Hamad awafanya watanganyika wawachukie wazanzibari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad awafanya watanganyika wawachukie wazanzibari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bams, Feb 9, 2011.

 1. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,585
  Likes Received: 2,972
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi hasira ya Watanganyika ni kubwa juu ya Hamad, Mzanzibari aliyeamua kushirikiana na CCM kuzuia mabadiliko yoyote ambayo watanganyika wanayataka katika Taifa lao.

  Ukweli ni kuwa vyama vikuu vya siasa kwa Zanzibar ni CCM na CUF, licha ya kwamba vyama vingine kama CHADEMA, NCCR, UDP, n.k. navyo vipo Zanzibar. Hivi vyama vingine kwa upande wa Zanzibar vinajitambua kuwa siyo popular, na ndiyo maana CUF kule Zanzibar inafanya mambo yake bila kuvishirikisha hivi vyama vingine vya upinzani kwa namna yoyote ile. Hivi vyama vingine vinaifahamu nafasi yao kule Zanzibar, na ndiyo maana hata pale CUF wanapofanya mambo yao kama vile hakuna vyama vingine vya upinzani, hatujasikia jitihada za hali ya juu za kukwamisha malengo na mipango ya CUF kule Zanzibar. Kinachoshangaza kwa upande wa Hamad Rashid, ni kwa nini busara ya namna hiyo hana inapokuja kwa masuala ya mwungano?

  Kwa upande wa Tanganyika vyama vikuu vya siasa ni CCM na CHADEMA. Hivi ndivyo vyama vinavyoungwa mkono na Watanganyika walio wengi. Kwa nini Hamad, asiye Mtanganyika, baada ya kufanya anayoyataka kule Zanzibar bila ya kuingiliwa na Mtanganyika yeyote, awe na ujasiri wa kuja kuzuia matakwa ya Watanganika zaidi ya milioni 43? Huyu Hamad amekosa hekima, staha na busara ambayo binadamu yeyote mstaarabu alistahili kuwa nayo.

  Serikali inayotamkwa kuwa ni ya mwungano, kiutendaji ni serikali ya Tanganyika. Wazanzibar wana serikali yao na bunge lao kule Zanzibar ambalo kila siku wanapitisha mambo yao yote wanayoyataka bila ya kuingiliwa na Mtanganyika yeyote, na tena wakihojiwa kidogo wanapokiuka katiba ya Mwungano wanakuwa wakali sana.

  Mambo yanayojadiliwa kwenye bunge la Mwungano, zaidi ya 95% yanahusu Tanganyika lakini mbunge wa Zanzibar anayewakilisha wazanzibari 5,000 anampinga mbunge wa Sengerema anayewakilisha Watanganyika 800,000. Mbunge huyo huyo anayewakilisha wazanzibari 5,000 anapewa posho, VX na kila kitu na serikali ya Mwungano, huku diwani wa Tanganyika anayewakilisha watanganyika 100,000 hapewi hata pikipiki. Mbaya zaidi, mbunge kama Hamad ambaye anapata kisicho stahili yake bado anakuwa kikwazo kwa wale wanaomfadhili.

  Tukiacha porojo na misemo ya kiswahili kuwa umoja ni nguvu, hivi Tanganyika inafaidika nini kuwa katika kiini macho hiki cha mwungano, zaidi ya maudhi yanayofanywa na Wazanzibari dhidi ya Watanganyika? Tunatumia gharama kubwa kuishi katika mwungano usio na faida. Gharama tunazozipata ni pamoja na kuhudumia ofisi ya makamu wa Rais ambayo hatuhitaji, wabunge wa Zanzibar; na mbaya zaidi ni sychological cost ambayo kila mara tunasababishiwa na Wazanzibari kama hili la kuingilia masuala yasiyowahusu huku kule kwao wamefanya bila kuingiliwa. Hawa akina Kafulila, Lipumba, Mrema, ni haki yao kuingilia maumuzi yeyote ya Tanganyika lakini siyo Hamad na wabunge wenzake wa Zanzibar kutaka kutuamulia sisi Watanganyika wakati wao tumewapa haki hiyo kule kwao Zanzibar.

  Wabunge Wazanzibari washiriki kutoa hoja kuhusiana na wizara zile za mwungano tu na si vinginevyo.

  Ifike wakati Watanganyika tutoe kauli juu ya hawa Wazanzibari ambao wameanza kupitiliza mipaka ya uvumilivu. Tuliungana kwa kuamini kuwa umoja huo ungetusaidia, na hasa wakati wa vita baridi. Kama hatuwezi kutaja faida tunazozipata Watanganyika kwa kuungana na Zanzibar lakini tukaweza kuorodhesha hasara, basi mwungano huu hauna utashi.

  Ninachojiuliza hasa ni kuwa huyu Hamad Rashid ni nani kwa Watanganyika, na Tanganyika inamhusu nini yeye kama Mzanzibari? Pesa tunayotaka matumizi yake yadhibitiwe na upinzani, Zanzibar inachangia kiasi gani? Wizi mkubwa wa fedha ya serikali hutokea kwenye miradi ya barabara, kwenye Halmashauri, kwenye ujenzi wa shule, miradi ya maji, n.k. Wizara zote zinazosimamia mambo hayo siyo za mwungano, na Wazanzibari wanazo zao kule kwao. Sasa kwa nini Hamad anataka atuamulie juu ya mbunge gani wa upinzani awe mwenyeketi wa kamati za bunge wa kusimamia haya?

  Wazanzibari wakiendelea na fitina dhidi ya Watanganyika, nina hakika Watanganyika wengi tutataka serikali tatu kwaajili ya majaribio, tukiona wanazidi kutuchokonoa, tutawaachilia, tuendelee nao kama majirani zetu na siyo kama wanandoa.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Nilishawachukia hata kabla ya kumfahamu Hamad!
   
 3. N

  Nonda JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kwa nini unawachukia watanzania wenzetu?
  Au jina la Tanzania limetuchosha sasa?
  Bila ya wazanzibari na Zanzibar yao hatuna Tanzania ,umelisahau hili?

  Wakiondoka hawa, ubaguzi na chuki utaanza miongoni mwetu. Kuna hotuba Mwalimu alitoa kuhusu dhambi ya ubaguzi..kwa faida yako itafute..
  Mimi naona huu muungano tuufanyie marekebisho uwe muungano wa haki na usawa...hapo tu ndio penye kasoro,,, nchi nyingi duniani huungana ili kupata manufaa na nguvu...pengine hata aina ya mfumo wa muungano wetu tuubadili ,uwe mfumo wa shirikisho.
   
 4. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jitahidini basi tuanze mapema hayo majaribio ya serikali tatu. Hahaha kidume hamad rashid kinawasumbua sio? Hamad rashid ni gwiji la siasa atawaendesha sana tu.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hamad wote wawili (mkubwa na mdogo) ni wabinafsi sana. hawaitakii mema nchi hii.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wala siwahitaji mkuu na sijutii kutowahitaji, kuhusu kuwa na tz wala siihitaji Tanzania naihitaji Tanganyika yetu. kwanini Muungano uwepo na Zanzibar iwepo wakati Tanganyika haipo? Iweje iwepo serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika isiwepo? Kwanini turuhusu mama mmoja aolewe na wanaume wawili na kumzuia mwingine asiolewe na wawili? Think about it, kama ni kuufurahia umoja sawa tu but tunachowapa wazanzibar tuwape pia watanganyika.

  Kama unafuatilia mkuu jaribu kufuatilia bei ya umeme zenji ulinganishe na na tunaolipa Hapa Bongo ingawa umeme wao unatoka huku, fuatilia kama kuna mgao balaa kama tunaoupata hapa bongo Fuatilia sheria juu ya mfungo wa ramadhani inasemaje kwa kwasio waislamu na ulinganishe na sheria za TANGANYIKA kisha nambie kama muungano upo kweli? Fuatilia mapato ya utalii na mengine toka zenji yanaingia wapi na mapato ya madini na utalii hapa TANGANYIKA yanakuwa shared namna gani kisha nambie kama kiuhalisia kuna muungano?

  Ni juzi tu kwenda zenji lazima mtu wa bara awe na kibali kwenda but mzeji kuja huku kulikuwa hakuna kuulizwa kisha nambie kam muungano tunao kweli?
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana kwamba masuala ya uendesheaji wa serikali ya bara ubaki na wabara si huyu Hamad aje ashikilie madaraka yanayohusu uendeshaji wa mambo yetu ya wabara. Nilishangaa kwa nini anang'ang'ania mambo ya bara kwa nini wamemnyima uwaziri huko Zanzibar?

  Nasema pamoja na tofauti tulizo nazo kati ya vyama CCM na Chadema bado wabunge wetu wameonyesha mshikamano katika kumtolea nje huyo Hamad bila kuchaguliwa kati ya kamati za bunge. Na kafulila aliyetekwa na Hamad kaambulia yasiyomhusu kwa kuacha uzalendo.
   
 8. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Cha msingi naona tuvunje tu huu muungano na tanzania ife... kila watu wafanye mambo yao kwa amani... Hakuna haja ya kuogopa eti mwl. alisema kwani tunaweza kuisimamia nchi yetu na tutafanya hivyo.... Kama wazenji mnapenda sana muungano kaunganeni na comoro!!! :twitch:
   
 9. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Mtabe wewe nae punga nini Hamad kidume hajui hata kutype na computer analilia pesa njaa inamsumbua kama wewe tu, hana lolote yule anasubiri posho tu. hajali nchi hii ina umasikini gani mana sio mwenzetu yeye ni mpemba.
   
 10. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Tafuteni Tanganyika yenu. Si mliiuwa wenyewe. Hakuna TANZANIA BILA YA ZNZ. Vunjeni Muungano . Wazanzibari hatuna haja nao.
   
 11. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna upuuzi kama huo. Zanzibar is of great strategic importance to Tanzania and it is above all a very beautiful place. Hatuwezi ichukia au kutengana nayo kisa Hamad or anyone. Chechnya yenyewe inawaumiza warusi lakini hawaiachii. How can we give up a part of our territory... ni upuuzi.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Tunaelekeza lawama sehemu au kwa mtu ambaye siye alituletea hali hii.
  Natumai unafahamu ni nani aliifuta serikali ya tanganyika kinyemela, na kuliuwa bunge la Tanganyika na pia kufuta jina Tanganyika.... In bold jina la Mwalimu linajitokeza.. au umesoma historia ipi wewe mkuu?

  kama hatujamtambua adui vipi tutaweza kupambana naye?

  Wabunge wetu wanaotoka Tanganyika na Rais wetu anayetoka Tanganyika ndio wametuundia shida hii, hawa ndio wa kuwa-force waturejeshee Tanganyika yetu na serikali yetu na bunge letu...Is this difficult to understand?
  Vyenginevyo tuna-misplace our blames! na kufanya ukombozi wetu kuwa mbali zaidi na mgumu kwa sababu tunalenga shabaha "wrong target"
   
 13. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Muungano hauna maana yoyote zaidi ya wao kutunyonya tu, na bado wanaendelea na ubaguzi wao vilevile.inauuma sana wanavyopendelewa kwenye huduma ya muhimu kama umeme
   
 14. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :A S thumbs_down:
  Oooppssss!!!! Hamad Rashid.......just one meaning tagged to your name.....Mlafi kutoka Pemba...that is all about you


  Is your concious still clear and positive na unaridhika sasa kuona umevuruga bunge hasa upande wa upinzani? Is it part of your gaddem mwafaka with mafisadi kudhoofisha na bunge la bara??

  Je ndio walikuambia ukubali kukosa uwaziri visiwani ili utumike vizuri huku Bara kudhoofisha upinzania bungeni? Your just a coward and like Kunguru wa Kwenu huko
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa Tanganyika wamelala usingizi wa pono hawana mbele wala nyuma itakuwaje wakubali kuongozwa na mbunge kutoka nhi jirani ya Zanzibar bado kidogo tutawaita wooot wabunge Kata,hawana walilonalo zaidi ya ujinga tuuu,munapitishaje kitu kinachoua demokrasia kwa ajili ya kufurahisha wahamiaji kutoka nchi jirani
   
 16. S

  Selungo JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKUU HESHIMA MBELE!

  Kama wananchi wa Sudan wameamua kuigawa nchi yao na kupatikana Sudan ya Kusini na Sudan ya Kaskazini, kuna hasara gani na sisi Watanzania tukauvunja muungano uliopo na nchi yetu Tanganyika irudi? Mbona mimi binafsi licha ya kufundishwa na kuisoma elimu ya siasa tangu enzi za mwalimu sijaona faida ya muungano huu zaidi ya changu ni chetu na chao ni chao? Nadhani kwa uwiano uliopo ambao si sawa kiuchumi na ki- idadi ya wananchi, si sahihi wengine kufaidi jasho la wenzao wakati jasho lao hawataki wenzao waliguse.

  Kilichoonyeshwa na Hamad Rashid ni kielelezo tosha wa siasa za kizandiki na zenye lengo la kuhakikisha kwamba wanaendelea kufaidi kile wasicho kitolea jasho. Hivi ni kwa nini tunawang'ang'ania wakati walishasema hawautaki muungano? Kama ni mafuta, mbona tangu miaka nenda rudi hayajavunwa na shughuli zinaendelea kama kawaida?

  Kuanzia sasa sihitaji na wala sitaki kusikia habari ya muungano. Taitamani tanganyika niliyo isoma kwenye somo la historia ya Tanganyika enzi hizo.
   
 17. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Amezungumza fact. wao wanafanya visa hata kwa mjasilia mali mdogo wa bar kwa kuichoma moto. na wao wanafikiri wana akili kuliko sisi kwa kuendeleza ajenda zao. wana ajenda kubwa sana na hasa ya udini. wabunge wa ccm hawajui kinachoendelea kwa ajili ya uvivu wao wa kufikiri. hawa cuf wa znzbr hawana haki ya kutuamulia maisha kwa namna yoyote.
   
 18. L

  Libaba Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katiba ya wananchi inakuja tunataka Tanganyika yetu yenye maziwa na asali.
   
 19. M

  Mwera JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyie malimbukeni chadema hamumuwezi hamad hata mfanyeje anauzoefu wasiasa zaid ya miaka 30,kwa taarifayenu alikua mwanasheria mkuu wa serkal zaid yamiaka 10,sasa mnataka kumshindanisha nahao mambumbumbu wenu wa cdm?na bado chamoto mtakiona mpk muwe na adabu kwa wakubwazenu.
   
 20. M

  Mwera JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kalagabaho we nyamaza!je namakamo wako wa raisi ni mkimbizi kutoka nchi jirani?soma katiba na jaribu kufatilitia japo kidogo sheria za nchiyako ili upunguze umbumbumbu japo kidogo uache kuropoka pumba.
   
Loading...