Halotel, huu ni utapeli? Sielewi kinachoendelea

Sam Drive

Member
Dec 27, 2020
22
32
Siku ya tarehe 17.7.2021 nilitoa pesa kimakosa kwa kukosea namba ya wakala.

Nikapiga simu wakasema wanashughulikia irudi. Nisubri masaa 72. Baada ya masaa hayo message ikaingia kwamba pesa imerudishwa kwa wakala.

20210803_090950.jpeg


Sasa baada ya hapo nimeendelea kupiga simu majibu yanayotoka ni

1. Kusubiri masaa 72 kutokea tarehe hiyo tarehe 17 imagine masaa 72 yamepita mangapi mpaka leo August 3

2. Nimekwenda kwenye ofisi zao kufuatilia wakaniambia ndani ya masaa mawili hiyo hela itakuwa imerudi. Nikapewa namba ili isipokuwa imerudi nipige. Ila hiyo namba haikupokelewa mpaka leo

3. Customer care namba 100 mpaka sasa hawapokei simu yangu.

Nachotaka kujua kwamba halotel pesa yangu mmenitapeli au wiki zaidi ya mbili mnanisumbua na simu yangu mmeacha kupokea.

Kama halotel wamo humu naomba mtu anisaidie kuwatag.

HALOTEL MNA CUSTOMER CARE MBOVU SANA
 
Dawa ni kwenda hukohuko ofisini kwao, mimi mwenyewe hiyo namba ya customer care haijawaigi kupokelewa
 
Huduma za pesa ni bora uwe unatumia m- pesa,
Halotel ukitaka kutuma pesa mda mwngine jina la mtu unaetaka kumtumia halifik kuna jamaa alikosea kutuma elf 50 akapiga huduma kwa wateja hakupew majib yanayoeleweka
 
Kwanza waingize commission zetu kwa sisi mawakala za Mwezi huu...naona kimya mpaka sasa hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom