Addis Ababas
JF-Expert Member
- Aug 5, 2018
- 351
- 353
Wafutiwe ruzuku... Chadema ndo mwasisi wa "siasa biashara," commercial politics. Mbowe akiona mtu yeyote anayeweza kumuongezea ruzuku, anafanya kila namna ampate. Wakati ni sasa, wasipewe ruzukuNi ubora duni wa wanasiasa pamoja na mpangilio hovyo wa vyama vyetu. CCM ina mtindo ambao uliigwa na vyama vingine. Yaani ukiwa Mkiti basi wewe ni yote. Unafuta na kuingiza watu wapya upendavyo. Kwa CCM labda tusema ni uraibu wa chama Kimoja, sasa CDM, UDP, TLP imekuwaje nao wanakuwa na abosolute power kwa wengine?
Namkumbuka Cheyo akisema, ".... Jidulamabambasi, OUT!" Akifukuza wanachama kama wapangaji wake. Leo hii Mbowe anatuhumiwa wizi/matumizi hovyo ya chama na mali zake, yeye kimya! Haoni sababu ya kujibu kwa kuamini ni chama chake, yeye ni supreme. Lipumba anaachisha watu uanachama, watu kimya na wengine wanalazimika kujikomba ili awapende.
Swali ni je, Tuendelee kulea wanasiasa kwa kodi zetu wakati ubora wao ni duni kiasi hiki?