Hamad Rashid Kulindwa na FFU kwao Wawi Pemba; hii inamaana gani kisiasa?

Panapofuka moshi......................................................................
 
kuweni wapevu kisiasa maalim seif na pinda ni viongozi wakuu wa serikali wana haki ya kulindwa na kupigiwa vingora kama ilivyo taratibu zetu za nchi,mbunge hana prevelage hio hii inaonesha wazi kwamba huyu ni kibaraka wa ccm na huo mkutano uliandaliwa kwa hela za ccm kama ambavyo walikuwa wanafanya kampeni pemba walijua hawana wafuaci walichokuwa wanafanya walikuwa wanakuja na meli mbili toka unguja na magari yote ya serikali pemba yalilazimisha kuja mkutanoni ili waonekane na wachukuliwe na vyombo vya habari,ukweli ni kwaba hao waliompokea hamad asilimia 95 si wakazi wa wawi wala wanachama wa cuf bali wa ccm toka sehem mbali mbali ili kutoa image ya utakatifu wa hamad ila ukweli ni kwamba hamad rashid amejinyea na maji ya mgao kusafishika ni ngumu .atafute kazi si kuwadanganya wapemba hawa hawadanganyiki na vijisenti licha ya umaskini wao hilo hata hamad rashid analijua.

ushauri achana na siasa tafuta nyavu ukavue chaza pemba

Unaandika kwa fikra binafsi zaidi.....unalazimisha watu waamini kile unachofikiri na kuamini Wewe binafsi, unaandika kinadharia zaidi, ni Kama ile hadithi taaamu ya kufikirika siasa haiko hivyo, imagination zako zinasukumwa zaidi na chuki binafsi AMA Fitna AMA kuna wanaokutumia kwa interest zao.
Sasa basi, hebu thibitisha kuhusu hizo meli zilizotoa watu Unguja to Pemba only for hiyo meeting......vp kuhusu polisi kugomea maandamano ya kutoka airport hadi kiwanjani kulikofanyika huo mkutano? Kati ya maalim SEIF na Hamad Rashid nani yuko serikalini.....nani anarungu la kumchapa mwenzake hapo?..........unajua lililofanyika hadi polisi ikaridhia kutoa huo ulinzi? Majimbo ya Pemba Ni madogo na hata wakazi wake c wengi kiasi inavyotamkwa, lakini serikali ina majukumu mengi zaidi ya kasimamia mikutano. sasa basi umetokea wapi hadi unathubutu kuandika uongo mkubwa kiasi hiki.......eti magari yote ya serikali Pemba yalienda katika mkutano wa hamad rashid......hivi unaakili timamu Wewe? Kulikuwa kuna kitu gani hasa hadi serikali iridhie kutoa magari yoooooote Pemba nzima eti tu kwa sababu Mbunge HR Moh'd ana kwenda JIMBONI Kwake.
Jitizame kwa umakini zaidi na elewa unaloandika humu JF wanaosoma Ni watu wazima wenye akili zao timamu.
 
Maana yake salama yake iko ndani ya muungano. Hatujawahi kuona ulinzi wa namna hii awapo Dar. Aachane kabisa na kauli zake zinazoashiria kuvunja muungano ingawa hatuuhitaji.

Nani kauli zake Ni za kuashiria kuvunja muungano?! Unajua Kilio cha HRashid CUF?! Ushajiuliza Ni kwa nini maalim SEIF hakuwahi kufanya mkutano hata mmoja wa kampeni bara katika uchaguzi wa 2010? Vipi kuhusu kauli ya HR ya Mgao wa fedha ndani ya chama CUF katika uchaguzi huo? Kwamba Zanzibar yenye wakazi wasiofikia hata milion1 walijitengea zaidi ya million 500 kwa kampeni za SEIF sharif na Lipumba akatengewa milioni70 azunguke tanzania bara yenye wakazi zaidi ya milion40 kuomba urais!! Inawezekana vp hapo? Sijaenda kwny sq.km hapo Ni idadi tu ya watu.......nani mwenye muonekano wa kuvunja muungano.
Acha kuandika non sense.
 
Bahamadi usijifiche,hatwebu tochi kukujua!!!
 
Kwa kweli mimi siyo mfuasi wa CUF lakini kwa hii ya Bahamadi inaonyesha dhahiri kwamba ule ulikuwa ni bonge la mchezo mmoja wa kuigiza. Yaani escort, mbwembwe pamoja na sare ya fulana nyeusi zimeandikwa virus - ha ha haaaaa!

Uzuri wa Wapemba ukienda na pochi la kutosha utapata wafuasi, iwe CCM, Chadema au chama chengine cho chote kile.
 
Bahamadi usijifiche,hatwebu tochi kukujua!!!

Usiwe Na fikra fupi kiasi hicho kifauongo...huyo bahamadi wako kaa ukijua kuna watu wanamsapoti......hasa Sisi wa huku bara a.k.a 'Tanganyika'(najua umefurahi zaidi kwa mimi kutumia neno hili)
Halafu NINYI ndo wanafiki wenyewe unajidai kumuita bahamadi bahamadi na nina hakika hadi mizinga unampiga akiwa pande hizo (coz lazima uko Karibu naye) lakini ndio wa kwanza kumnanga......hivi ile haki sawa kwa wote iko wapi pale Chuki'Ubinafsi'na'Fitna a.k.a chama cha kisultani?!!
 
Rejea mchango wa Hamad Rashid baada ya hotuba ya waziri kivuli wa sheria na katiba kuhusu muswada wa katiba mpya then utafute maana ya hilo neno kwenye bold!

Sihitaji kufika kwny mchango wa bahamadi wenu!! Ninachoweza kukuambia Ni kwamba Kama Umeisoma vizuri post yangu niliyokujibu then Ishu ya nani anavunja AMA anataka muungano uwepo ishajijibu. Acha ushabiki na Kama Ni kweli kuna jipya kwny huo mchango uweke hadharani watu wasome.....sio wote waliopo JF wanaaccess or even idea ya wapi watapata huo mchango wake after hiyo hotuba ya Waziri kivuli.
Jipange.
 
a.k.a chama cha wachaga,chama wagala
Usiwe Na fikra fupi kiasi hicho kifauongo...huyo bahamadi wako kaa ukijua kuna watu wanamsapoti......hasa Sisi wa huku bara a.k.a 'Tanganyika'(najua umefurahi zaidi kwa mimi kutumia neno hili)
Halafu NINYI ndo wanafiki wenyewe unajidai kumuita bahamadi bahamadi na nina hakika hadi mizinga unampiga akiwa pande hizo (coz lazima uko Karibu naye) lakini ndio wa kwanza kumnanga......hivi ile haki sawa kwa wote iko wapi pale Chuki'Ubinafsi'na'Fitna a.k.a chama cha kisultani?!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom