Zanzibar 2020 Hamad Masoud Hamad wa ACT-Wazalendo aliyedaiwa kutekwa, afikishwa Kituo cha Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Mpanga mikakati ya ushindi wa chama cha ACT-Wazalendo, Hamad Masoud Hamad, anayedaiwa kutekwa leo asubuhi Visiwani Wete, Pemba, amefikishwa kituo cha Polisi cha mji huo.

Inaelezwa kuwa Hamad, ambaye ni mtaalamu wa mawasiliano na takwimu, alitekwa leo alfajiri na watu wanaodaiwa kuwa maofisa wa Idara ya Usalama, wakati akiwa uwanja wa ndege wa Wete.

Inaelezwa kuwa akiwa uwanja huo wa ndege alivamiwa na watu asiowafamu na kumwamuru kuondoka eneo la uwanja huo na kuongozana nao.

Nje kidogo ya uwanja walimuingiza kwenye gari na kutokomea kusikojulikana. Gari lililombeba ni aina ya Landrover. Namba za usajili za gari hilo hazikufahamika mara moja, kwani ghafla baada ya kumbeba Hamad liliondoka kwa kasi.

Mashuhuda wanaeleza kwamba Hamad, alipiga kelele, lakini alizibwa mdomo na mmoja wa watekaji hao.

Inaelezwa kuwa Hamad ndiye "kiongozi mkusanya taarifa zote za kura" kuanzia kesho na siku ya kupiga kura kwa Umma, Oktoba 28, Jumatano ya kesho kutwa.

Tayari viongozi wa juu wa ACT -Wazalendo wanakutana muda huu mjini Zanzkbar na taarifa rasmi itatolewa kuhusu kutekwa kwa mtendaji wao.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Pemba, Omar Ali Shehe ameithibitishia JamiiForums kwamba kiongozi wao alitekwa na kwamba baada ya kufuatilia wamepata taarifa yupo kituo cha Polisi.

Amesema hana taarifa za sababu za kukamatwa kwake, ingawa tangu Jana kulikuwa na tetesi za kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho cha upinzani.

Shehe amesema baada ya kufuatilia kwa karibu, wamegundua kwamba kuwepo kwa viongozi wengi Watano wa juu wa chama hicho visiwani Pemba.

JamiiForums imeambiwa na kiongozi mmoja wa Polisi Pemba kwamba watu hao sita wanashikiliwa kwa kuhojiwa kuhusu masuala kadhaa. Hakuwa tayari kuweka wazi mazungumzo hayo yanahusu nini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo na kuomba waulize "wakubwa" kutoka Zanzibar.

Simu ya msemaji wa Polisi imekuwa ikiita tu bila kupokelewa.
 
Nina wasi wasi hali ya hewa itachafuka sana Zanzibar kwa vitendo hivi vinavyo endelea. Hivi hakuna ustarabu wa kumwita mtu kituo cha polisi au kumkamata kwa heshima hadi iwe vurumai? Haya Kamnda Sirro anasemaje matendo ya vijana wake? Aaaah jibu litakua "Taarifa za intelligencia zinaonyesha........"
 
Halafu watu wanasema tuwaombee, inchi gani hii ya kutishana hivi mapadri na mashekhe hamuyaoni haya, kwa Nini tusimuone shehe ponda Kama mkombozi
 
Inaelezwa kuwa Hamad ndiye "kiongozi mkusanya taarifa zote za kura" kuanzia kesho na siku ya kupiga kura kwa umma, Oktoba 28, Jumatano ya kesho kutwa.

Kazi ya ZEC na NEC hiyo, majanga mengine huwa mnayachokonoa wenyewe!
 
Mpanga mikakati ya ushindi wa chama cha ACT-Wazalendo, Hamad Masoud Hamad, anayedaiwa kutekwa leo asubuhi Visiwani Wete, Pemba, amefikishwa kituo cha Polisi cha mji huo.

Inaelezwa kuwa Hamad, ambaye ni mtaalamu wa mawasiliano na takwimu, alitekwa leo alfajiri na watu wanaodaiwa kuwa maofisa wa Idara ya Usalama, wakati akiwa uwanja wa ndege wa Wete.

Inaelezwa kuwa akiwa uwanja huo wa ndege alivamiwa na watu asiowafamu na kumwamuru kuondoka eneo la uwanja huo na kuongozana nao.

Nje kidogo ya uwanja walimuingiza kwenye gari na kutokomea kusikojulikana. Gari lililombeba ni aina ya Landrover. Namba za usajili za gari hilo hazikufahamika mara moja, kwani ghafla baada ya kumbeba Hamad liliondoka kwa kasi.

Mashuhuda wanaeleza kwamba Hamad, alipiga kelele, lakini alizibwa mdomo na mmoja wa watekaji hao.

Inaelezwa kuwa Hamad ndiye "kiongozi mkusanya taarifa zote za kura" kuanzia kesho na siku ya kupiga kura kwa Umma, Oktoba 28, Jumatano ya kesho kutwa.

Tayari viongozi wa juu wa ACT -Wazalendo wanakutana muda huu mjini Zanzkbar na taarifa rasmi itatolewa kuhusu kutekwa kwa mtendaji wao.

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Pemba, Omar Ali Shehe ameithibitishia JamiiForums kwamba kiongozi wao alitekwa na kwamba baada ya kufuatilia wamepata taarifa yupo kituo cha Polisi.

Amesema hana taarifa za sababu za kukamatwa kwake, ingawa tangu Jana kulikuwa na tetesi za kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho cha upinzani.

Shehe amesema baada ya kufuatilia kwa karibu, wamegundua kwamba kuwepo kwa viongozi wengi Watano wa juu wa chama hicho visiwani Pemba.

JamiiForums imeambiwa na kiongozi mmoja wa Polisi Pemba kwamba watu hao sita wanashikiliwa kwa kuhojiwa kuhusu masuala kadhaa. Hakuwa tayari kuweka wazi mazungumzo hayo yanahusu nini kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo na kuomba waulize "wakubwa" kutoka Zanzibar.

Simu ya msemaji wa Polisi imekuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Najaribu kuwaza tu "kama vile tunaenda kutengeneza wakimbizi!? Kama vile rasmi tunaelekea kwenye kutoaminiana!? Kama vile vitisho na mauaji kitakuwa kitu cha kawaida!? Nazidi kuwaza sipati picha maisha baada ya uchaguzi huu yatakuwaje!??? Ubabe... ubabe..!!! Faida yake nini? Walipoandika "usitupe taka ndipo utakuta jaa limefurika!!"
Reconciliation.... kabla mambo hayajazidi kuharibika zaidi
 
Back
Top Bottom