Hamad Rashid amuumbua Maalim Seif; agoma kuhojiwa!

Katika maelezo yake, Hamad amesema kuwa mojawapo ya tuhuma inasema kuwa yeye(Hamad) amefadhiliwa fungu la fedha na Mbunge wa Monduli, EL, ili azitumie kukisambaratisha chama cha CUF!
NI SARAKASI YA AINA YAKE NDANI YA CUF!
 
Hamad Rashid amegoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CUF kuhusu tuhuma zake za ‘uasi’ katyika CUF. Ameyatamka hayo mbele ya waandishi wa habari leo.

Amesema sababu ni kwamba kamati hiyo haipo kikatiba (katiba ya CUF), hana imani na wanakamati, na kwamba tayari ameshahukumiwa kabla hata ya kwenda mbele ya kamati

Anasema Maalim Sewif baada ya kufanya ziara Pemba na kwingineko bara na visiwani na kufanya vikao na watendaji wa chama, alimuandikia barua M/Kiti Prof Lipumba kwamba “kwa mawazo ya wengi aliyopata, ni kwamba Hamadi Rashidi afukuzwe kutoka chama.”

Kuna mengine mengi kayasema ambayo Ch 10 bulletin ya 7pm ilimkatiza.

Nawasilisha.

Duh! Kumbe ni kweli Maalim ana mambo ya kichiini chini hivyo? Mbona sasa anajipaka tope?
 
Kama ni kweli Maalim Seif alifanya hivyo, basi alikuwa na ajenda ya siri dhidi ya HR. Nilifikiri Maalim ni mtu wa busara, kumbe... au kisha onjeshwa na magamba?

naona sasa anajimaliza mwenyewe. Nawasikitikia CUF bara, sijui nani atawatetea, maana Mtatiro kisha viukwa kilemba cha kipemba. Too sad!

Seif atajimaliza mara mbili? Ndiyo maana safari za ghafla huku bara -- kumbe alikuwa anapandikiza chuki?
 
Kwa kuwa Seif amemua kumuua jamaa kisiasa namshauri Hamad aumwage hadharani waraka wa Seif ili tuone kilichoandikwa kwenda ka m/kiti wa cuf ndipo tutamwamini kuwa ni mwanamapinduzi wa kweli
 
Seif atajimaliza mara mbili? Ndiyo maana safari za ghafla huku bara -- kumbe alikuwa anapandikiza chuki?
Kazi imeanza rasmi, na kama ni game ndiyo kwanza mbichi kabisa, ngoja tusubiri next episode tuone nini kitatokea, ila kuna tofauti gani kati ya Maalimu seif na madikteta wengine duniani kama Gadaffi, Ben Ali, Mubaraka wanaong'ang'ania madaraka kwa muda mrefu?

Ushauri wangu kwa Maalimu Seif; achia madaraka kabla wananchi hawajakuchoka, miaka 4 iliyobaki yakunywa whisky na kuku ikulu inakutosha ikichukulia wewe ni mgonjwa; I remember umekaa miezi 3 Middle East kwa matibabu,
 
Na tofauti iko wapi na kardinali Pengo ambaye tangu nimalize shule jina ni lake tu?.
 
Kwa kuwa Seif amemua kumuua jamaa kisiasa namshauri Hamad aumwage hadharani waraka wa Seif ili tuone kilichoandikwa kwenda ka m/kiti wa cuf ndipo tutamwamini kuwa ni mwanamapinduzi wa kweli

YESSSSSSS!!!!! Aumwage hadharani. Lakini mwenye kutaka kujua fitina za Maalim, si aende akamuulize Abud Jumbe? Yuko hai bado.
Huyu mjamaa (seif) nilimpenda sana huko nyuma lakini sasa sijui kitu gani kimemuingia -- ni yule mdudu 'king'ang'anizi cha madaraka?"
 
Hapana. Nadhani Maalim anachukuwa sana ushauri wa Lyatonga -- ndo sababu.
 
Na ni rahisi sana kuhisi serikali ya CCM iko upande gani katika bifu hili. Upande wa Maalim of course. Hivyo HR ana kamlima hapo, hawamagamba kazi yao kubwa ni kuchukuwa upande katika vyama vyenye mgogoro, na mara zote hujikita upande ule wa wanaompinga kipenzi cha walio wengi.

Mgogoro wa NCCR wa 1996 serikali ilijikita upande wa akina Marando na kundi lake.

Ni mtazamo tu.
 
Seif ana umri gani wakuu?

Walio karibu yake wamshauri huyu mzee wetu apumzike ajiongezee japo siku za kuishi badala ya blood pressure ya HR na nguvu mpya ya vijana
 
Na tofauti iko wapi na kardinali Pengo ambaye tangu nimalize shule jina ni lake tu?.
Kuna watu humu wanawashwa makalio, Pengo anahusika nini na Topic hii? usivamie vitu usivyovijuwa cardinal Pengo ni successor wa Cardinal Rugambwa, na Cleric leader sio uongozi wa kisiasa maamuma mkubwa wewe!!
 
YESSSSSSS!!!!! Aumwage hadharani. Lakini mwenye kutaka kujua fitina za Maalim, si aende akamuulize Abud Jumbe? Yuko hai bado.
Huyu mjamaa (seif) nilimpenda sana huko nyuma lakini sasa sijui kitu gani kimemuingia -- ni yule mdudu 'king'ang'anizi cha madaraka?"
'king'ang'anizi cha madaraka+tonge
Viongozi wetu wengi, aliye masikini huingia kwenye siasa kupata mlo bila jasho na aliye tajiri hujiongezea kwa migongo ya Watanzania.
 
Laana ya kuwadharau watanzania na kuungana kuwakandamiza watanzania na mume wao CCM...hakika watavuna walichopanda! Huyu Hamad Rashid ndiye alikuwa mtoa hoja kuwa CHADEMA ni chama cha vurugu wakati wa kupitisha mswada wa mabadiliko ya katiba...
 
Back
Top Bottom