Mohamed na Seif Shariff Hamad walikuwa miongoni mwa vijana ambao hatimaye waliunga mkono hatua ya Jumbe kuvuliwa urais na nyadhifa zake zote kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar na mara kwa mara walikuwa wakielezwa kutoelewana na wahafidhina wa Mapinduzi ya mwaka 1964 kama vile Kanali Seif Bakari, Abdallah Natepe, Said Washoto na Brigedia Yusuf Himidi.
Mwishoni mwa miaka ya 1980, Hamad na Maalim Seif walifungwa pamoja jela kwa madai ya kupanga njama za kuipindua Serikali ya Rais Idris Abdul Wakil na wote walipotoka jela walikuwa waanzilishi wa umoja ulioitwa KAMAHURU uliokuja kuzaa CUF baadaye.
Wakati Maalim Seif alijenga ngome yake ya kisiasa Zanzibar, Hamad mara nyingi alikuwa akitafuta uhusiano na kutengeneza mtandao wa chama hicho Tanzania Bara na mara nyingi ilikuwa ikionekana kuwa yeye ndiye aliyekuwa namba mbili ndani ya CUF.